November 2024
-
Zaidi ya mashabiki 60,000 walioujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam walilipuka kwa shangwe baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo dhidi ya Guinea na kuibuka na ushindi wa goli 1-0, ushindi uliomaanisha kuwa Tanzania kwa mara ya nne imefuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 itakayofanyika nchini Morroco Tanzania inafuzu kushiriki michuano hii kwa mara ya nne ikiwa imefanya hivyo mwaka 1981, 2019, 2023 na sasa 2025. Kwa hatua hii Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia katika vitabu vya kumbukumbu na historia ya michezo nchini kwa kuwa Rais ambaye chini ya uongozi wake timu ya Taifa imefanikiwa kufuzu kushiriki mashindano haya makubwa zaidi kwa ngazi ya nchi barani Afrika mara mbili tena mfululizo. Mafanikio haya hayatokei kwa bahati mbaya na ni dhahiri kuwa ni matokeo uongozi thabiti na motisha kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Sote tunafahamu namna ambavyo amekuwa akichochea timu za Taifa na hata vilabu vinavyoshiriki michuano ya kimataifa kupata matokeo chanya kwa kuweka motisha ya goli la Mama. Katika mchezo dhidi ya Ethiopia uliofanyika nchini Congo, Rais Samia alitoa ndege maalum iliyowapeleka wachezaji katika mchezo ule na kuwawezeshea kurejea kwa wakati nchini kujiandaa na mchezo dhidi ya Guinea ambao ndio umeipatia Tanzania tiketi ya kufuzu Afcon 2025. Ushindi dhidi ya Guinea ulichagizwa kwa kiasi kikubwa na nguvu ya mashabiki zaidi ya 60,000 walioujaza uwanja wa Taifa. Nakukumbusha tu mashabiki hawa wote waliingia bure kwani Rais Samia aliwalipia wote viingilio ili tu wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono Taifa Stars. Habari njema zaidi ni kwamba baada ya Afcon 2025, michuano inayofuata mwaka 2027 Tanzania pia imo ndani kwani kwa mara ya kwanza michuano hii itafanyika katika ardhi ya Afrika Mashariki kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya na Uganda hivyo tayari tuna tiketi ya moja kwa moja. Mashindano haya kuja Afrika Mashariki… Read More
-
Kati ya mwezi Januari hadi Julai 2024 jumla ya ajira 607,475 zimezalishwa nchini ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kufikia lengo la kuzalisha ajira milioni 1.2 kila mwaka. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma. Jitihada za kuhakikisha watanzania wanapata ajira zinaakisi lengo la kuzalisha ajira milioni nane kama ilivyoelezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025. Akizungumzia maeneo ambayo Serikali inayaangazia katika kuzalisha ajira ameeleza kuwa Serikali inatumia balozi zake kutafuta nafasi za kazi kwa watanzania kwenye maeneo yalipo balozi hizo. Vilevile ametaja njia nyingine kuwa ni kupitia taasisi za elimu, wizara na vyuo vikuu ambako baadhi ya watanzania wanapata ajira nje ya nchi, zikiwamo nafasi za utafiti na fursa kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa. Pia Naibu Waziri Katambi ameeleza kuwa Serikali tayari imeanza kutekeleza mpango maalumu kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) ili kubaini ajira zinazotangazwa mtandaoni na kuwafikia watanzania katika kanzidata, pia kuwasaidia kwa mafunzo ili kuhakikisha wanastahili kupata ajira hizo. Read More
-
Ili kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Serikali imekabidhi magari 88 kwa taasisi hiyo. Magari hayo ambayo yatasambazwa mikoa yote Tanzania yamekabidhiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi hiyo, hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro. Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa huku mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea. Read More