Uncategorized

  • Watalii wafurika nchini miezi iliyotambuliwa kama ‘low season’ miaka ya nyuma

    Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu hali ya uchumi kwa Mei 2024 imeonesha kuwa watalii wameendelea kumiminika nchini ambapo miezi ya Machi na Aprili ambayo ilitambulika huko nyuma kwa kuwa na idadi ndogo ya watalii (low season), kwa mwaka 2024 watalii wa kimataifa wameongezeka kwa asilimia 21.9 na asilimia 21.8 mtawalia ikilinganishwa na miezi kama hiyo mwaka jana. Hali hii ambayo ni matokeo ya kuendelea kuimarika kwa sekta ya utalii nchini na duniani inaifanya sekta hiyo kuendelea kuwa chanzo kikubwa cha fedha za kigeni ambapo katika miezi hiyo utalii umeingiza dola za Marekani bilioni 3.58 kwa Machi na dola za Marekani bilioni 5.75 kwa Aprili kutoka dola za Marekani bilioni 2.7 na dola za Marekani bilioni 2.8, mtawaliwa kwa miezi kama hiyo mwaka jana 2023. Mafanikio haya yametokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali pamoja na sekta binafsi ikiwemo kutangaza vivutio vya utalii nje ya nchi, huduma bora kwa wageni wanaofika kutalii nchini pamoja na kuimarisha huduma za usafiri, mathalani sekta ya anga. Ripoti ya BoT inaunga mkono utafiti uliofanywa na Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) kwa robo ya Januari-Machi 2024, ambapo kwa ukuaji unaoendelea sasa wa sekta ya utalii, Tanzania ilishika nafasi ya kwanza Afrika na ya nne duniani kwa ongezeko kubwa la watalii ikilinganishwa na kabla ya UVIKO-19, yaani mwaka 2019. Mafanikio na kuimarika kwa sekta ya utalii, pamoja na sekta nyinginezo kama madini, usafirishaji, kilimo kutaendelea kuchochea ukuaji wa Pato la Taifa kufikia asilimia 5.8 mwaka huu.   Read More

  • EPUKA UPOTOSHAJI: Tanzania haijatoa bahari wala madini yake kwa Korea

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu yupo nchini Korea ambapo amekamilisha ziara rasmi na sasa anaendelea na ziara ya kikazi hadi Juni 6 mwaka huu, ambapo hadi sasa Tanzania imeendelea kunufaika na ziara hiyo kufuatia kusainiwa kwa mkataba, tamko na hati za makubaliano ambazo zitaimarisha uhusiano uliopo na kufungua fursa mpya za ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wa pande zote. Kufuatia kusainiwa kwa makubaliano hayo, kumekuwa na upotoshaji mitandaoni ambapo moja ya vyombo vya habari kimeeleza kuwa Tanzania imepokea mkopo toka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini. Balozi wa Tanzania nchini Korea, Togolani Mavura amekanusha habari hiyo akieleza kuwa Tanzania haijasaini mkataba wowote na Korea unaohusu bahari wala madini katika ziara ya Mheshimiwa Rais Samia, na kwamba katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais ameshuhudia utiwaji saini wa mkataba mmoja wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu. Mbali na mkataba huo, Mheshimiwa Rais alishuhudia utiwaji saini wa hati za makubaliano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za ushirikiano katika sekta za uchumi wa buluu na madini ya kimkakati pamoja na Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA). Amesisitiza kuwa Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandika, kwani inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu. Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028). Aidha, ameweka wazi kuwa Tanzania ni moja ya nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinazofaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF. Mkopo ambao Tanzania imeupata, tofauti na ilivyopotoshwa na chomho hicho, ni mkopo wa masharti nafuu na una riba ya asilimia 0.01,… Read More

  • Mama Yuko Kazini: Miradi ya uwekezaji yaongezeka mara mbili robo ya kwanza ya 2024

