Samia Suluhu Hassan

  • Ziara ya Rais Samia nchini China yafungua fursa zaidi za Kahawa ya Tanzania

    Wafanyabiashara wa kahawa kutoka Tanzania wanaolengeka kuuza kahawa katika soko la China wametakiwa kujisajili kupitia Wizara ya Kilimo nchini Tanzania, ili kukidhi vigezo vya kulifikia soko hilo. Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amenukuliwa akisema kuwa mabadiliko hayo yatarahisisha usajili wa kampuni za Tanzania zenye nia ya kuuza kahawa katika soko la China ambapo awali kampuni nyingi zilikuwa zikipata changamoto kufanya usajili katika mtandao wa Mamlaka ya Forodha ya China (GACC). Hatua hii ni mwendelezo wa fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo Tanzania inaendelea kuzipata tangu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara nchini China ambapo akiwa na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping walishuhudia utiaji saini mikataba 15 ya kimkakati inayolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Hadi sasa kampuni saba zimeshasajiliwa kuingiza kahawa nchini China ikiwa ni pamoja Kilimanjaro Cables (T) Limited, Cotacof Limited, Taylor Winch Tanzania Limited, Dorman (Tanzania) Ltd, Kamal Agro Limited, Redloong Investment Company Limited na Ibero Coffee Trading Company (T) Limited. Uhakika wa soko la kahawa unaweka uhakika ajira na kuzalisha ajira zaidi kupitia mnyororo wa uongezaji thamani kahawa, soko la uhakika kwa wakulima na kuongeza mapato ya Serikali kwa kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi. Wakati Tanzania ikilenga kuongeza uzalishaji wa kahawa kutoka tani 65,235 mwaka 2021/2022 hadi tani 72,000 mwaka 2022/2023, wakati huo huo inalenga kuongeza mauzo yake ya kahawa nchini China na mipango inaendelea kwa wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki katika Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yanayotarajiwa kufanyika Juni 2023 huko Hunan. Read More

  • Mheshimiwa Rais Samia anavyotekeleza kwa vitendo dira ya kujenga Taifa lenye haki

    Haki ni moja ya mahitaji ya msingi kwa kila mwananchi. Akitambua umuhimu huo, Julai 2022 Mheshimiwa Rais SamIA Suluhu Hassan alitangaza kuwa ameunda kamati ya watu watano ikiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chade ambayo inafanya kazi ya kupitia miundo na utendaji kazi wa taasisi za haki jamii, kuhakikisha kuwa zinawahudumia wananchi kwa uadilifu. Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema mapitio hayo ambayo yameanza na Jeshi la Polisi yatafanyika pia katika taasisi nyingine ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, TAKUKURU, Jeshi la Magereza na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya lengo likiwa ni kuleta mabadiliko ya kiutendaji yenye matokeo kwenye vyombo hivyo. Hii si mara ya kwanza kwa Rais kuweka wazi azma yake ya kusimamia haki nchini, kwani itakumbukwa kwa agizo lake kwa Polisi kuhusu wenye kesi ambazo hazina ushahidi waachiwe lilipelekea kuachiwa kwa takribani wananchi 2,000 ambao kesi zao hazikuwa na ushahidi wa maana. “Kabla ya kumpeleka mtu ndani hakikisha umefanya kazi yako vizuri. Una ushahidi wa kutosha ndio unakwenda kumsweka,” alisema Rais Samia akizungumza na maafisa wa Jeshi la Polisi na kueleza kuwa mrundikano mkubwa wa mahabusu ni gharama kwa Serikali kwani inalazimika kuwalisha na kuwapatia huduma za afya, lakini pia ni usumbufu kwa familia. Hatua nyingine kubwa katika masuala ya haki chini ya uongozi wa Rais Samia ni pale mahakama ilipotoa haki kwa wafungwa kupiga kura, baada ya kubatilisha kifungu cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambacho kilikuwa kinapingana na katiba. Aidha, ameendeleza mapambano dhidi ya rushwa akiamini kuwa rushwa inamzuia mwenye haki kupata haki yake na asiyestahili anaipata, akitolea mfano wakati wa uchaguzi ambapo wasio na fedha wanaweza kujikuta hawachaguliwi kwa kushindwa kutoa rushwa. Wakati huo huo, ameendelea kutekeleza ahadi yake ya maridhiano kwa kukutana na kuzungumza na vyama vya siasa akifahamu kuwa haki haiwezi kustawi sehemu isiyo… Read More

  • Rais Dkt. Samia atunukiwa tuzo ya kimataifa kukuza sekta ya utalii

    Utendaji kazi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umeendelea kutambulika kimataifa ambapo siku chache tangu atajwe miongoni mwa wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka wa pili mfululizo, sasa ametunukiwa tuzo ya Mwongozaji Bora wa Watalii, tuzo iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Awards ya nchini India. Taasisi hiyo imemtunuku Dkt. Samia tuzo hiyo kutokana na mchango wake katika uandaaji wa filamu ya Tanzania: The Royal Tour ambayo imekuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza sekta ya utalii, hasa baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO19 tangu mwaka 2019. Akipokea tuzo hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana amesema itaipa Serikali ari ya kuendelea kuboresha sekta ya utalii ambayo imeendelea kukua ambapo mwaka 2021 Tanzania ilipokea watalii 992,692 lakini mwaka 2022 tayari imepokea watalii zaidi ya milioni 1, huku wengine wakiendelea kuingia. Mbali na kutangaza utalii filamu hiyo imeonesha fursa za biashara na uwekezaji zilizomo nchini ambapo wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali, ikiwemo Marekani, wamefika nchini kwa ajili ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji. Read More

