March 2023
-
‘Champion’ wa mageuzi ya demokrasia, ndiyo sifa Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris aliyompa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na mageuzi ya kisiasa aliyofanya nchini ikiwa ni pamoja na kuruhusu mikutano ya hadhara, kukutana na viongozi wa vyama vya siasa na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari. Kutokana na uongozi bora wa Rais Samia, Marekani na Tanzania zimekubaliana kupanua ushirikiano ambao utawezesha upatikanaji wa dola za Kimarekani milioni 500 (TZS trilioni 1.2) kugharamia uletaji wa bidhaa na huduma nchini Tanzania katika sekta za usafirishaji, nishati salama, teknolojia ya kidijitali na miundombinu. Aidha, katika muktadha huo wa kukuza uchumi amesema kazi ya ujenzi wa kiwanda cha kwanza na cha aina yake Afrika kitakachotumika kuchakata madini yanayotengeneza betri za magari ya umeme ambayo yatakuwa yanatumika duniani kote ikiwepo Marekani inandelea na uzalishaji utaanza mwaka 2026. Kuongezeka kwa fursa hizi kutazalisha ajira kwa maelfu ya Watanzania, na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika ramani ya kiuchumi Afrika na duniani. Wakati huo huo, Kamala amempongeza Rais Samia kwa namna miaka miwili ya uongozi wake imewezesha kumwinua mwanamke kiuchumi, akisisitiza kuwa mwanamke akiinuliwa kiuchumi, basi familia na jamii nzima inanufaika. Read More
-
Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris akianza ziara yake ya siku tatu (Machi 29-31) nchini leo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na uchumi wameeleza kuwa ujio wake ni matokeo ya kazi kubwa ya kuimarisha diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa iliyofanywa katika miaka miwili ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Kwa Tanzania, ziara hiyo inalenga pamoja na mambo mengine, kuimarisha ushirikiano hususani kwenye maeneo ya kimkakati ambayo yanagusa maisha ya Watanzania ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, utalii, elimu, afya na utunzaji wa mazingira. Ziara hiyo imekuja takribani mwaka mmoja tangu Rais Samia alipofanya ziara nchini Marekani, ambapo alimwalika Kamala kuzuru Tanzania, hivyo kuitikia wito huo kunadhihirisha uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Marekani ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 62. Marekani ni moja ya washirika wakubwa wa maendeleo nchini ambapo imewekeza kwenye miradi 266 yenye thamani ya takribani trilioni 11 ambayo imetengeneza ajira zipatazo 54,584 kwa Watanzania. Itakumbukwa pia katika ziara ya Rais Samia nchini Marekani Aprili 2022 alifanikiwa kuvutia uwekezaji wa zaidi ya TZS trilioni 2, hivyo ujio wa kiongozi huyo wa juu wa Marekani unatazamiwa kuwa na matokeo zaidi ya hayo katika sekta ya biashara na uwekezaji. Ni dhahiri kuwa Tanzania kuchaguliwa miongoni mwa nchi zaidi ya 50 za Afrika ni fursa muhimu ambayo inathibitisha kuimarika kwa mazingira ya kisiasa na kiuchumi, na hivyo ziara hiyo itaitangaza zaidi Tanzania kimataifa na kuvutia uwekezaji kutoka Marekani na sehemu nyingine. Read More
-
Mkakati wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuboresha mazingira ya biashara nchini na kuvutia uwakezaji umezaa matunda ambapo takwimu kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa thamani ya uwekezaji nchini umekua kwa asilimia 173. Ripoti ya TIC inaonesha kuwa thamani ya uwekezaji imepanda kufikia TZS trilioni 19.87 katika miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita, kutoka TZS trilioni 7.27 iliyorekodiwa katika miaka miwili kabla hajaingia madarakani. Ongezeko hilo ni matokeo ya kazi kubwa ya Rais ya kurejesha imani ya wawekezaji ndani na nje ya nchi ambao amekuwa akikutana katika ziara zake nje ya nchi na ndani ya nchi ambapo pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji, pia alizipatia ufumbuzi changamoto zilizowakabili. Kati ya Machi 2021 na Februari 2023 idadi ya miradi iliyosajiliwa imeongezeka kutoka 455 hadi 575, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 26. Kati ya miradi hiyo, asilimia 32 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42 ni ya wageni na asilimi 27 ni ubia kati ya wageni na wazawa. Kutokana na uwekezaji huo, idadi ya ajira zilizozalishwa kwa Watanzania zimeongezeka kutoka 61,900 hadi 87,187, uwekezaji mkubwa ukiwa kwenye sekta za viwanda, ujenzi wa majengo ya kibiashara na usafirishaji. Mafanikio haya yamehusishwa pia na Tanzania kushiriki katika mikutano ya kimataifa. Read More
