November 2022

  • BWAWA LA KIDUNDA: RAIS SAMIA ATEGUA KITENDAWILI KILICHOSHINDIKANA TANGIA UHURU

    Waswahili wana msemo wao usemao “Lisilo budi hutendwa”, kwa kadhia ya upatikanaji wa maji waliyoipata wakaazi wa mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Pwani mtawalia ndani wiki kadhaa nyuma, serikali ya Rais Samia Suluhu haikuwa na budi kuidhinisha utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la Kidunda. Leo tarehe 11.11.2022 Rais Samia Suluhu ameshuhudia utiaji wa saini wa ujenzi wa mradi wa bwawa kubwa la Kidunda, ambapo saini hiyo ilifuatia na kumkabidhi mkandarasi eneo la mradi tayari kwa kuanza utekelezaji. Wazo la kujenga bwana la Kidunda lilikuwepo tangu baada ya nchi yetu kupata Uhuru mwaka 1961. 1961 chini ya Shirika la Chakula Duniani (FAO) Tanzania ilifanya upembuzi yakinifu ya ujenzi wa bwawa hilo, 1992 ukafanyika utafiti kwa mara ya pili, utafiti wa tatu ukafanywa Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) mwaka 1994 na 2008 Wizara ya Maji na Umwagiliaji ikafanya nayo upembuzi yakinifu ya ujenzi wa mradi huo mkubwa. Katika nyakati zote hizo, licha ya maazimio mengi kuwekwa bungeni, mradi huo ulikuwa ni kitendawili kigumu kwenye utekelezaji kutokana na ufinyu wa bajeti. Baada ya miaka zaidi ya sitini leo tarehe 11.11.2022 Rais Samia Suluhu anashuhudia utiaji wa saini wa mradi mkubwa wa ujenzi wa bwana la Kidunda. Mradi huu unakwenda kuwa suluhu ya kudumu ya upungufu wa maji katika jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani na habari njema zaidi utatekelezwa kwa fedha za ndani. Bwawa la Kidunda litakuwa na uwezo wa kukusanya na kuhifadhi maji mita za ujazo milioni 150, na kisha kutiririsha maji hayo kwenye Mto Ruvu nyakati za uhaba na kupelekea uhakika wa kupatikana maji katika jiji la Dar es Salaam na Pwani ambao hutegemea maji katika Mto Ruvu kwa zaidi ya asilimia 90. Mradi huu utatumia gharama ya shilingi bilioni 329 na utatumia muda wa miaka miwili na miezi sita kukamilika. Mradi huu wa… Read More