Rais wa Tanzania
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anadhihirisha kwa vitendo kauli yake aliyotoa kuwa hataki kuingia katika historia ya kuwa mmoja wa wanaowalaumu vijana kuwa hawajiajiri, badala yake anawawekea mazingira wezeshi ya kujiajiri kupitia kilimo ambapo lengo ni kuzalisha ajira milioni 3, kipaumbele kikiwa vijana na wanawake. Machi 20 mwaka huu amezindua mashamba ya pamoja (Block Farms) zaidi ya ekari 12,000 ambazo zitagawawiwa kwa vijana, kila mmoja kwa ukubwa usiozidi ekari 10, pia alizindua ndege zisizo na rubani, mashine za umwagiliaji na magari kwa ajili ya maafisa wa wilaya ili kuhakikisha vijana popote walipo nchini wanapata usaidizi wa kitaalamu katika kufanya kilimo cha kibiashara. Katika azma ya kukifanya kilimo kuwa cha vijana, ameahidi kuendelea kutenga bajeti mahsusi kwa ajili ya watendaji kwenye sekta ya kilimo ili shughuli zote zifanyike kwa usasa kuanzia uzalishaji hadi uuzaji mazao na bidhaa. “Tunasema ni kilimo cha vijana, hivyo vijana wawepo shambani, wawepo kwenye utaalamu, wawepo kwenye kuendesha mitambao, sehemu zote kuwa na vijana wanaokwenda kwenye sekta ya kilimo,” amesema akizindua programu ya Building a Better Tomorrow. Katika miaka miwili ya uongozi wake, kilimo ni moja tu ya njia anazotumia kumwinua kijana wa Kitanzania na kukabiliana na changamoto ya ajira inayoisumbua dunia. Ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika kila wilaya, mikopo ya halmashauri, kuboresha mazingira ya biashara hasa kwa wajasiriamali ni maeneo mengine ambayo yametoa ajira kwa vijana wengi. Read More
-
Msemo wa Wahenga kuwa Mgaagaa na upwa hali wali mkavu umejirihirisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na manufaa lukuki yanayowafaidisha Watanzania kutokana na safari za nje ya nchi ambapo manufaa hayo awamu hii yanagusa zaidi wanawake na vijana. Ziara zake zimewezesha wafanyabiashara kutoka Ulaya kuja nchini wiki iliyopita ambapo kupitia Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) walitoa mikopo yenye masharti nafuu ya TZS trilioni 1.4 kwenye benki za CRDB, NBC na KCB ambayo itawanufaisha wajasiriamali, pamoja na TZS bilioni 318 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ujasiriamali ya Uholanzi (FMO) na Taasisi ya Ufaransa ya Kufadhili Maendeleo (PROPARCO). Nusu ya fedha za EIB, TZS bilioni 700 zitatumika kukuza biashara za wajasiriamali ambapo TZS bilioni 421 zitaelekezwa kufanikisha miradi na biashara zinazoendeshwa na kusimamiwa na wanawake na TZS bilioni 248 zitatumika kwenye miradi iliyopo kwenye uchumi wa bahari. Kupitia mikopo hiyo, benki za ndani zitakuwa na uwezo wa kutoa mikopo kwa wanawake na wajasiriamali wengi zaidi ambao changamoto ya mitaji imekuwa kubwa kwao. Tukio hili moja ni ushuhuda namna kila safari ambayo Mheshimiwa Rais anafanya nje ya nchi imeleta fursa zaidi za kibiashara na kuvutia wawekezaji nchini. Read More
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wanafunzi wa elimu ya juu nchini kwa kuongeza fedha za kujikimu kutoka TZS 8,500 HADI TZS 10,000, kauli ambayo iliibua shangwe huku wanafunzi wakiimbia “tuna imani na Samia,” pamoja na kupiga makofi ya furaha. Wakati wanafunzi hao wakishangilia kwa aamuzi huo uliokonga nyoyo zao, Rais Samia amesema ombi lao la wanafunzi wa ngazi ya stashahada na astashahada kupatiwa mikopo litawekewa mipango kwanza. “Kwa kazi tunazozifanya sasa hivi na hali ya bajeti, hili bado hatujafikia huko, kwa hiyo tunalifikiria, tunaliweka kwenye mipango yetu,” amesema Rais Samia huku akieleza amemuagiza waziri wa fedha aangalie uwezekano wa kupata fedha, akifanikiwa atamuongezea nyingine ili wananchi hao wanufaike. Wakati hayo yakiendelea, Rais Samia ameeleza mikakati ambayo Serikali yake inachukua kuwawezesha wahitimu kujiajiri pindi wanapohitimu masomo yao ikiwa ni pamoja na mapitio ya mitaala na kuhimiza elimu na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. “Tunataka elimu isiwe chanzo cha changamoto ya ajira, bali itoe suluhisho […] Ndio maana tumejielekeza sana sasa kwenye elimu ya TEHAMA ili vijana muweze kujiajiri wenyewe,” amesema Rais Samia. Wanafunzi wa elimu ya juu wakiwakilishwa na viongozi wao wamemshukuru Rais Samia kwa hatua ambazo ameendelea kuchukua kuboresha elimu ya juu nchini ambapo wameanza kuona matokeo. Read More
