Rais Samia Suluhu Hassan

  • Shangwe la wafanyakazi baada ya nyongeza ya mishahara kutoka kwa Mheshimiwa Rais

    “Wafanyakazi mambo ni moto, mambo ni fire,” ni maneno aliyoyatumia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhitimisha hotuba yake ya Mei Mosi 2023 ambayo ilijaa matumaini kwa maelfu ya watumishi wa umma waliokuwa wameujaza uwanja wa Jamhuri Morogoro wakimsikiliza. Miongoni mwa mengi yaliyowafurahisha watumishi hao ambao wameendelea kushuhudia mabadiliko makubwa kwenye mazingira ya kazi na maslahi yao chini ya Rais Samia ni uamuzi wa Rais kurejesha nyongeza ya mishahara ya kila mwaka, ikiwa ni miaka saba tangu kuondolewa kwa mfumo huo. Itakumbukwa kuwa Mei 2022 Rais Samia aliridhia nyongeza ya mishahara ambapo alipandisha kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3, ambapo TZS trilioni 1.59 zilitumika kwa ongezeko hilo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Aidha, mbali na kurejesha utaratibu huo, Rais amesema kuwa nyongeza ya posho ambayo ilipandishwa mwaka jana lakini baadhi ya watumishi hawakuanza kuipata kwa sababu bajeti za taasisi zao tayari zilishapitishwa, wataanza kupata fedha hizo mwaka wa fedha ujao. “Tumejiandaa pia kupandisha madaraja, vyeo vitaendelea kupandishwa, kutenganisha makundi na madaraja mserereko wale ambao hawakupata mwaka jana watapata mwaka huu” ameahidi. Pia, alisema Serikali anayoiongoza itaendelea kuwekeza na kuvutia uwekezaji nchini, ili kujenga uchumi na kuzalisha ajira kwa Watanzania na zipatikane fedha za kuboresha maslahi ya watumishi. Read More

  • Umoja wa Mataifa: Tanzania ya tatu kwa kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi Afrika

    Licha ya kuwa ukuaji wa bara la Afrika unatarajiwa kushuka kutoka asilimia 4.1 mwaka 2022 hadi asilimia 3.8 mwaka 2023, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua zaidi huku Umoja wa Mataifa (UN) ukiitaja kuwa ni nchi ya tatu barani Afrika kwa kuwa na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi mwaka 2023. Tanzania ambayo inaendelea kuwa mfano Afrika kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, inatarajiwa kushuhudia ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.6, ikitanguliwa na Ivory Coast ambayo uchumi wake utakua kwa asilimia 6.5 pamoja na Rwanda itakayoshuhudia ukuaji wa asilimia 7.8. Mafanikio hayo ni matokeo ya mikakati ya Rais Samia ambapo katika miaka miwili ya uongozi wake amesajili miradi ya uwekezaji ya TZS trilioni 17, ambayo imechochea ukuaji wa sekta nyingine pamoja na kutoa fursa za ajira kwa maelfu ya Watanzania. Mikakati hiyo pia imewezesha uchumi kukabiliana na changamoto za dunia kama mfumuko wa bei, gharama kubwa za ukopaji na mabadiliko ya tabianchi. Wakati ripoti ya UN ikionesha hivyo, Benki ya Dunia (WB) imeitaja Tanzania kuwa nchi ya 10 kwa utajiri barani Afrika kwa kwa kuzingatia Pato Ghafi la Taifa (FDP) kwa kuangalia viwango vya sasa vya kubadili fedha. Ukuaji huo mbali na kuendelea kuboresha maisha ya Watanzania lakini pia unawapa imani wawekezaji waliopo na wanaokusudia kuwekeza nchini, kwa kuwafanya waamini Tanzania ni sehemu salama kuwekeza mitaji yao ya mabilioni, hivyo kufanya uchumi kukua zaidi na zaidi. Read More

