September 2023

  • BoT kununua dhahabu inathibitisha nia ya Serikali kuimarisha utulivu wa kiuchumi

    Dar es Salaam, Tanzania – Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uchumi wa nchi, ambapo sasa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imechukua hatua kubwa ya kimkakati ya kununua dhahabu ya ndani ili kuimarisha hifadhi ya fedha za kigeni na kuongeza nguvu ya shilingi ya Tanzania. Tayari BoT inanunua dhahabu kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa ndani kwa kutumia shilingi ya Tanzania ambapo tayari imenunua kilogramu 418, lengo likiwa ni kununua kilogramu 6,000 katika mwaka wa fedha 2023/24. Hatua hii muhimu ina manufaa mbalimbali kwa taifa na wananchi kwa kununua dhahabu kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni, taifa letu linajikinga dhidi ya athari zitokanazo na mabadiliko ya ghafla (kutokuwepo kwa uhakika) ya kiuchumi wa kimataifa. Dhahabu imekuwa kimbilio la thamani kwa miongo mingi wakati wa migogoro ya kiuchumi na kisiasa duniani. Kwa hivyo, kwa kuchanganya dhahabu katika akiba ya fedha za kigeni, Tanzania inaweza kusaidia kulinda thamani ya shilingi ya nchi wakati wa mazingira magumu ya kiuchumi duniani. Pia, hatua ya kununua dhahabu kutoka kwa wazalishaji wa ndani kutachangia kukuza uchumi wa ndani kwani itachochea uzalishaji wa dhahabu. Kukua kwa uzalishaji kunaenda moja kwa moja na kuongezeka kwa ajira, kwani shughuli za uchimbaji na biashara ya dhahabu zinahitaji wafanyakazi, na pia ongezeko la wachimbaji litanufaisha sekta nyingine zinazofungamana na sekta hiyo ikiwemo ya huduma (chakula, maji, nishati, mawasiliano). Uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania wa kununua dhahabu kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni na kulinda uchumi unathibitisha nia ya serikali ya kusimamia utulivu wa kiuchumi na kujenga nguvu za kifedha, hatua ambayo inaweza kuwa na athari chanya kwa maendeleo na ustawi wa nchi. Read More

  • Royal Tour Imejibu: Utalii waongoza katika kuingiza fedha za kigeni

    Kazi kubwa aliyoifanya na inayoendelea kufanywa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza fursa za utalii unaweza kusema ‘imejibu’ baada ya sekta hiyo kuendelea kuimarika na kupita madini ya dhahabu katika kuiingizia nchi fedha za kigeni, ikiwa ni kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne tangu ilipoanza kushuka. Mlipuko wa janga la kidunia la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO) mwaka 2019 kuliiathiri sekta hiyo ambapo mchango wake kwenye fedha za kigeni ulishuka kutoka dola za kimarekani bilioni 2.52 (TZS trilioni 6.3) mwishoni mwa mwaka 2019 hadi dola za Kimarekani bilioni 1 (TZS trilioni 2.5) mwishoni mwa mwaka 2020, na hivyo kupelekea dhahabu iliyoingiaza dola za Kimarekani bilioni 2.9 (TZS trilioni 7.2) kuongoza. Kuhakikisha sekta ya utalii ambayo inatoa ajira zaidi ya milioni 1.6, inachangia asilimia 25 ya fedha za kigeni na asilimia 21 ya Pato la Taifa inaimarika, Mheshimiwa Rais Samia alichukua jukumu la kurekodi filamu ya Tanzania: The Royal Tour ambayo ilizinduliwa nchini Marekani na hivyo kuiwezesha nchi kutangaza fursa za utalii na vivutio vya utalii kwa mamilioni ya watu dunia, hatua ambayo imepelea kuendelea kuongezeka kwa watalii kutoka ndani na nje ya nchi. Matokeo yameendelea kuonekana ambapo takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kuwa mapato yatokanayo na utalii yamepanda kufikia dola za Kimarekani bilioni 2.999 (TZS trilioni 7.5) katika mwaka ulioishia Julai 2023 kutoka dola za Kimarekani bilioni 1.95 (TZS trilioni 4.8) mwaka ulioishia Julai 2022, huku mapato ya dhahabu kwa mwaka ulioishia Julai 2023 yakiwa dola za Kimarekani bilioni 2.9 (TZS trilioni 7.3). Mafanikio hayo yametokana na kuendeleo kuongezeka kwa watalii kutoka nje ya nchi ambapo ripoti ya BoT inaonesha kuwa watalii wameongezeka kwa asilimia 37.2 kufikia 1,658,043 katika mwaka huo, idadi ambayo haijawahi kufikiwa kabla. Licha ya mafanikio haya, Mheshimiwa Rais Samia anaendelea kutangaza utalii ili kufikia lengo la watalii milioni 5 ifikapo… Read More

