Shahada ya Udakari ya Rais Samia ni kuendelea kutambua utumishi wake bora kwa Watanzania

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Doctor of Letters – Honoris Causa) ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutokana na jitihada zake za kutafuta maarifa/kujifunza na kuchochea maendeleo ya kijamii.

Akitoa wasifu wa Rais Samia kabla ya kutunukiwa shahada, Prof. Penina Mlama kutoka UDSM ameeleza mambo mbalimbali ambayo yamedhihirisha kuwa mtajwa amekidhi vigezo ambapo kwanza ni namna alivyogusa na kubadili maisha ya watu katika ngazi mbalimbali alizopita kutoka kuwa karani wa ofisi hadi kuwa Rais wa nchi.

Katika sekta ya elimu ambayo ndiyo kigezo cha kutunukiwa shadaha hiyo, Prof. Mlama ametaja mengi yaliyofanyika kuwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa kila mtoto kupata elimu (kujenga shule, madarasa na kunua vitendea kazi), kuwekeza katika vyuo vya kati, ufundi na vyuo vikuu, kuhuisha mkakati wa kitaifa wa elimu jumuishi, kuongeza mikopo ya elimu ya juu, kufanya mapitio ya sera na mitaala ili itoe elimu-ujuzi kulingana na mazingira ya nchi na soko la ajira.

Katika uchumi, Rais amefanya marekebisho ya sera, kanuni na sheria, ameboresha mazingira ya biashara ikiwemo kuweka mazingira rafiki kwa walipakodi, kuimarisha sekta za kiuchumi kama kilimo, viwanda, nishati na utalii, ameimarisha diplomasia ya kiuchumi na kuridhia mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika ambavyo kwa pamoja vimewezesha uchumi kukua, kuvutia wawekezaji na kukuza sekta binafsi nchini.

Kuhusu mageuzi yaliyofanywa kwenye kilimo ikiwemo ruzuku ya mbolea, ugawaji mbegu bora, kilimo cha umwagiliaji, kuongezeka kwa bajeti ya kilimo na kufungua masoko nje ya nchi, Prof. Mlama amesema “mpango huu inalenga kugusu uchumi wa mtu binafsi, kumwinua mwanamke na kuhakikisha pesa zinabaki katika mifuko ya watu.”

“Katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameudhihirishia ulimwengu kuwa ni rahisi mahiri ambaye ameweza kuutumikia umma wa Watanzania kwa viwango vya juu kabisa, na bado kazi inaendelea,” amehitimisha Prof. Mlama.