Rais Samia Suluhu Hassan
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali anayoiongoza inatambua na kuthamini mchango wa wachimbaji wadogi katika kuzalisha ajira nchini, na ameahidi kuwa ataendelea kuwaunga mkono kwa kuboresha mazingira ya uchimbaji pamoja na biashara ya madini ili waweze kuboresha maisha yao na kuchangia kwenye uchumi wa taifa. Ametoa ahadi hiyo leo wakati akizindua vifaa vya uchimbaji madini vilivyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambapo ni pamoja mitambo mitano ya kuchoronga, ambayo inatarajiwa kuongezwa kufikia 15 ifikapo Juni 2024. Mitambo mingine ni mitambo 10 ya kutwanga mawe yanayoaminika kuwa na dhahabu, mitambo mitatu ya kuzalisha mkaa mbadala pamoja na makontena ya kusambaza mkaa huo na magari ya STAMICO. Mitambo hiyo ambayo itatumiwa na wachimbaji wadogo nchi nzima itawapunguzia gharama, mfano mtambo wa kuchoronga sasa utakodishwa kwa bei nafuu ikilinganishwa na gharama ya TZS 375,000 ambayo walitozwa na wamiliki binafsi kwa kuchoronga kwa kila mita moja. Mitambo ya kutwanga mawe itaongeza uwezo wao kutoka tani 2 za sasa kwa siku hadi tani 12 kwa siku. Kununuliwa kwa mitambo hiyo ni mwendelezo wa mikakati ya serikali kuwainua wachimbaji wadogo ambapo hatua nyingine zilizochukuliwa ni kufutwa kwa kodi ya ongezeko la thamani ya asilimia 18 pamoja na kodi ya zuio ya asilimia 5 kwa wachimbaji wadogo watakaouza madini yao kwenye masoko ya ndani ya nchi. Kama haitoshi, serikali pia imetoa punguzo la asilimia mbili la mrahaba pamoja na kuondoa asilimia 1 ya ada ya ukaguzi wa madini kwa wachimbaji wa dhahabu ambao wengi wao ni wachimbaji wadogo. “Hii ina maana wale watakaouza dhahabu kwenye viwanda hivyo watapata punguzo la asilimia tatu ya tozo za serikali kwenye mauzo ghafi ya madini yao,” amesema Mheshimiwa Rais Samia akiongeza kuwa hatua hizo ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoielekeza serikali kubuni na kuendeleza mikakati ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo kufanya shughuli zao kwa… Read More
-
Doha- Qatar: Oktoba 2 mwaka huu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki uzinduzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Mboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) ambayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kujifunza na kuwekeza katika kilimo, hususani kwenye teknolojia rafiki ya mazingira. Kazi kubwa ya kuimarisha sekta ya mboga na matunda inayagusa moja kwa moja maisha ya vijana na wanawake ambao ndio wanufaika wakubwa wa ajira takribani milioni 6.5 zinazotokana na sekta, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa familia na taifa kwa ujumla. Ushiriki wake kwenye jukwaa hilo la kimataifa ni mwendelezo wa mageuzi ya kilimo aliyoyaanzisha nchini ambapo Serikali ya Tanzania kupitia taasisi zake mbalimbali na sekta binafsi inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutafuta masoko ya mazao ya kilimo pamoja na kuvutia uwekezaji kwenye sekta hiyo iliyoajiri zaidi ya asilimi 65 ya Watanzania. Mkakati wa Mheshimiwa Rais ni kuona kilimo kinakuwa kwa wastani wa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030, ambapo mbali na kufungua fursa za masoko kimataifa, hatua nyingine za kimkakati alizochukua kutimiza lengo ni pamoja na upatikanaji wa mbegu bora, miundombinu ya umwagiliaji, utafiti na upatikanaji wa mbolea nafuu na viuatilifu. Juhudi hizi zinalenga kupunguza gharama za uzalishaji kwa mkulima na kuongeza tija na uzalishaji, kuimarisha usalama wa chakula nchini na kuiwezesha Tanzania kuuza chakula nje, ikiendelea ushiriki wake katika kuongeza usalama wa chakula duniani na kutunza mazingira kwa wakati mmoja. Read More
-