  • Miaka miwili ya Mama: Uwekezaji wa trilioni 17 wazalisha maelfu ya ajira

    Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi Januari 2023 Serikali imesajili miradi ya uwekezaji 537 yenye thamani ya TZS trilioni 17, ikiwa ni matokeo mazuri katika mkakati wa Mheshimiwa Rais wa kukuza biashara na uwekezaji nchini. Ongezeko la usajili wa miradi hiyo linatarajiwa kutoa ajira takribani 92,770 ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kuandikishwa katika kipindi chochote tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961. Hatua alizochukua Rais Samia kuboresha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kuimarisha Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja na maboresho ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania zimevutia wawekezaji wapya, zimetatua changamoto zilizokuwa zikiwakabilia wafanyabiashara na kuvutia wawekezaji na kurahisisha utoaji huduma. Aidha, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) imesajili miradi 38 yenye thamani ya TZS bilioni 327.7 na mauzo nje yenye thamani ya TZS bilioni 448.2. Miradi hiyo ni mahsusi katika sekta zinazozalisha bidhaa zitokanazo na kilimo, bidhaa za viwandani, bidhaa za mifugo, bidhaa za kemikali, bidhaa za madini na bidhaa za misitu. Kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji nchini kunakuza mzunguko wa fedha nchini, kunajenga imani ya wawekezaji waliopo pamoja na kuvutia uwekezaji zaidi. Read More

  • Rais Samia afungua fursa: Mchango wa Diaspora wavuka trilioni 2

    Moja ya mikakati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoiweka wazi baada ya kuingia madarakani ni kutoa fursa zaidi kwa Watanzania waishio nje kushiriki katika shughuli za maendeo na kijamii nchini kwa kuweka mazingira yatakayowawezesha kufanya shughuli zao nchini. Mafanikio yameendelea kuonekana ambapo kwa mwaka 2022 pekee diaspora walituma nchini TZS trilioni 2.6, na pia wamewekeza kupitia ununuzi wa nyumba na viwanja wenye thamani ya TZS bilioni 4.4 na ununuzi wa hisa za TZS bilioni 2.5. Ili kupanua ushiriki wa diaspora katika maendeo ya Tanzania Serikali inatarajia kuwa imekamilisha mfumo wa kidigitali wa uandikishaji wa diaspora Juni mwaka huu ili kuwezesha ukusanyaji endelevu wa takwimu zao. Mbali na kutuma fedha na kuwekeza nchini, diaspora pia huchangia ukuaji wa uchumi kwa kutangaza fursa za kiuchumi, biashara, utalii na uwekezaji zinazopatikana nchini. Mchango mwingine ni kuleta mitaji, utaalam na teknolojia ambavyo huchangia katika kukuza uzalishaji wa mazao, bidhaa na huduma mbalimbali zenye tija kiuchumi. Hadi sasa idadi ya diaspora wa Tanzania ni milioni 1.5, idadi ambayo Rais anaamini itakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi ikiwekewa mazingira rafiki. Read More

  • #MiakaMiwiliYaMama: Amewajengea vijana uwezo wa kujiajiri kupitia kilimo

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anadhihirisha kwa vitendo kauli yake aliyotoa kuwa hataki kuingia katika historia ya kuwa mmoja wa wanaowalaumu vijana kuwa hawajiajiri, badala yake anawawekea mazingira wezeshi ya kujiajiri kupitia kilimo ambapo lengo ni kuzalisha ajira milioni 3, kipaumbele kikiwa vijana na wanawake. Machi 20 mwaka huu amezindua mashamba ya pamoja (Block Farms) zaidi ya ekari 12,000 ambazo zitagawawiwa kwa vijana, kila mmoja kwa ukubwa usiozidi ekari 10, pia alizindua ndege zisizo na rubani, mashine za umwagiliaji na magari kwa ajili ya maafisa wa wilaya ili kuhakikisha vijana popote walipo nchini wanapata usaidizi wa kitaalamu katika kufanya kilimo cha kibiashara. Katika azma ya kukifanya kilimo kuwa cha vijana, ameahidi kuendelea kutenga bajeti mahsusi kwa ajili ya watendaji kwenye sekta ya kilimo ili shughuli zote zifanyike kwa usasa kuanzia uzalishaji hadi uuzaji mazao na bidhaa. “Tunasema ni kilimo cha vijana, hivyo vijana wawepo shambani, wawepo kwenye utaalamu, wawepo kwenye kuendesha mitambao, sehemu zote kuwa na vijana wanaokwenda kwenye sekta ya kilimo,” amesema akizindua programu ya Building a Better Tomorrow. Katika miaka miwili ya uongozi wake, kilimo ni moja tu ya njia anazotumia kumwinua kijana wa Kitanzania na kukabiliana na changamoto ya ajira inayoisumbua dunia. Ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika kila wilaya, mikopo ya halmashauri, kuboresha mazingira ya biashara hasa kwa wajasiriamali ni maeneo mengine ambayo yametoa ajira kwa vijana wengi. Read More

