Mama yukokazini

  • #MiakaMiwiliYaMama na Diplomasia ya Uchumi: Shilingi ya Tanzania kutumika kununua bidhaa nchini India

    Azma ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji inazaa matunda ambapo Tanzania na India zimefikia makubaliano ya kibiashara ambayo yatawezesha wafanyabiashara kutoka pande zote kutumia fedha zao (shilingi na rupia) katika kufanya miamala ya kibiashara. Nafasi hii itarahisisha biashara ambapo India ni moja ya washirika wakubwa wa kibiashara na Tanzania ambapo thamani ya biashara kati ya nchi hizi ni TZS trilioni 10.4 katika mwaka ulioishia Machi 2022. Takwimu zinaonesha kuwa katika mwaka wa kwanza wa Rais Samia, India iliingiza nchini bidhaa zenye thamani ya TZS trilioni 5.3, huku ikipokea bidhaa za TZS trilioni 5.1 kutoka Tanzania. Utaratibu huu mpya si tu utakuza biashara kati ya mataifa haya kufikia lengo la zaidi ya TZS trilioni 13.8 mwaka huu, bali pia utaziwezesha kutunza akiba ya fedha za kigeni ambao sasa hazitahitajika kufanya miamala. Watanzania wanaofanya kazi katika sekta za kilimo na madini watanufaika zaidi kutokana na sekta hizo kuingiza bidhaa zaidi nchini India. Kwa mujibu wa wachumi na wataalamu wa biashara, uamuzi huo pia utaimarisha utabirikaji wa viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni jambo ambalo ni la muhimu sana katika biashara za kimataifa kwani ina usimamizi wa fedha yake tofauti na awali ilipokuwa ikitumia dola za Marekani. Read More

  • Miaka Miwili: Mheshimiwa Rais alivyoiimarisha sekta ya sanaa na kuzalisha ajira kwa vijana

    Machi 2023 Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatimiza miaka miwili tangu achukue usukani wa kuiongoza Tanzania. Watanzania wakitazama nyuma wanaona kuwa amefanya mambo mengi makubwa, ambayo yameboresha taswira ya nchi kikanda na kimataifa pamoja na kuchochea maendeleo ya Mtanzania mmoja mmoja. Sekta ya sanaa haikuwa mbali kufikiwa na mafanikio haya, ambapo kwa sasa wasanii wana mengi ya kuelekeza kwa namna walivyoshikwa mkono. Haya ni baadhi ya mengi aliyoyafanya; Kuwa Mwigizaji namba moja wa filamu Filamu ya kutangaza utalii nchini, Tanzania: The Royal Tour ilikuwa ishara ya kwanza kwa wasanii juu ya namna Rais anavyoitazama kwa umuhimu tasnia ya filamu, na hivyo kuwapa hamasa kubwa wasanii. Tuzo za Muziki Machi 2022 tuzo za muziki zilirejeshwa nchini ikiwa ni miaka sita tangu mara ya mwisho zilipotolewa na sasa zinasimamiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia. Kurejeshwa kwa tuzo hizo kumewapa hamasa wasanii kufanya kazi bora zaidi za sanaa na kuonesha kuwa Serikali inatambua jitihada zao. Tuzo za Filamu Tangu Rais Samia aingie madarakani, tuzo za filamu zimetolewa mara mbili, utaratibu ambao awali haukuwepo, huku Watanzania wakiziona katika nchi nyingine. Mwaka 2021 tuzo zilitolewa jijini Mbeya na mwaka 2022 zilitolewa jijini Arusha, na hivyo kuongeza motisha kwa wasanii kufanya kazi bora kuanzia uandaaji, picha na maudhui. Mirabaha Ombi la miaka mingi la wasanii lilipata majibu ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia ambapo walilipwa fedha kutokana na kazi zao kutumika katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana ambapo TZS milioni 312 zilitolewa. Mikopo kwa Wasanii TZS bilioni 2.5 zilizotengwa kwa ajili ya wasanii kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa zinawawezesha wasanii kuboresha kazi zao na kutoa fursa za ajira kwa vijana zaidi. Rais Samia alifufua mfuko huo ambao uliacha kufanya kazi tangu mwaka 2013, na tayari wasanii wamepewa mikopo ya hadi TZS milioni 40. Tanzania Mwenyeji mashindano ya kimataifa Mashindano ya urembo… Read More