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anadhihirisha kwa vitendo kauli yake aliyotoa kuwa hataki kuingia katika historia ya kuwa mmoja wa wanaowalaumu vijana kuwa hawajiajiri, badala yake anawawekea mazingira wezeshi ya kujiajiri kupitia kilimo ambapo lengo ni kuzalisha ajira milioni 3, kipaumbele kikiwa vijana na wanawake. Machi 20 mwaka huu amezindua mashamba ya pamoja (Block Farms) zaidi ya ekari 12,000 ambazo zitagawawiwa kwa vijana, kila mmoja kwa ukubwa usiozidi ekari 10, pia alizindua ndege zisizo na rubani, mashine za umwagiliaji na magari kwa ajili ya maafisa wa wilaya ili kuhakikisha vijana popote walipo nchini wanapata usaidizi wa kitaalamu katika kufanya kilimo cha kibiashara. Katika azma ya kukifanya kilimo kuwa cha vijana, ameahidi kuendelea kutenga bajeti mahsusi kwa ajili ya watendaji kwenye sekta ya kilimo ili shughuli zote zifanyike kwa usasa kuanzia uzalishaji hadi uuzaji mazao na bidhaa. “Tunasema ni kilimo cha vijana, hivyo vijana wawepo shambani, wawepo kwenye utaalamu, wawepo kwenye kuendesha mitambao, sehemu zote kuwa na vijana wanaokwenda kwenye sekta ya kilimo,” amesema akizindua programu ya Building a Better Tomorrow. Katika miaka miwili ya uongozi wake, kilimo ni moja tu ya njia anazotumia kumwinua kijana wa Kitanzania na kukabiliana na changamoto ya ajira inayoisumbua dunia. Ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika kila wilaya, mikopo ya halmashauri, kuboresha mazingira ya biashara hasa kwa wajasiriamali ni maeneo mengine ambayo yametoa ajira kwa vijana wengi. Read More
-
Katika moja ya hotuba zake kwa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alieleza umuhimu wa kubadili mfumo wa kilimo nchini akisema kuwa kilimo cha kutegemea mvua, kisicho na mbolea, dawa na maarifa, hakitusaidii sana. Anayoyafanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Kupitia Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) ni kuyaishi maono ya Mwalimu Nyerere kwani anakuza kilimo kwa kuwapatia vijana pembejeo (dawa, mbegu bora, viuatilifu), ili kubadili kilimo na kufikia lengo la kumnufaisha mkulima, kukuza mchango wake kwenye uchumi, kuongeza uzalishaji wa chakula na malighafi za viwandani. Kama hilo halitoshi, Machi 20 mwaka huu Rais atazindua programu ya Building a Better Tomorrow – Youth Agribusiness Initiative (BBT-YIA) ambapo katika awamu ya kwanza vijana 812 watapatiwa mafunzo kwa miezi minne bure, kisha watapewa mashamba ambayo tayari yamewekewa mifumo ya umwagiliaji kwa ajili ya kilimo. Ikiwa kati ya Watanzania 10, saba wanajishughulisha na kilimo, na ikiwa vijana ndio nguvu kazi kubwa, uamuzi wa Rais kuwekeza kwa vijana kwenye kilimo utabadili dhana kuwa kilimo hakilipi, kilimo ni cha wazee na changamoto ya ajira ambayo inawakabili vijana duniani kote itapungua nchini. Rais ametoa wito wa sekta binafsi na taasisi za kimataifa kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha vijana na wanawake, hasa kuwapatia mitaji ya shughuli za kilimo, uvuvi na ufugaji ili kuwawezesha kufikia malengo binafsi na ya kitaifa. Read More
-
Azma ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji inazaa matunda ambapo Tanzania na India zimefikia makubaliano ya kibiashara ambayo yatawezesha wafanyabiashara kutoka pande zote kutumia fedha zao (shilingi na rupia) katika kufanya miamala ya kibiashara. Nafasi hii itarahisisha biashara ambapo India ni moja ya washirika wakubwa wa kibiashara na Tanzania ambapo thamani ya biashara kati ya nchi hizi ni TZS trilioni 10.4 katika mwaka ulioishia Machi 2022. Takwimu zinaonesha kuwa katika mwaka wa kwanza wa Rais Samia, India iliingiza nchini bidhaa zenye thamani ya TZS trilioni 5.3, huku ikipokea bidhaa za TZS trilioni 5.1 kutoka Tanzania. Utaratibu huu mpya si tu utakuza biashara kati ya mataifa haya kufikia lengo la zaidi ya TZS trilioni 13.8 mwaka huu, bali pia utaziwezesha kutunza akiba ya fedha za kigeni ambao sasa hazitahitajika kufanya miamala. Watanzania wanaofanya kazi katika sekta za kilimo na madini watanufaika zaidi kutokana na sekta hizo kuingiza bidhaa zaidi nchini India. Kwa mujibu wa wachumi na wataalamu wa biashara, uamuzi huo pia utaimarisha utabirikaji wa viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni jambo ambalo ni la muhimu sana katika biashara za kimataifa kwani ina usimamizi wa fedha yake tofauti na awali ilipokuwa ikitumia dola za Marekani. Read More