  • Una miaka kati ya 15 hadi 35? Bofya hapa kuona fursa kutoka Serikalini

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anafungua fursa zaidi za mafunzo ya ufundi ikiwa ni moja ya njia za kukabiliana na changamoto ya ajira nchini hasa kwa vijana na wanawake. Hapa chini ni tangazo la fursa za mafunzo kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambayo yanatolewa bure na Serikali katika vyuo 28 nchini. Hapa chini ni fomu ya kutuma maombi; Read More

  • Nishati ya Uhakika ni Uhuru: Mheshimiwa Rais anavyovipa vijiji vya Tanzania Uhuru

    Maendeleo ya Watanzania na maendeleo ya nchi yanategemea sana upatikanaji wa nishati ya uhakika, na kwa kulitambua hilo, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katika miaka yake miwili ya uongozi ameendelea kuimarisha sekta hiyo ambayo imefungua zaidi fursa za kiuchumi kwa wananchi, ushuhuda wa karibuni ukiwa ni wananchi wa Kigoma walioanza kunufaika na umeme wa gridi ya Taifa ambao ni wa uhakika zaidi kuliko uliokuwa ukizalishwa kwa majenereta. Katika muktadha huo huo wa kuwawezesha wananchi, Serikali imesaini mikataba ya utekelezaji wa miradi mikubwa mitatu ya kupelekea umeme zaidi vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA), miradi ambayo itagusa sekta za kilimo, afya, maji, viwanda vidogo na madini. Mradi wa kwanza (Ujazilizi 2B) ambao utafikisha umeme katika vitongoji 1,522 ambao utaunganisha umeme kwa wananchi zaidi ya 88,000. Mradi wa pili unapeleka umeme kwenye migodi na maeneo yenye shughuli za kilimo 336 yaliyopo katika mikoa 25 ya Tanzania Bara. Mradi huu utawapunguzia gharama (fedha na muda) za uchimbaji madini wachimbaji wadogo, utazalisha ajira zaidi, utawawezesha kutumia teknolojia ya kisasa, utachochea ukuaji wa sekta ya madini pamoja na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa. Aidha, kwa kufikisha umeme katika maeneo yenye shughuli za kilimo kunaendana na lengo la Serikali la kuifanya Tanzania kuwa kapu la chakula kwa Afrika, kwa kuvutia vijana kufanya kilimo cha kibiashara. Umeme utasaidia katika umwagiliaji na uongezaji thamani wa mazao. Mradi wa tatu unahusisha kupeleka umeme katika vituo vya afya 63 na pampu za maji 333 vijijini katika mikoa 25. Kufika kwa nishati kwenye maeneo hayo kutaboresha utoaji huduma za afya, mathalani nyakati za usiku, kutapunguza vifo vya mama na mtoto, na kuwezesha upatikanaji huduma nyinginezo zinazohitaji umeme. Wakati huo huo, uwepo wa umeme unaosukuma maji katika pampu utahakikisha vijiji vinakuwa na maji ya uhakika, hatua ambayo itakuza usafi na kupambana na magonjwa ya mlipuko, lakini pia itapunguza muda wa… Read More