  • Miaka miwili ya Mheshimiwa Rais inavyonufaisha vijana na wanawake kwa mitaji

    Msemo wa Wahenga kuwa Mgaagaa na upwa hali wali mkavu umejirihirisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na manufaa lukuki yanayowafaidisha Watanzania kutokana na safari za nje ya nchi ambapo manufaa hayo awamu hii yanagusa zaidi wanawake na vijana. Ziara zake zimewezesha wafanyabiashara kutoka Ulaya kuja nchini wiki iliyopita ambapo kupitia Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) walitoa mikopo yenye masharti nafuu ya TZS trilioni 1.4 kwenye benki za CRDB, NBC na KCB ambayo itawanufaisha wajasiriamali, pamoja na TZS bilioni 318 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ujasiriamali ya Uholanzi (FMO) na Taasisi ya Ufaransa ya Kufadhili Maendeleo (PROPARCO). Nusu ya fedha za EIB, TZS bilioni 700 zitatumika kukuza biashara za wajasiriamali ambapo TZS bilioni 421 zitaelekezwa kufanikisha miradi na biashara zinazoendeshwa na kusimamiwa na wanawake na TZS bilioni 248 zitatumika kwenye miradi iliyopo kwenye uchumi wa bahari. Kupitia mikopo hiyo, benki za ndani zitakuwa na uwezo wa kutoa mikopo kwa wanawake na wajasiriamali wengi zaidi ambao changamoto ya mitaji imekuwa kubwa kwao. Tukio hili moja ni ushuhuda namna kila safari ambayo Mheshimiwa Rais anafanya nje ya nchi imeleta fursa zaidi za kibiashara na kuvutia wawekezaji nchini. Read More

  • Una miaka kati ya 15 hadi 35? Bofya hapa kuona fursa kutoka Serikalini

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anafungua fursa zaidi za mafunzo ya ufundi ikiwa ni moja ya njia za kukabiliana na changamoto ya ajira nchini hasa kwa vijana na wanawake. Hapa chini ni tangazo la fursa za mafunzo kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambayo yanatolewa bure na Serikali katika vyuo 28 nchini. Hapa chini ni fomu ya kutuma maombi; Read More

  • Miaka Miwili: Mageuzi (Reforms) ya Mheshimiwa Rais Samia yanavyoimarisha biashara nchini

    Ikiwa mageuzi (reforms) ni moja ya nguzo nne (4Rs) za uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ndani ya kipindi kifupi amefanya mageuzi makubwa kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, hatua ambayo imefufua biashara na kuvutia uwekezaji ndani na nje ya nchi. Mageuzi hayo yaliyofanyika, Rais amelenga kuimarisha taasisi na kuhakikisha sera, sheria, na kanuni zinazosimamia biashara na uwekezaji zinatabirika, lakini pia zinachochea uwazi, zinaondoa ukiritimba na changamoto nyingine ambazo zimekuwa zikikwamisha ustawi wa biashara nchini. Mafanikio makubwa yamepatikana katika mageuzi hayo ambayo ni pamoja na kufuta kodi na tozo zaidi ya 230 ambazo ziliathiri ukuaji wa biashara. Aidha, Tanzania imeimarisha ushirikiano na mataifa mengine katika masuala ya kikodi ambapo tayari imetia saini makubaliano na nchi 10 kuondoa utoaji kodi mara mbili na kuzuia ukwepaji kodi, moja ya nchi hizo ni Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Zaidi ya hapo mageuzi yamefanyika katika kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli za ukadiriaji kodi zinafanyika kwa haki, kuhakiksha ritani za kodi zinafanyika kwa wakati, kutumia mifumo ya kodi ya kidijitali ikiwa ni pamoja na dirisha la mtandaoni linalowawezesha wateja kujihudumia na dirisha la pamoja la kielektroniki linalorahisisha ufanyaji wa miamala. Pia, Serikali imefanya mabadiliko Sheria ya Rufaa za Kodi, Sura ya 408 na kujumuisha njia mbadala ya usuluhishi wa migogoro na hivyo kupunguza mlolongo mrefu katika kushughulikia rufaa za kikodi. Katika muktadha huo huo, Rais Samia amefanikisha upatikanaji wa sheria mpya ya uwekezaji (Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 2022) ambayo imeiondoa Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 1997. Sheria mpya imeweka mazingira bora zaidi ya biashara ikipunguza muda wa kupata leseni kutoka siku 14 za kazi hadi siku 7 za kazi na pia kutoa nafasi usuluhishi wa migogoro kwenye taasisi za kimataifa. Kutokana na ukweli kuwa mazingira ya biashara yatafanikiwa kukiwa na… Read More

