Biashara Tanzania
-
Mei mwaka huu Tanzania ilivunja rekodi iliyodumu kwa miaka 10 kwa kusajili miradi mpya ya uwekezaji 52 yenye thamani ya TZS bilioni 783, ikitarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 6,200 ikiwa ni matokeo ya sera za kibiashara za Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Tangu alipoingia madarakani Machi 2021, Rais Samia ameifungua nchi na kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini hatua ambayo imerejesha imani ya wawekezaji ambao wameiona Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza mabilioni yao ya mitaji pamoja na kuvutia uwekezaji mpya. Kutokana na mkakati huo mwamko wa wakezaji wa ndani nao umekuwa mkubwa kuchangamkia fursa zinazojitokeza ambapo kwa mujibu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) asilimia 50 iliyosajiliwa kati ya Aprili hadi Juni mwaka huu inamilikiwa na wazawa, mingine ikiwa ni ya wageni na ubia, ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 20 iliyokuwepo Januari. Ongezeko la uwekezaji nchini limeendelea kuwa na manufaa kwa Watanzania ambapo zaidi ya ajira za moja kwa moja 30,000 zinatokana na miradi yote iliyosajiliwa kati ya Januari hadi Juni mwaka huu, huku kukiwa na maelfu ya fursa za ajira zisizo za moja kwa moja. Manufaa mengine ni kuchochea ukuaji wa uchumi, pia kuongezeka kwa uwekezaji kunajenga imani kwa wawekezaji wapya kuja nchini. Katika kurahisisha biashara na uwekezaji, Serikali imeanzisha kituo cha pamoja ambacho kina jumla ya taasisi 12 zinazohusika na sekta hiyo ambacho kinarahisisha utoaji wa leseni, vibali na nyaraka nyingine muhimu ndani ya muda mfupi. Aidha, Mei mwaka huu TIC imeanza kutumia mfumo wa Dirisha la Pamoja la Kuhudumia Wawekezaji la Kielektroniki Tanzania (TeIW) ambalo limekuwa suluhisho katika kurahisha upokeaji wa maombi, utoaji wa huduma za vibali, leseni na usajili kwa wawekezaji kwa haraka. Lengo la Mfumo huo ni kutumika kurahisisha mtiririko wa taarifa kati ya taasisi zote zilizoko ndani ya kituo. Read More
-
Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi Januari 2023 Serikali imesajili miradi ya uwekezaji 537 yenye thamani ya TZS trilioni 17, ikiwa ni matokeo mazuri katika mkakati wa Mheshimiwa Rais wa kukuza biashara na uwekezaji nchini. Ongezeko la usajili wa miradi hiyo linatarajiwa kutoa ajira takribani 92,770 ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kuandikishwa katika kipindi chochote tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961. Hatua alizochukua Rais Samia kuboresha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kuimarisha Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja na maboresho ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania zimevutia wawekezaji wapya, zimetatua changamoto zilizokuwa zikiwakabilia wafanyabiashara na kuvutia wawekezaji na kurahisisha utoaji huduma. Aidha, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) imesajili miradi 38 yenye thamani ya TZS bilioni 327.7 na mauzo nje yenye thamani ya TZS bilioni 448.2. Miradi hiyo ni mahsusi katika sekta zinazozalisha bidhaa zitokanazo na kilimo, bidhaa za viwandani, bidhaa za mifugo, bidhaa za kemikali, bidhaa za madini na bidhaa za misitu. Kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji nchini kunakuza mzunguko wa fedha nchini, kunajenga imani ya wawekezaji waliopo pamoja na kuvutia uwekezaji zaidi. Read More
-
Ikiwa mageuzi (reforms) ni moja ya nguzo nne (4Rs) za uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ndani ya kipindi kifupi amefanya mageuzi makubwa kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, hatua ambayo imefufua biashara na kuvutia uwekezaji ndani na nje ya nchi. Mageuzi hayo yaliyofanyika, Rais amelenga kuimarisha taasisi na kuhakikisha sera, sheria, na kanuni zinazosimamia biashara na uwekezaji zinatabirika, lakini pia zinachochea uwazi, zinaondoa ukiritimba na changamoto nyingine ambazo zimekuwa zikikwamisha ustawi wa biashara nchini. Mafanikio makubwa yamepatikana katika mageuzi hayo ambayo ni pamoja na kufuta kodi na tozo zaidi ya 230 ambazo ziliathiri ukuaji wa biashara. Aidha, Tanzania imeimarisha ushirikiano na mataifa mengine katika masuala ya kikodi ambapo tayari imetia saini makubaliano na nchi 10 kuondoa utoaji kodi mara mbili na kuzuia ukwepaji kodi, moja ya nchi hizo ni Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Zaidi ya hapo mageuzi yamefanyika katika kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli za ukadiriaji kodi zinafanyika kwa haki, kuhakiksha ritani za kodi zinafanyika kwa wakati, kutumia mifumo ya kodi ya kidijitali ikiwa ni pamoja na dirisha la mtandaoni linalowawezesha wateja kujihudumia na dirisha la pamoja la kielektroniki linalorahisisha ufanyaji wa miamala. Pia, Serikali imefanya mabadiliko Sheria ya Rufaa za Kodi, Sura ya 408 na kujumuisha njia mbadala ya usuluhishi wa migogoro na hivyo kupunguza mlolongo mrefu katika kushughulikia rufaa za kikodi. Katika muktadha huo huo, Rais Samia amefanikisha upatikanaji wa sheria mpya ya uwekezaji (Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 2022) ambayo imeiondoa Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 1997. Sheria mpya imeweka mazingira bora zaidi ya biashara ikipunguza muda wa kupata leseni kutoka siku 14 za kazi hadi siku 7 za kazi na pia kutoa nafasi usuluhishi wa migogoro kwenye taasisi za kimataifa. Kutokana na ukweli kuwa mazingira ya biashara yatafanikiwa kukiwa na… Read More