-
Wafanyabiashara wa kahawa kutoka Tanzania wanaolengeka kuuza kahawa katika soko la China wametakiwa kujisajili kupitia Wizara ya Kilimo nchini Tanzania, ili kukidhi vigezo vya kulifikia soko hilo. Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amenukuliwa akisema kuwa mabadiliko hayo yatarahisisha usajili wa kampuni za Tanzania zenye nia ya kuuza kahawa katika soko la China ambapo awali kampuni nyingi zilikuwa zikipata changamoto kufanya usajili katika mtandao wa Mamlaka ya Forodha ya China (GACC). Hatua hii ni mwendelezo wa fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo Tanzania inaendelea kuzipata tangu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara nchini China ambapo akiwa na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping walishuhudia utiaji saini mikataba 15 ya kimkakati inayolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Hadi sasa kampuni saba zimeshasajiliwa kuingiza kahawa nchini China ikiwa ni pamoja Kilimanjaro Cables (T) Limited, Cotacof Limited, Taylor Winch Tanzania Limited, Dorman (Tanzania) Ltd, Kamal Agro Limited, Redloong Investment Company Limited na Ibero Coffee Trading Company (T) Limited. Uhakika wa soko la kahawa unaweka uhakika ajira na kuzalisha ajira zaidi kupitia mnyororo wa uongezaji thamani kahawa, soko la uhakika kwa wakulima na kuongeza mapato ya Serikali kwa kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi. Wakati Tanzania ikilenga kuongeza uzalishaji wa kahawa kutoka tani 65,235 mwaka 2021/2022 hadi tani 72,000 mwaka 2022/2023, wakati huo huo inalenga kuongeza mauzo yake ya kahawa nchini China na mipango inaendelea kwa wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki katika Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yanayotarajiwa kufanyika Juni 2023 huko Hunan. Read More
-
Ruzuku ya Serikali kwenye mafuta iliyoanza kutolewa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa ahueni kubwa kwa wananchi kutokana na bei ya mafuta kuendelea kupungua katika soko la ndani. Takwimu zinaonesha kuwa bei ya petroli kwa kipindi hicho imepungua kwa wastani wa asilimia 14 kwa petroli iliyoingizwa nchini kupitia bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara. Kuanzia Agosti hadi Januari 2023 bei ya petroli iliyopokelewa Bandari ya Dar es Salaam baada ya ruzuku imepungua kutoka TZS 3,410 hadi TZS 2,819. Wakati huo huo, bei ya petroli kupitia bandari ya Tanga imeshuka kutoka TZS 3,435 hadi TZS 2,989, huku petroli iliyopita Bandari ya Mtwara ikishuka kutoka TZS 3,393 hadi TZS 2,993. Kuendelea kushuka kwa bei ya mafuta nchini ni matokeo ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ili kumpa kila mwananchi nafuu ya maisha. Ruzuku ya TZS 100 bilioni ilianza kutumika kuanzia Juni 1, 2022 ambapo wadau na wananchi wamekiri kwamba imekuwa ahueni kubwa kwao, hasa ikilinganishwa na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania ndio ina bei ndogo zaidi ya petroli. Read More
-
Haki ni moja ya mahitaji ya msingi kwa kila mwananchi. Akitambua umuhimu huo, Julai 2022 Mheshimiwa Rais SamIA Suluhu Hassan alitangaza kuwa ameunda kamati ya watu watano ikiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chade ambayo inafanya kazi ya kupitia miundo na utendaji kazi wa taasisi za haki jamii, kuhakikisha kuwa zinawahudumia wananchi kwa uadilifu. Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema mapitio hayo ambayo yameanza na Jeshi la Polisi yatafanyika pia katika taasisi nyingine ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, TAKUKURU, Jeshi la Magereza na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya lengo likiwa ni kuleta mabadiliko ya kiutendaji yenye matokeo kwenye vyombo hivyo. Hii si mara ya kwanza kwa Rais kuweka wazi azma yake ya kusimamia haki nchini, kwani itakumbukwa kwa agizo lake kwa Polisi kuhusu wenye kesi ambazo hazina ushahidi waachiwe lilipelekea kuachiwa kwa takribani wananchi 2,000 ambao kesi zao hazikuwa na ushahidi wa maana. “Kabla ya kumpeleka mtu ndani hakikisha umefanya kazi yako vizuri. Una ushahidi wa kutosha ndio unakwenda kumsweka,” alisema Rais Samia akizungumza na maafisa wa Jeshi la Polisi na kueleza kuwa mrundikano mkubwa wa mahabusu ni gharama kwa Serikali kwani inalazimika kuwalisha na kuwapatia huduma za afya, lakini pia ni usumbufu kwa familia. Hatua nyingine kubwa katika masuala ya haki chini ya uongozi wa Rais Samia ni pale mahakama ilipotoa haki kwa wafungwa kupiga kura, baada ya kubatilisha kifungu cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambacho kilikuwa kinapingana na katiba. Aidha, ameendeleza mapambano dhidi ya rushwa akiamini kuwa rushwa inamzuia mwenye haki kupata haki yake na asiyestahili anaipata, akitolea mfano wakati wa uchaguzi ambapo wasio na fedha wanaweza kujikuta hawachaguliwi kwa kushindwa kutoa rushwa. Wakati huo huo, ameendelea kutekeleza ahadi yake ya maridhiano kwa kukutana na kuzungumza na vyama vya siasa akifahamu kuwa haki haiwezi kustawi sehemu isiyo… Read More
-
Safari ya miaka 50 ya kuelekea umeme wa kutosha leo imepiga hatua kubwa baada ya Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP) kuanza kujazwa maji leo zoezi ambalo limezinduliwa la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kufunga mahandaki yaliyokuwa yakichepusha maji ili kupisha ujenzi. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Samia amesema kuwa mradi huu ambao ujenzi wake ulianza mwaka 2018 ni mojawapo ya miradi mikubwa ya umeme barani Afrika ambapo bwawa hilo litaweza kuhifadhi maji lita bilioni 32, hivyo kuwezesha shughuli za umeme kuendelea pindi mvua zinapopungua. Dkt. Samia amekuwa na mchango mkubwa katika mradi huo ambao utaleta manufaa ya kiuchumi na kijamii, ambapo ndani ya miezi 22 amefanikiwa kujenga asilimia 41.68 ya mradi huo, wakati hapo awali ulijengwa asilimia 37 kwa muda wa miezi 27. Akitaja manufaa mengine ya mradi huo mbali na umeme utakaokizi mahitaji ya ndani na hata kuuzwa nje, amesema kuwa utachochea ukuaji wa sekta ya utalii, kutokana na kuwa katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, na pia kuwezesha fursa za uvuvi, ambapo bwawa hilo lenye urefu wa kilomita 100 litakapojaa litakuwa na ukubwa kuliko Ziwa Rukwa, hivyo ametaka ufanyike uvuvi wa kisasa. Kuhusu kilimo, amesema mradi huo utafungua fursa za kilimo katika Delta ya Rufiji na hivyo ameiagiza wizara ya kilimo, wizara ya ardhi na TAMISEMI kupima eneo la ekari 400,000 linalofaa kwa kilimo na kufanya mnada wa wazi kwa wawekezaji wa uhakika katika kilimo. “Nawasihi pia, tutenge maeneo maalum kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo, hasa wa maeneo haya, yatakayokuwa na miundombinu ya umwagiliaji,” ameagiza. Aidha, katika mradi huo limejengwa daraja la kudumu ambalo linaiunganisha mikoa ya kusini na mikoa ya kati na kaskazini mwa Tanzania, ambapo msafiri ataweza kutoka Mtwara kwenda Dodoma, Arusha au Kilimanjaro bila kupita Dar es Salaam. Pia, kutokana na bwawa hilo kuwa na maji… Read More
-
Tanzania inaendelea kujiimarisha katika mkakati wa kuwa kitovu cha usafiri na usafirishaji pamoja na biashara ambapo leo imesaini mkataba na mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kipande cha sita cha reli ya kisasa kutoka Tabora hadi Kigoma (506km) kwa gharama ya TZS trilioni 5. Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dkt. Samia amesema kuwa “hilo litafanikiwa tukihakikisha miradi yote tunayoitekeleza, tunaisimamia na kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.” Ujenzi wa kipande cha Tabora – Kigoma ambacho kitaungana na kipande cha Uvinza-Musongati-Kindu itaiunganisha Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DCR), upande wa mashariki ambapo kuna mizigo mingi inayohitaji kusafirishwa kwenda na kutoka Bandari ya Dar es Salaam, ikifahamika kuwa mwaka 2021 taifa hilo lilipitisha mizigo ya tani milioni 2.4 katika bandari hiyo. Aidha, ujenzi wa reli hiyo utachochea ukuaji wa biashara kwa kupunguza gharama za kusafirisha mizigo