  • Mheshimiwa Rais Samia apongezwa kila kona kwa kuongeza ‘boom’ vyuo vikuu

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wanafunzi wa elimu ya juu nchini kwa kuongeza fedha za kujikimu kutoka TZS 8,500 HADI TZS 10,000, kauli ambayo iliibua shangwe huku wanafunzi wakiimbia “tuna imani na Samia,” pamoja na kupiga makofi ya furaha. Wakati wanafunzi hao wakishangilia kwa aamuzi huo uliokonga nyoyo zao, Rais Samia amesema ombi lao la wanafunzi wa ngazi ya stashahada na astashahada kupatiwa mikopo litawekewa mipango kwanza. “Kwa kazi tunazozifanya sasa hivi na hali ya bajeti, hili bado hatujafikia huko, kwa hiyo tunalifikiria, tunaliweka kwenye mipango yetu,” amesema Rais Samia huku akieleza amemuagiza waziri wa fedha aangalie uwezekano wa kupata fedha, akifanikiwa atamuongezea nyingine ili wananchi hao wanufaike. Wakati hayo yakiendelea, Rais Samia ameeleza mikakati ambayo Serikali yake inachukua kuwawezesha wahitimu kujiajiri pindi wanapohitimu masomo yao ikiwa ni pamoja na mapitio ya mitaala na kuhimiza elimu na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. “Tunataka elimu isiwe chanzo cha changamoto ya ajira, bali itoe suluhisho […] Ndio maana tumejielekeza sana sasa kwenye elimu ya TEHAMA ili vijana muweze kujiajiri wenyewe,” amesema Rais Samia. Wanafunzi wa elimu ya juu wakiwakilishwa na viongozi wao wamemshukuru Rais Samia kwa hatua ambazo ameendelea kuchukua kuboresha elimu ya juu nchini ambapo wameanza kuona matokeo. Read More

  • Nafasi mpya za ajira Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuongeza nafasi za ajira katika taasisi mbalimbali za Serikali ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi. POST: ASSISTANT LECTURER (ACCOUNTING) – 1 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: ASSISTANT LECTURER (ENVIRONMENTAL ECONOMICS) – 1 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: ASSISTANT LECTURER (ENVIRONMENTAL ECONOMICS) – 1 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT- CLINICAL NUTRITION AND DIETETICS – 5 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT-NURSING MANAGEMENT AND EDUCATION – 2 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT -BIOSTATISTICS – 1 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT -EPIDEMIOLOGY – 1 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT -PHARMACOLOGY – 1 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT -PSYCHIATRY – 2 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT -PARASITOLOGY – 1 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT (CHINESE LANGUAGE) – 3 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply POST: TUTORIAL ASSISTANT- CLINICAL NUTRITION AND DIETETICS – 5 POST Employer: The University of Dodoma (UDOM) More Details 2023-02-04  Login to Apply   Read More

  • Mheshimiwa Rais Samia achochea mabadiliko kwenye vyombo vya dola ili kulinda haki za wananchi

    Akiendelea kufanya vizuri kwenye mageuzi ya kiuchumi na kisiasa, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amegeukia sekta ya haki ambapo leo amezindua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai ili kuhakikisha zinatoa haki kwa wananchi wa wakati na kwa misingi ya kisheria. Taasisi ambazo zinakwenda kufanyiwa maboresho ni Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Jeshi la Magereza pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Wakati wa mapitio tume hiyo itaangalia masuala mbalimbali kwenye taasisi husika ikiwa ni pamoja na mifumo ya utendaji, mafunzo, mifumo ya ajira, matumizi ya TEHAMA, fikra za kiutendaji na mahusiano kati ya taasisi hizo na raia. Katika maboresho hayo Rais Samia anelenga kukomesha vitendo mbalimbali ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa na wananchi ikiwa ni pamoja na mamlaka husika kuwabambikia kesi, kucheleweshwa kwa upelelezi, msongamano mkubwa wa mahabusu magerezani, kupambana na rushwa pamoja na kuimarisha uwezo wa taasisi hizo katika kulinda na kutetea maslahi ya nchi kwa kuhakikisha ajira zinatolewa kwa mujibu wa sheria na kunakuwepo mafunzo ya mara kwa mara. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema “hakuna kitu kibaya duniani kukichepusha kama haki ya mtu,” na hivyo kama ambavyo hakuna atakaye haki yake ipokonywe, vivyo hivyo anatakiwa kuhakikisha hashiriki katika upokonyaji wa haki ya mwingine. Read More