-
Machi 2023 Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatimiza miaka miwili tangu achukue usukani wa kuiongoza Tanzania. Watanzania wakitazama nyuma wanaona kuwa amefanya mambo mengi makubwa, ambayo yameboresha taswira ya nchi kikanda na kimataifa pamoja na kuchochea maendeleo ya Mtanzania mmoja mmoja. Sekta ya sanaa haikuwa mbali kufikiwa na mafanikio haya, ambapo kwa sasa wasanii wana mengi ya kuelekeza kwa namna walivyoshikwa mkono. Haya ni baadhi ya mengi aliyoyafanya; Kuwa Mwigizaji namba moja wa filamu Filamu ya kutangaza utalii nchini, Tanzania: The Royal Tour ilikuwa ishara ya kwanza kwa wasanii juu ya namna Rais anavyoitazama kwa umuhimu tasnia ya filamu, na hivyo kuwapa hamasa kubwa wasanii. Tuzo za Muziki Machi 2022 tuzo za muziki zilirejeshwa nchini ikiwa ni miaka sita tangu mara ya mwisho zilipotolewa na sasa zinasimamiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia. Kurejeshwa kwa tuzo hizo kumewapa hamasa wasanii kufanya kazi bora zaidi za sanaa na kuonesha kuwa Serikali inatambua jitihada zao. Tuzo za Filamu Tangu Rais Samia aingie madarakani, tuzo za filamu zimetolewa mara mbili, utaratibu ambao awali haukuwepo, huku Watanzania wakiziona katika nchi nyingine. Mwaka 2021 tuzo zilitolewa jijini Mbeya na mwaka 2022 zilitolewa jijini Arusha, na hivyo kuongeza motisha kwa wasanii kufanya kazi bora kuanzia uandaaji, picha na maudhui. Mirabaha Ombi la miaka mingi la wasanii lilipata majibu ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia ambapo walilipwa fedha kutokana na kazi zao kutumika katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana ambapo TZS milioni 312 zilitolewa. Mikopo kwa Wasanii TZS bilioni 2.5 zilizotengwa kwa ajili ya wasanii kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa zinawawezesha wasanii kuboresha kazi zao na kutoa fursa za ajira kwa vijana zaidi. Rais Samia alifufua mfuko huo ambao uliacha kufanya kazi tangu mwaka 2013, na tayari wasanii wamepewa mikopo ya hadi TZS milioni 40. Tanzania Mwenyeji mashindano ya kimataifa Mashindano ya urembo… Read More
-
Msemo wa Wahenga kuwa Mgaagaa na upwa hali wali mkavu umejirihirisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na manufaa lukuki yanayowafaidisha Watanzania kutokana na safari za nje ya nchi ambapo manufaa hayo awamu hii yanagusa zaidi wanawake na vijana. Ziara zake zimewezesha wafanyabiashara kutoka Ulaya kuja nchini wiki iliyopita ambapo kupitia Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) walitoa mikopo yenye masharti nafuu ya TZS trilioni 1.4 kwenye benki za CRDB, NBC na KCB ambayo itawanufaisha wajasiriamali, pamoja na TZS bilioni 318 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ujasiriamali ya Uholanzi (FMO) na Taasisi ya Ufaransa ya Kufadhili Maendeleo (PROPARCO). Nusu ya fedha za EIB, TZS bilioni 700 zitatumika kukuza biashara za wajasiriamali ambapo TZS bilioni 421 zitaelekezwa kufanikisha miradi na biashara zinazoendeshwa na kusimamiwa na wanawake na TZS bilioni 248 zitatumika kwenye miradi iliyopo kwenye uchumi wa bahari. Kupitia mikopo hiyo, benki za ndani zitakuwa na uwezo wa kutoa mikopo kwa wanawake na wajasiriamali wengi zaidi ambao changamoto ya mitaji imekuwa kubwa kwao. Tukio hili moja ni ushuhuda namna kila safari ambayo Mheshimiwa Rais anafanya nje ya nchi imeleta fursa zaidi za kibiashara na kuvutia wawekezaji nchini. Read More
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anafungua fursa zaidi za mafunzo ya ufundi ikiwa ni moja ya njia za kukabiliana na changamoto ya ajira nchini hasa kwa vijana na wanawake. Hapa chini ni tangazo la fursa za mafunzo kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambayo yanatolewa bure na Serikali katika vyuo 28 nchini. Hapa chini ni fomu ya kutuma maombi; Read More