  • Shahada ya Udakari ya Rais Samia ni kuendelea kutambua utumishi wake bora kwa Watanzania

    Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Doctor of Letters – Honoris Causa) ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutokana na jitihada zake za kutafuta maarifa/kujifunza na kuchochea maendeleo ya kijamii. Akitoa wasifu wa Rais Samia kabla ya kutunukiwa shahada, Prof. Penina Mlama kutoka UDSM ameeleza mambo mbalimbali ambayo yamedhihirisha kuwa mtajwa amekidhi vigezo ambapo kwanza ni namna alivyogusa na kubadili maisha ya watu katika ngazi mbalimbali alizopita kutoka kuwa karani wa ofisi hadi kuwa Rais wa nchi. Katika sekta ya elimu ambayo ndiyo kigezo cha kutunukiwa shadaha hiyo, Prof. Mlama ametaja mengi yaliyofanyika kuwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa kila mtoto kupata elimu (kujenga shule, madarasa na kunua vitendea kazi), kuwekeza katika vyuo vya kati, ufundi na vyuo vikuu, kuhuisha mkakati wa kitaifa wa elimu jumuishi, kuongeza mikopo ya elimu ya juu, kufanya mapitio ya sera na mitaala ili itoe elimu-ujuzi kulingana na mazingira ya nchi na soko la ajira. Katika uchumi, Rais amefanya marekebisho ya sera, kanuni na sheria, ameboresha mazingira ya biashara ikiwemo kuweka mazingira rafiki kwa walipakodi, kuimarisha sekta za kiuchumi kama kilimo, viwanda, nishati na utalii, ameimarisha diplomasia ya kiuchumi na kuridhia mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika ambavyo kwa pamoja vimewezesha uchumi kukua, kuvutia wawekezaji na kukuza sekta binafsi nchini. Kuhusu mageuzi yaliyofanywa kwenye kilimo ikiwemo ruzuku ya mbolea, ugawaji mbegu bora, kilimo cha umwagiliaji, kuongezeka kwa bajeti ya kilimo na kufungua masoko nje ya nchi, Prof. Mlama amesema “mpango huu inalenga kugusu uchumi wa mtu binafsi, kumwinua mwanamke na kuhakikisha pesa zinabaki katika mifuko ya watu.” “Katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameudhihirishia ulimwengu kuwa ni rahisi mahiri ambaye ameweza kuutumikia umma wa Watanzania kwa viwango vya juu kabisa, na… Read More

  • BWAWA LA KIDUNDA: RAIS SAMIA ATEGUA KITENDAWILI KILICHOSHINDIKANA TANGIA UHURU

    Waswahili wana msemo wao usemao “Lisilo budi hutendwa”, kwa kadhia ya upatikanaji wa maji waliyoipata wakaazi wa mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Pwani mtawalia ndani wiki kadhaa nyuma, serikali ya Rais Samia Suluhu haikuwa na budi kuidhinisha utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la Kidunda. Leo tarehe 11.11.2022 Rais Samia Suluhu ameshuhudia utiaji wa saini wa ujenzi wa mradi wa bwawa kubwa la Kidunda, ambapo saini hiyo ilifuatia na kumkabidhi mkandarasi eneo la mradi tayari kwa kuanza utekelezaji. Wazo la kujenga bwana la Kidunda lilikuwepo tangu baada ya nchi yetu kupata Uhuru mwaka 1961. 1961 chini ya Shirika la Chakula Duniani (FAO) Tanzania ilifanya upembuzi yakinifu ya ujenzi wa bwawa hilo, 1992 ukafanyika utafiti kwa mara ya pili, utafiti wa tatu ukafanywa Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) mwaka 1994 na 2008 Wizara ya Maji na Umwagiliaji ikafanya nayo upembuzi yakinifu ya ujenzi wa mradi huo mkubwa. Katika nyakati zote hizo, licha ya maazimio mengi kuwekwa bungeni, mradi huo ulikuwa ni kitendawili kigumu kwenye utekelezaji kutokana na ufinyu wa bajeti. Baada ya miaka zaidi ya sitini leo tarehe 11.11.2022 Rais Samia Suluhu anashuhudia utiaji wa saini wa mradi mkubwa wa ujenzi wa bwana la Kidunda. Mradi huu unakwenda kuwa suluhu ya kudumu ya upungufu wa maji katika jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani na habari njema zaidi utatekelezwa kwa fedha za ndani. Bwawa la Kidunda litakuwa na uwezo wa kukusanya na kuhifadhi maji mita za ujazo milioni 150, na kisha kutiririsha maji hayo kwenye Mto Ruvu nyakati za uhaba na kupelekea uhakika wa kupatikana maji katika jiji la Dar es Salaam na Pwani ambao hutegemea maji katika Mto Ruvu kwa zaidi ya asilimia 90. Mradi huu utatumia gharama ya shilingi bilioni 329 na utatumia muda wa miaka miwili na miezi sita kukamilika. Mradi huu wa… Read More