  • Mheshimiwa Rais azipatia ufumbuzi changamoto kubwa nne za wananchi Mtwara

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan leo Septemba 17, 2023 amemaliza ziara yake siku nne mkoani Mtwara, ziara ambayo imekuwa na mafanikio makubwa ikiendelea kuifungua Mtwara kuwa kitovu cha biashara kwa ajili ya Kanda ya Kusini pamoja na nchi jirani za Msumbiji, Malawi na Comoro. Wakati wote wa ziara hiyo Mheshimiwa Rais alikagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumzia na wananchi, ambapo walieleza changamoto kubwa nne ambazo ni suala la maji, umeme, bei za mazao pamoja na miundombinu ya usafiri na usafirishaji. Katika mkutano wake wa mwisho wilayani Masasi, ameeleza mkakati wa Serikali kutatua changamoto hizo ambazo kwa upande wa maji amesema kuwa kwa sasa mkoani Mtwara kuna miradi 66 inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ambayo inanufaisha vijiji 190, hivyo kufanya jumla ya vijiji vyenye majisafi na salama kufikia 650 kati ya vijiji takribani 750. Aidha, amesema Serikali inaendelea na uchimbaji wa visima, ikiwemo wilayani Liwale ambapo mitambo ya kuchimba visima ilianza kazi saa 24 baada ya Rais kumtaka waziri wa maji kuhakikisha changamoto ya wananchi hao inatatuliwa. Kuhusu changamoto ya umeme, Mheshimiwa Rais amewaahidi wakazi wa mkoa huo baada ya miezi 18 changamoto hiyo itakuwa imekwisha kwa sababu miradi miwili mikubwa inatekeleza. Mradi wa kwanza ni wa kuunganisha Masasi kwenye gridi ya Taifa kwa kutoa umeme mkoani Ruvuma, na mradi wa pili ni kutoa umeme wilayani Ruangwa. Aidha, kwa upande wa bei za mazao, amesema mkakati wa Serikali umewezesha mazao ya ufuta na mbaazi kupata bei nzuri msimu huu na kwamba anaamini korosho nayo itauzwa kwa bei nzuri. Hata hivyo, amewahakikishia wananchi kuwa miaka miwili ijayo korosho yote utabanguliwa nchi kabla ya kusafirishwa, mkakati ambao utawanufaisha wakulima zaidi kwa kupandisha thamani zao hilo pamoja na ajira kwenye kongani ya viwanda ambayo itajengwa katika Kijiji cha Maranje wilayani Nanyumbu. Mageuzi makubwa yanaendelea kwenye upande wa miundombinu ambapo sambamba na… Read More

  • Mheshimiwa Rais Samia atoa mwelekeo mchakato wa katiba mpya

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema anatambua umuhimu wa katiba mpya kama ambavyo maoni ya makundi mbalimbali, ikiwemo kikosi kazi, yaliyotolewa na kusisitiza kuendelezwa kwa mchakato huo ambao ulikwama tangu mwaka 2014. Licha wa umuhimu huo ametahadhari kuwa upatikanaji wa katiba mpya ni mchakato na kwamba mchakato huo sio mali ya wanasiasa bali ni ya Watanzania wote, hivyo amewataka wanasiasa kutokuhodhi sauti kwenye mchakato huu. “Katiba ni ya Watanzania, awe ana chama, awe hana, awe ana dini, awe hana, awe mrefu, awe mfupi, mnene, mwembamba, mkubwa, mdogo. Kwa hiyo matengenezo yake yanahitaji tafakuri kubwa sana,” amesema Mheshimiwa Rais. Hata hivyo, amesema kuwa katiba si kitabu, bali ni misingi ya maadili, itikadi na namna ambavyo Watanzania wanakubaliana kuendesha Taifa lao, hivyo, makubaliano hayo yanaandikwa, hivyo, haiwezi kuwa sawa na nchi nyingine. “Tunaanza na elimu Watanzania wajue [katiba] ni kitu gani […] Kwa hiyo tusiwaburuze wananchi. Katiba viongozi wa kisiasa si mali yetu, ni mali ya Watanzania. Tunachokitaka kwenu ni maoni katiba iweje,” ameongeza. Aidha, ameongeza demokrasia lazima iakisi namna watu ndani ya nchi yanavyoendesha masuala yao ikiwemo tamaduni, maadili, mila, desturi, na kwamba huwezi kuchukua demokrasia kutoka nchi nyingine na kuiingiza nchini bila kuzingatia masuala ya ndani. Read More