    Mikakati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kupitia Diplomasia ya Uchumi inazidi kuzaa matunda ambapo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili ongezeko la miradi ya uwekezaji kwa asilimia 111, kutoka miradi 100 Januari hadi Machi 2023 hadi miradi 211 kipindi kama hicho mwaka 2024. Thamani ya uwekezaji huo imeongezeka kwa USD milioni 217.98 (TZS bilioni 566.75) kutoka USD bilioni 1.26 (TZS trilioni 3.26) katika robo ya kwanza ya mwaka 2023 hadi kufikia USD bilioni 1.48 (TZS trilioni 3.85) katika robo ya kwanza ya mwaka 2024. Uwekezaji huu utawanufaisha maelfu ya wananchi ambapo idadi ya ajira imeongezeka kufikia 24,931 katika kipindi tajwa kwa mwaka 2024 kutoka ajira 17,016 zilizosajiliwa mwaka jana, sawa na ongezeko la asilimia 46.5. Mafanikio haya ni matokeo ya hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwemo kuboresha Sheria ya Uwekezaji ambayo inatoa msamaha wa ushuru wa forodha wa asilimia 75, imepunguza kiwango cha mtaji wa uwekezaji kwa wazawa toka USD 100,000 hadi USD 500,000. Mengine yaliyofanyika ni kuwa na kituo cha pamoja ambacho mwekezaji atapata huduma zote, kuwezesha usajili wa miradi kwa njia ya mtandao, kufuta au kupunguza ada na tozo, kurahisisha utoaji wa leseni pamoja na kufanya mikutano na wafanyabishara nje ya nchi, hasa kupitia ziara za Mheshimiwa Rais na maonesho mbalimbali, ambavyo vimeendelea kuitangaza nchi yetu na kuendelea kuimarika kwa amani na utulivu nchini.   Read More

  • Maeneo 8 ya vipaumbele ya Mheshimiwa Rais Samia uandaaji wa Dira ya 2050

    Tanzania ipo katika mchakato wa kuandaa dira mpya ya Taifa ya maendeleo ya miaka 25 (mwaka 2025 hadi mwaka 2050) ambayo itakuwa ni dira ya pili kuandaliwa nchini baada ya ile iliyoanza mwaka 2000 na inatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Akizindua mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi kwa ajili ya kuandaa dira mpya, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameainisha maeneo nane ya kipaumbele katika dira mpya ambayo yanatokana na mahitaji ya sasa ya dunia, makosa na mafanikio yaliyotokana na utekelezaji wa dira inatoelekea ukomo pamoja na mahitaji mengine ya kitaifa. Kwanza, ukuaji wa uchumi kufungamanishwa na sekta za uzalishaji zinazowagusa wananchi wengi zaidi na kutengeneza ajira kwaajili yao kama vile sekta ya kilimo. Pili, kukusanywa kwa takwimu kutoka sekta isiyo rasmi ili kupata hali halisi ya uchumi badala ya kutumia takwimu za sekta rasmi pekee, hali inayosababisha kukosa uhalisia wa hali ya uchumi. Eneo la tatu ni tathmini na ufuatiliaji ambao utawezesha kubaini viashiria vya kasoro kwenye utekelezaji wa dira mapema na kuzifanyia kazi ili kuhakikisha malengo yanafikiwa. Nne, uratibu wa kufungamanisha miradi ya kipaumbele kwa sekta zinazohusika katika uzalishaji. Katika hili Mheshimiwa Rais amesisitiza kuwa mipango ya sekta moja inapotekelezwa iwe na mwingiliano na mchango katika sekta nyingine ili kutumia rasilimali chache kwa matokeo makubwa. Tano, amesisitiza dira iweke mwelekeo wa uwekezaji na usimamizi wa maboresho ya kiutendaji wa mashirika ya serikali ili yaongeze ufanisi katika uendeshaji na yaweze kuhimili ushindani wa kikanda na kimataifa. Ushiriki wa sekta binafsi katika kukuza uchumi ni eneo la sita alilolitaja ambapo amesema lazima sekta binafsi iimarishwe na iwe tayari kuimarika ili ziwe na uwezo na utayari wa kufanya biashara, kutengeneza ajira pamoja na kushirikiana na sekta binafsi nje ya nchi. Uimarishaji huo unajumuisha uwepo wa mifumo rafiki ya kisheria, upatikanaji wa mitaji na rasilimali watu yenye ujuzi. Kuzingatiwa kwa maadili ya Taifa ni sehemu… Read More