  • Fursa za ajira mpya kwa vijana kutoka Shirika la Posta Tanzania

    Read More

  • Changamkia nafasi mpya za ajira IFM, WCF, JKCI na KCMC

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuongeza nafasi za ajira katika taasisi mbalimbali za Serikali ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi. POST: ASSISTANT LECTURER – IN ACCOUNTING – 1 POST Employer: Institute Of Finance Management (IFM) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: COMPLIANCE OFFICER – 11 POST Employer: Workers Compensation Fund (WCF) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: ASSISTANT LECTURER – IN ACCOUNTING – 1 POST Employer: Institute Of Finance Management (IFM) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: ASSISTANT LECTURER – IN ACTUARIAL STUDIES/SCIENCE – 1 POST Employer: Institute Of Finance Management (IFM) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: ASSISTANT LECTURER – IN BANKING – 3 POST Employer: Institute Of Finance Management (IFM) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: COMPLIANCE OFFICER – 11 POST Employer: Workers Compensation Fund (WCF) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: TECHNICIAN II (ELECTRICAL)(RE-ADVERTISED) – 1 POST Employer: Kilimanjaro Christian Medical Centre(KCMC) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: COMPLIANCE OFFICER – 11 POST Employer: Workers Compensation Fund (WCF) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: MEDICAL SPECIALIST II (RE-ADVERTISED) – 6 POST Employer: Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: TECHNOLOGIST II (DENTAL)(RE-ADVERTISED) – 1 POST Employer: Kilimanjaro Christian Medical Centre(KCMC) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: TECHNOLOGIST II (PHARMACY)(RE-ADVERTISED) – 1 POST Employer: Kilimanjaro Christian Medical Centre(KCMC) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: ASSISTANT NURSING OFFICER I(RE-ADVERTISED) – 3 POST Employer: Kilimanjaro Christian Medical Centre(KCMC) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: MEDICAL SPECIALIST II (RE-ADVERTISED) – 4 POST Employer: The Benjamin Mkapa Hospital More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: COMPLIANCE OFFICER – 11 POST Employer: Workers Compensation Fund (WCF) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: ASSISTANT LECTURER – IN PROGRAMMING – 1 POST Employer: Institute Of Finance Management (IFM) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: ICT OFFICER (COMPUTER SYSTEMS PROGRAMMER) – 4 POST Employer: Workers Compensation Fund (WCF) More Details 2023-02-19  Login to Apply POST: COMPLIANCE OFFICER – 11 POST… Read More

  • Nishati ya Uhakika ni Uhuru: Mheshimiwa Rais anavyovipa vijiji vya Tanzania Uhuru