kwenda DRC ambapo sasa gharama za kusafirisha kontena moja hufika hadi TZS milioni 35, huku ikichukua hadi mwezi mmoja. Kuanza kutumika kwa reli kutapunguza muda na gharama hadi kufikia TZS milioni 9 na muda wa siku moja, huku ukiwa usafiri ulio salama zaidi. “Takwimu zinaonesha ujenzi wa reli hii utasaidia kufungua maeneo yenye machimbo ya madini yenye mzigo wa zaidi ya tani milioni 150 na mizigo mingine ya kuwezesha migodi hiyo kufanya kazi,” ameeleza Dkt. Samia. Mbali na hayo ujenzi wa reli umeendelea kutoa ajira kwa Watanzania ambapo zaidi ya wananchi 20,000 wamepata ajira za moja kwa moja, huku waajiriwa wakilipwa TZS bilioni 237.7. Pia umetoa zabuni kwa Watanzania zenye thamani ya takribani trilioni 2 na hivyo kuiwezesha Serikali kukusanya kodi TZS bilioni 949. Read More
-
“Si wakati wakati wote ni wa kupongezana na si wakati wote ni wa kupingana. Kwenye kujenga Tanzania bora natamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Natamani kujenga umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote.” Hayo ni maneno ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika barua yake aliyoitoa Tanzania ikiadhimisha miaka 30 tangu kurejea kwenye mfumo wa vyama vingi, ambapo alieleza azma yake ya kujenga jamii inayopata haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana na inayotoa fursa sawa za kiuchumi kwa wote. Katika kufanikisha nia hiyo, Rais ametimiza kiu ya muda mrefu ya vyama vya upinzani kwanza kwa kukutana na kuzungumza na wanasiasa wa upinzani akiwemo viongozi wa CHADEMA, CUF na ACT-Wazalendo, mazungumzo ambayo yameendelea kujenga imani miongoni mwa viongozi hao kuhusu nia thabiti ya Rais kujenga umoja wa kitaifa. Aidha, katika kutekeleza matakwa na viongozi wa vyama vya upinzani ambayo ni pamoja na kufufuliwa kwa mchakato wa katiba mpya na kuundwa tume huru ya uchaguzi, Rais aliunda kikosi kazi kilichojumuisha wawakilishi kutoka vyama vya upinzani, na tayari kimewasilisha mapendekezo serikali juu ya namna ya kuyafikia matamanio hayo. “Mama Samia amekuwa Rais wa kwanza kwenye nchi yetu baada ya ujio wa pili wa vyama vingi mwaka [19]92 kusimama hadharani, na nilisimama naye Ikulu, tukazungumza na vyombo vya habari mimi na yeye, kwamba tufanye nini kila mmoja […] tuondoe maumivu yaliyopo katika Taifa hili,” alisema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Machi 2022. Uamuzi wa Mbowe kusimama kwenye maridhiano umeungwa mkono na viongozi wa CHADEMA ambapo aliyewahi kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesema kwa sababu njia za maandamano walizowahi kujaribu huko nyuma hazikufanikiwa, basi, sasa njia ya kuelekea ni maridhiano. Kwa upande wake kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alisema “hakuna njia yoyote ya kuifanya nchi yetu iweze kwenda mbele isipokuwa njia hii ambayo [Rais Dkt. Samia… Read More
-
Utendaji kazi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umeendelea kutambulika kimataifa ambapo siku chache tangu atajwe miongoni mwa wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka wa pili mfululizo, sasa ametunukiwa tuzo ya Mwongozaji Bora wa Watalii, tuzo iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Awards ya nchini India. Taasisi hiyo imemtunuku Dkt. Samia tuzo hiyo kutokana na mchango wake katika uandaaji wa filamu ya Tanzania: The Royal Tour ambayo imekuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza sekta ya utalii, hasa baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO19 tangu mwaka 2019. Akipokea tuzo hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana amesema itaipa Serikali ari ya kuendelea kuboresha sekta ya utalii ambayo imeendelea kukua ambapo mwaka 2021 Tanzania ilipokea watalii 992,692 lakini mwaka 2022 tayari imepokea watalii zaidi ya milioni 1, huku wengine wakiendelea kuingia. Mbali na kutangaza utalii filamu hiyo imeonesha fursa za biashara na uwekezaji zilizomo nchini ambapo wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali, ikiwemo Marekani, wamefika nchini kwa ajili ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji. Read More