  • Dodoma, London, Maputo: Septemba ya Rais Samia na Diplomasia ya Uchumi

    Septemba 17 mwaka huu Rais Samia aliondoka nchini kuelekea Uingereza kuhudhuria mazishi wa Malkia Elizabeth II baada ya kualikwa kama mmoja wa viongozi wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola. Watu mashuhuri dunianiani takribani 500 walipewa mualiko huo ambao ulizingatia si tu uanachama wa Jumuiya ya Madola lakini pia rekodi ya haki za binadamu kwa kiongozi mwalikwa na nchi anayotoka. Pamoja na mambo na kupata nafasi ya kukutana na viongozi wa mataifa mengine, kuhudhuria mazishi hayo kitendo hicho ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uingereza pamoja na jumuiya hiyo ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa kwa zaidi ya miaka 50 hivi sasa. Kwa mujibu wa takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania, Uingereza ni moja ya wawekezaji wakubwa zaidi Tanzania ikiwa na zaidi ya 30% ya uwekezaji wa Tanzania unaotoka nje (FDI). Mfano kati ya mwaka 1990 hadi 2013 Uingereza iliwekeza Tanzania zaidi ya shilingi Trilioni 8.5 ikizalisha ajira 271,000 kwa Watanzania. Baada ya shughuli hiyo, Rais Samia alielekea nchini Msumbiji kwa  ziara ya kiserikali ya siku tatu ambayo imekuwa na manufaa makubwa kati ya mataifa haya jirani katika kuimarisha ushirikiano wake. Tanzania na Msumbiji zina uhusiano mkubwa wa kihistoria. Nchi hizi zinashea mpaka wa pamoja wa zaidi ya kilometa 800, eneo muhimu katika usalama na uchumi hasa nyakati hizi za ugunduzi wa gesi kwenye mikoa ya kusini mwa nchi yetu.  Mwenendo huu unafanya Msumbiji kuwa mbia muhimu wa Tanzania katika uchumi, ulinzi na usalama. Ili kuimarisha ulinzi na usalama ambao ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi, Tanzania na Msumbiji zilitia saini hati mbili za makubaliano, moja ikiwa ni ushirikiano katika masuala ya ulinzi na ya pili ikiwa Uratibu wa Huduma za Utafutaji na Uokoaji ikikumbukwa kuwa Taifa hilo limekuwa likipambana na magaidi katika jimbo la Cabo Delgado ambalo kwa Tanzania limepakana na… Read More

  • Barua ya wazi ya Rais Samia Suluhu

    Tanzania inatimiza miaka 30 tangu turejee rasmi katika siasa za mfumo wa vyama vingi katika kipindi hicho, Taifa letu limepitia kipindi cha furaha, majonzi, misukusuko na changamoto zote wakati Taifa linapoanza njia mpya. Jambo hili si jepesi, kwa sababu nyakati hizo hazikuwa rahisi duniani kote. Miaka ambayo Tanzania ilirejea katika mfumo huo ilikuwa migumu. Miaka ya mwanzoni ya 1990, ndiyo ilishuhudia changamoto kama vile kuanguka kwa iliyokuwa Urusi, vita vya wenyewe kwa wenyewe Afrika, mauaji ya Kimbari na migogoro mingi ya kisiasa na kiuchumi katika nchi zinazoendelea kama yetu Lakini Watanzania walipita wakati wote huo, wakiwa wamoja na tumeendeleza utamaduni huo miaka 30 baadaye. Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza wote, na ni matumaini yangu makubwa, kwamba viongozi watakaokuja miaka 50 hadi 100 baadaye wataendelea kuongoza nchi iliyo moja na wananchi wasiobaguana na kupigana, hata kama wanapingana kuhusu namna ya kuendesha nchi yao. Ni vizuri kuzungumza kuhusu nana tulivyoingia katika mfumo huu. Rais Ali Hassan Mwinyi aliunde Tume ya Jaji Francis Nyalali iliykuja na majibu kwamba ni azilimia 20 tu ya Watanzania ndio walitaka mfumo wa vyama vingi. Ni busara ya Mzee Mwinyi na viongozi wenzake wa wakati huo walioamua kusikiliza wachache. Kama wazee wetu wangesubiri mpaka asilimia 80 itake vyama vingi ndiyo tukubali pengine leo tusingekuwa tulipo. Hili ni miongoni mwa mafunzo makubwa kwa wanasiasa wa kizazi changu na watakaokuja baadaye. Kwenye jambo la maslahi ya nchi, maarifa na busara ndiyo muhimu kuliko namba. Kutoka kuwa na chama kimoja cha siasa – Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa tuna vyama vilivyosajiliwa 20. Badala ya kusikia sauti moja. Badala ya kusikia sauti moja na wakati mwingine tukisema “Zidumu Fikra za Mwenyekiti”. Sasa Watanzania wanasikia kuhusu fikra za sauti tofauti. Kwa bahati nzuri, hata Mwenyekiti Mao alipata kusema “acha maua 100 yamee kwa pamoja”. Kipekee kabisa, nitumie nafasi hi kuwapongeza wote waliofanikisha safari… Read More