    Maendeleo ya Watanzania na maendeleo ya nchi yanategemea sana upatikanaji wa nishati ya uhakika, na kwa kulitambua hilo, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katika miaka yake miwili ya uongozi ameendelea kuimarisha sekta hiyo ambayo imefungua zaidi fursa za kiuchumi kwa wananchi, ushuhuda wa karibuni ukiwa ni wananchi wa Kigoma walioanza kunufaika na umeme wa gridi ya Taifa ambao ni wa uhakika zaidi kuliko uliokuwa ukizalishwa kwa majenereta. Katika muktadha huo huo wa kuwawezesha wananchi, Serikali imesaini mikataba ya utekelezaji wa miradi mikubwa mitatu ya kupelekea umeme zaidi vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA), miradi ambayo itagusa sekta za kilimo, afya, maji, viwanda vidogo na madini. Mradi wa kwanza (Ujazilizi 2B) ambao utafikisha umeme katika vitongoji 1,522 ambao utaunganisha umeme kwa wananchi zaidi ya 88,000. Mradi wa pili unapeleka umeme kwenye migodi na maeneo yenye shughuli za kilimo 336 yaliyopo katika mikoa 25 ya Tanzania Bara. Mradi huu utawapunguzia gharama (fedha na muda) za uchimbaji madini wachimbaji wadogo, utazalisha ajira zaidi, utawawezesha kutumia teknolojia ya kisasa, utachochea ukuaji wa sekta ya madini pamoja na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa. Aidha, kwa kufikisha umeme katika maeneo yenye shughuli za kilimo kunaendana na lengo la Serikali la kuifanya Tanzania kuwa kapu la chakula kwa Afrika, kwa kuvutia vijana kufanya kilimo cha kibiashara. Umeme utasaidia katika umwagiliaji na uongezaji thamani wa mazao. Mradi wa tatu unahusisha kupeleka umeme katika vituo vya afya 63 na pampu za maji 333 vijijini katika mikoa 25. Kufika kwa nishati kwenye maeneo hayo kutaboresha utoaji huduma za afya, mathalani nyakati za usiku, kutapunguza vifo vya mama na mtoto, na kuwezesha upatikanaji huduma nyinginezo zinazohitaji umeme. Wakati huo huo, uwepo wa umeme unaosukuma maji katika pampu utahakikisha vijiji vinakuwa na maji ya uhakika, hatua ambayo itakuza usafi na kupambana na magonjwa ya mlipuko, lakini pia itapunguza muda wa… Read More

  • Mheshimiwa Rais amedhamiria kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini. Bonyeza hapa kutuma maoni kwa Tume aliyoiunda

    Kwa muda sasa kumekuwa na malalamiko kuhusu wananchi kutoridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya taasisi zinazosimamia haki jinai nchini kuanzia kwenye ukamataji wa mtuhumiwa, upelelezi, utoaji wa dhamana, uendeshaji wa mashtaka, kesi na eneo ambalo aliyehukumiwa anatumikia kifungu chake. Kutokana na hali hiyo Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai, iliyoundwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inakualika mwananchi na mdau wa haki kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kuboresha taasisi hizo. Kwa maelezo zaidi soma tangazo hili; Read More

  • Mheshimiwa Rais Samia apongezwa kila kona kwa kuongeza ‘boom’ vyuo vikuu

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wanafunzi wa elimu ya juu nchini kwa kuongeza fedha za kujikimu kutoka TZS 8,500 HADI TZS 10,000, kauli ambayo iliibua shangwe huku wanafunzi wakiimbia “tuna imani na Samia,” pamoja na kupiga makofi ya furaha. Wakati wanafunzi hao wakishangilia kwa aamuzi huo uliokonga nyoyo zao, Rais Samia amesema ombi lao la wanafunzi wa ngazi ya stashahada na astashahada kupatiwa mikopo litawekewa mipango kwanza. “Kwa kazi tunazozifanya sasa hivi na hali ya bajeti, hili bado hatujafikia huko, kwa hiyo tunalifikiria, tunaliweka kwenye mipango yetu,” amesema Rais Samia huku akieleza amemuagiza waziri wa fedha aangalie uwezekano wa kupata fedha, akifanikiwa atamuongezea nyingine ili wananchi hao wanufaike. Wakati hayo yakiendelea, Rais Samia ameeleza mikakati ambayo Serikali yake inachukua kuwawezesha wahitimu kujiajiri pindi wanapohitimu masomo yao ikiwa ni pamoja na mapitio ya mitaala na kuhimiza elimu na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. “Tunataka elimu isiwe chanzo cha changamoto ya ajira, bali itoe suluhisho […] Ndio maana tumejielekeza sana sasa kwenye elimu ya TEHAMA ili vijana muweze kujiajiri wenyewe,” amesema Rais Samia. Wanafunzi wa elimu ya juu wakiwakilishwa na viongozi wao wamemshukuru Rais Samia kwa hatua ambazo ameendelea kuchukua kuboresha elimu ya juu nchini ambapo wameanza kuona matokeo. Read More