Dar es Salaam, Tanzania – Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uchumi wa nchi, ambapo sasa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imechukua hatua kubwa ya kimkakati ya kununua dhahabu ya ndani ili kuimarisha hifadhi ya fedha za kigeni na kuongeza nguvu ya shilingi ya Tanzania. Tayari BoT inanunua dhahabu kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa ndani kwa kutumia shilingi ya Tanzania ambapo tayari imenunua kilogramu 418, lengo likiwa ni kununua kilogramu 6,000 katika mwaka wa fedha 2023/24. Hatua hii muhimu ina manufaa mbalimbali kwa taifa na wananchi kwa kununua dhahabu kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni, taifa letu linajikinga dhidi ya athari zitokanazo na mabadiliko ya ghafla (kutokuwepo kwa uhakika) ya kiuchumi wa kimataifa. Dhahabu imekuwa kimbilio la thamani kwa miongo mingi wakati wa migogoro ya kiuchumi na kisiasa duniani. Kwa hivyo, kwa kuchanganya dhahabu katika akiba ya fedha za kigeni, Tanzania inaweza kusaidia kulinda thamani ya shilingi ya nchi wakati wa mazingira magumu ya kiuchumi duniani. Pia, hatua ya kununua dhahabu kutoka kwa wazalishaji wa ndani kutachangia kukuza uchumi wa ndani kwani itachochea uzalishaji wa dhahabu. Kukua kwa uzalishaji kunaenda moja kwa moja na kuongezeka kwa ajira, kwani shughuli za uchimbaji na biashara ya dhahabu zinahitaji wafanyakazi, na pia ongezeko la wachimbaji litanufaisha sekta nyingine zinazofungamana na sekta hiyo ikiwemo ya huduma (chakula, maji, nishati, mawasiliano). Uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania wa kununua dhahabu kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni na kulinda uchumi unathibitisha nia ya serikali ya kusimamia utulivu wa kiuchumi na kujenga nguvu za kifedha, hatua ambayo inaweza kuwa na athari chanya kwa maendeleo na ustawi wa nchi. Read More
-
Tanzania imeendelea kutekeleza sera yake ya Diplomasia ya Uchumi inayolenga kujenga na kuimarisha uhusiano wake wa kimataifa na kujenga mahusiano ya kibiashara na kiuchumi na taasisi pamoja na mataifa mengine ili kuchochea maendeleo. Historia nyingine imeandika baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kushiriki na kuhutubia katika Mkutano wa 15 wa BRICS (Brazil, Russia, India, China, South Africa) ambalo ni jukwaa la nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi duniani ambapo pato la Taifa la mataifa hayo ni quadrilioni TZS 63.3, ambapo pia kutokana na kupokea wanachama wapya sita, kuanzia Januari 2024 nchi sita kati ya tisa zinazozalisha mafuta zaidi duniani zitakuwa mwanachama wa jukwaa hilo. Kwa kushiriki kwenye mkutano huo, Tanzania itapata manufaa makubwa kiuchumi na kibiashara kwani kunaiwezesha kujenga mahusiano ya kiuchumi na biashara na nchi hizo zenye nguvu hatua inayoweza kufungua fursa mpya au kupanua fursa zilizopo za kuuza bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya nchi hizo, na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi. Ni wazi pia kuwa mataifa ya BRICS yamepiga hatua kwenye teknolojia, hivyo Tanzania inaweza kujifunza matumizi bora ya teknolojia katika kurahisisha utoaji huduma na kuchochea maendeleo. China ambayo ni mwanachama wa BRICS ni mshirika mkubwa maendeleo wa Tanzania ambapo kwa miezi saba ya mwaka 2023 imeongoza kwa uwezekaji (Foreign Direct Investment) nchini ikiwekeza mtaji wa zaidi ta TZS trilioni 1.2 ambao pamoja na mambo mengi utazalisha ajira kwa maelfu ya Watanzania. Katika mkutano huo Rais Samia alipata nafasi ya kuzungumza na Rais wa China, Xi Jinping, ikiwa ni mara nyingine kwa viongozi hao kukutana baada ya ziara ya Rais Samia nchini China. Mazungumzo hayo huenda yakaongeza uwezekano wa kufadhili miradi muhimu kama miundombinu, nishati, kilimo, na teknolojia, uwekezaji pamoja ushirikiano wa kiusalama. Katika dunia ya sasa, nchi haiwezi kujitenga kama kisiwa, inailazimu kutoka, kukutana na kushirikiana na mataifa mengine ili kufanikisha masuala mbalimbali… Read More