  • Orodha ya vigezo vya udahili kwa wanufaika wa Samia Scholarship

    Wanafunzi 640 wanatarajiwa kunufaika na mpango wa ufadhili wa masomo ya chuo kikuu, Samia Scholarship, utakaoanza mwaka wa masomo 2022/23 kwa kutoa ufadhili wa asilimia 100 kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi na hisabati kwenye mtihani wa kidato cha sita. Licha ya kuwa wanafunzi 640 (wavulana 396 na wasichana 244) wamekidhi kigezo cha ufaulu cha kupata ufadhili, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeainisha vigezo vingine vitakavyozingatiwa ambavyo ni; 1. Lazima awe Mtanzania 2. Awe amefaulu ufaulu wa juu katika mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2022 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN). 3. Mwombaji awe amepata udahili kusoma fani ya teknolojia, hisabati, uhandisi na elimutiba katika chuo kikuu kinachotambuliwa na Serikali hapa nchini. 4. Aombe ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa. Mpango huu utakuwa na manufaa mbalimbali ambayo ni; 1. Kuchochea ari ya wanafunzi kupenda na kusoma masomo ya sayansi 2. Kutoa ahueni kubwa wazazi ambao pengine wangelazimika kuuza mali zao ili kumudu gharama za kusomesha watoto fani za sayansi. 3. Kukuza sekta ya sayansi na teknolojia nchini ili kunufaika zaidi na mapinduzi ya nne ya viwanda. 4. Kuongeza idadi ya wasichana/wanawake kwenye fani za sayansi ambao wamebaki nyuma kutokana na mifumo na imani potofu za jamii. Ufadhili huo ambao utazingatia vigezo vya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) utagharamia maeneo yafuatayo; Ada ya mafunzo, posho ya chakula na malazi, posho ya vitabu na viandikwa, mahitaji maalum ya vitivo, mafunzo kwa vitendo, tafiti, vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na bima ya afya. Wanafunzi watakaofadhiliwa watagharamiwa kwa miaka mitatu hadi mitano kulingana kila mmoja programu aliyodahiliwa, na atatakiwa kuwa na ufaulu usiopungua GPA ya 3.8 katika mwaka wa masomo ili kukidhi kigezo cha kuendelea na ufadhili. Read More

  • Dodoma, London, Maputo: Septemba ya Rais Samia na Diplomasia ya Uchumi

    Septemba 17 mwaka huu Rais Samia aliondoka nchini kuelekea Uingereza kuhudhuria mazishi wa Malkia Elizabeth II baada ya kualikwa kama mmoja wa viongozi wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola. Watu mashuhuri dunianiani takribani 500 walipewa mualiko huo ambao ulizingatia si tu uanachama wa Jumuiya ya Madola lakini pia rekodi ya haki za binadamu kwa kiongozi mwalikwa na nchi anayotoka. Pamoja na mambo na kupata nafasi ya kukutana na viongozi wa mataifa mengine, kuhudhuria mazishi hayo kitendo hicho ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uingereza pamoja na jumuiya hiyo ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa kwa zaidi ya miaka 50 hivi sasa. Kwa mujibu wa takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania, Uingereza ni moja ya wawekezaji wakubwa zaidi Tanzania ikiwa na zaidi ya 30% ya uwekezaji wa Tanzania unaotoka nje (FDI). Mfano kati ya mwaka 1990 hadi 2013 Uingereza iliwekeza Tanzania zaidi ya shilingi Trilioni 8.5 ikizalisha ajira 271,000 kwa Watanzania. Baada ya shughuli hiyo, Rais Samia alielekea nchini Msumbiji kwa  ziara ya kiserikali ya siku tatu ambayo imekuwa na manufaa makubwa kati ya mataifa haya jirani katika kuimarisha ushirikiano wake. Tanzania na Msumbiji zina uhusiano mkubwa wa kihistoria. Nchi hizi zinashea mpaka wa pamoja wa zaidi ya kilometa 800, eneo muhimu katika usalama na uchumi hasa nyakati hizi za ugunduzi wa gesi kwenye mikoa ya kusini mwa nchi yetu.  Mwenendo huu unafanya Msumbiji kuwa mbia muhimu wa Tanzania katika uchumi, ulinzi na usalama. Ili kuimarisha ulinzi na usalama ambao ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi, Tanzania na Msumbiji zilitia saini hati mbili za makubaliano, moja ikiwa ni ushirikiano katika masuala ya ulinzi na ya pili ikiwa Uratibu wa Huduma za Utafutaji na Uokoaji ikikumbukwa kuwa Taifa hilo limekuwa likipambana na magaidi katika jimbo la Cabo Delgado ambalo kwa Tanzania limepakana na… Read More