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameianzisha safari itakayoshuhudia mageuzi makubwa ya mashirika ya umma, taasisi na wakala za Serikali ikiwa ni utekelezaji wa maono ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere pamoja na kuziwezesha taasisi hizo kujiendesha kwa tija na ufanisi ili kupunguza utegemezo kutoka Serikalini. Mageuzi hayo yametokana na uhalisia kuwa licha ya wingi wa mashirika na wakala hizo (248) ambazo Serikali imewekeza mtaji wa TZS trilioni 73, bado mchango wake kwenye uchumi ni mdogo sana, kwani kwa sasa taasisi hizo zinachangia asilimia 3 tu kwenye bajeti ya Serikali, huku nyingi zikitegemea ruzuku ili kujiendesha. Mheshimiwa Rais ameeleza kuwa maono ya Mwalimu Nyerere kuanzisha mashirika ya umma alitaka yamilikiwe na wananchi wenyewe kupitia hisa na kwamba wananchi washirikishwe kwenye masuala ya mashirika hayo, na hivyo ameagiza hatua zichukuliwe ili kurudi kwenye msingi huo. “Kwa kuwa kwa sasa wapo wananchi wenye uwezo wa kununua hisa, hata kama ni kidogo kidogo, nadhani turejee kwenye mwelekeo huo,” ameagiza. Ili kufikia malengo hayo, Mheshimiwa Rais ameridhia mabadiliko mbalimbali ambayo ni pamoja na kutoa uhuru kwa taasisi kujiendesha katika mambo ya msingi, kufanya maboresho katika taratibu za ajira kwa watumishi wao na katika sheria ya ununuzi wa umma, na kuongeza kusiwepo kwa kuingiliwa kisiasa kwenye utendaji wa taasisi hizi. Pia, Serikali ipo kwenye mchakato wa kutunga sheria itakayobadili hadhi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kuwa Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma, na kuangalia uwezekano wa kuanzishwa kwa Mfuko wa Uwekezaji wa Umma ili kuondoa utegemezi kutoka mfuko mkuu wa Serikali. Kutokana na uchunguzi uliobaini uwepo wa taasisi ambazo majukumu yake yanashabihiana au hayana umuhimu kwa sasa na zile ambazo zinalega lega Serikali itaziunganisha au kutatua changamoto zao ziwezeshe kujiendesha kwani mashirika hayo ni muhimu kwa uchumi zikiwa zinatoa asilimia 17 ya ajira zote nchini. Amewatoa hofu watumishi kuwa mabadiliko yatakayofanyika hayataathiri ajira zao… Read More
-
Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) limeipongeza serikali ya Tanzania kwa kuimarisha utulivu wa kiuchumi wakati ambapo dunia ilikuwa inapitia changamoto mbalimbali ikiwemo janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), vita vya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya tabianchi. Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bo Li baada ya kumaliza ziara yake nchini ambapo amesema “jitihada za haraka za serikali ya Tanzania zilisaidia kudhibiti mfumuko wa bei na kulinda uchumi dhidi ya athari za vita nchini Ukraine.” Licha ya mafanikio hiyo, taasisi hiyo imeihimiza Tanzania kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo yatakuza uwezo wa Serikali katika kugharamia huduma za kijamii na kuongeza uwekezaji katika elimu, afya, maji na sekta nyingine muhimu. Li akizungumza na wawakilishi wa sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo ameeleza kuvutiwa sana na nguvu na uhai wa uchumi wa Tanzania. Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika zenye kiwango cha chini zaidi cha mfumuko wa bei ambapo kwa miezi sita mfululizo umekuwa ukishuka kutoka asilimia 4.9 Januari hadi asilimia 3.6 Juni mwaka huu. Read More
-
Wakuu wa nchi za Afrika, viongozi wa ngazi mbalimbali na wadau wengine wamekusanyika Tanzania kujadili mustakabali wa rasilimali watu barani Afrika ambapo Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu ametumia jukwaa hilo kueleza hatua mbalimbali ambazo Tanzania imezichukua kuimarisha sekta hiyo ambayo ni pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya afua mbalimbali za lishe na huduma za afya ya uzazi wa mama na mtoto. Hatua nyingine ni kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na elimu ili kuondoa udumavu ambao, mara nyingi, hupunguza kiwango cha uelewa na uwezo wa kusoma kwa waoto na kuhakikisha watoto wanaandaliwa kimwili, kiakili, kiisimu/kijinsia kiubunifu na kiakili-hisia. Aidha, Serikali imetoa afua kwa kaya masikini, inatoa elimu bila malipo kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha sita, inapanua elimu ya ufundi na mafunzo ya amali, imefuta ada kwa baadhi ya vyuo vya ufundi, imeanza kutoa mikopo kwa vyuo vya kati, inatoa mikopo kwa vijana, inaruhusu waliokatisha masomo kurejea shule pamoja na kuweka mkakati wa kuvutia vijana kwenye kilimo, yote haya yakilenga kuongeza mchango wao kwenye uchumi. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022, vijana ndio kundi lenye watu wengi zaidi nchini Tanzania, hivyo hatua ambazo Rais ameeleza kuwa Tanzania imezichukua kwa asilimia kubwa zimewalenga vijana kwani anaamini kwamba maisha bora ambayo vijana wengi hukimbilia Ulaya kuyafuata yanaweza kupatikana barani Afrika endapo Serikali zao zitawawezesha. “Viongozi wenye maono hujenga sera zao kwenye maendeleo ya watu na kufuatiwa na maendeleo ya vitu,” amesema Rais Samia akitoa wito kwa viongozi wenzake wa Afrika na kusisitiza kwamba Afrika haitoweza kuendelea endapo rasilimali watu isipoendelezwa. Read More
-
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi ya uwekezaji 229 yenye thamani ya TZS trilioni 4.5 kati ya Januari hadi Juni mwaka huu, ambapo lengo ni kufikia miradi 400 ifikapo Desemba 2023. Idadi hiyo inadhihirisha kasi kubwa ya usajili wa miradi nchini ikilinganishwa na miradi 293 iliyosajiliwa mwaka 2022, hivyo kusajili asilimia 78 ya miradi hiyo ndani ya nusu mwaka ni mafanikio makubwa kwa nchi. Kusajiliwa kwa miradi hiyo inayotoa ajira zaidi ya 30,000 kwa Watanzania katika sekta mbalimbali ni matokeo ya sera ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, ikiwemo kuboresha sheria, kupunguza tozo/kodi mbalimbali na kuimarisha amani na utulivu. Aidha, takwimu zinaonesha mkakati huo wa Rais umefanikiwa zaidi kwani kwa miaka sita ya Serikali ya awamu ya tano, jumla ya miradi ya TZS trilioni 45 ilisajiliwa, huku miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita ikisajili miradi ya trilioni 22 ndani ya miaka miwili, takwimu zinazoonesha kuwa itafanya vizuri kuliko awamu iliyopita. Aidha, sababu nyingine ni taasisi 12 za usimamizi kuwa katika jengo moja hivyo kurahisisha utoaji huduma pamoja na matumizi ya TEHAMA yaliyorahisisha utoaji wa leseni na vibali mbalimbali vya biashara na uwekezaji hasa kupitia dirisha ya kielektroniki ambapo mwekezaji sasa anaweza kuwasilisha maombi akiwa popote dunia Read More
-
Kwa mara ya kwanza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza hadharani kuhusu suala la uwekezaji na uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na sekta binafsi akisisitiza kuwa ni mihimu kama nchi tukatumia fursa zinazojitokeza kabla hazijaondoka au kukwapuliwa na washindani wetu, wakati tukibaki kulumbana. Ametoa rai hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwaapisha viongozi aliowateua karibuni, mmoja wao akiwa ni Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo na kumueleza kwamba moja ya majukumu yake ni kuangalia changamoto na fursa zilizopo nchini ili zitumike vizuri kwa manufaa ya Watanzania. “Wakati sisi tunalumbana, bandari apewe nani, iende, isiende, wenzetu kwa kuona malumbano yetu wame-jump [kimbilia] wamekwenda kule kule […] sasa muone jinsi fursa zinavyokuja na kukimbia haraka haraka, na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia haraka haraka,” amesema. Amesema kazi kubwa iliyopo nchini ni kuleta mabadiliko, lakini kwenye nia safi ya kujenga nchi mabadiliko yanakaribishwa na kwamba licha ya kuwa watu hawajazoea, kwa kwenda nao taratibu na kadiri watakavyoendelea kuona matokeo, watazoea. Kupitia uwekezaji unaokusudiwa bandarini, Tanzania inalenga kuongeza uwezo wa bandari kufadhili bajeti ya nchi kw asilimia 30, kuzalisha ajira zaidi ya 70,000, kuongeza mapato ya Serikali, kupunguza muda wa kuhudumia meli, kuongeza uwezo wa bandari kupokea meli kubwa na kuifanya bandari hiyo kukidhi viwango vya kimataifa. Read More