Benki Kuu ya Tanzania
-
Utekelezaji imara wa sera za kiuchumi, kuimarika kwa amani na utulivu na mikakati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuifungua nchi kumeendelea kuimarisha uchumi wa Tanzania licha ya changamoto zilizotokana na mtikisiko katika uchumi wa dunia, uimara unaotarajiwa kuendelea katika siku zijazo, hususan robo ya pili ya mwaka 2024. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeainisha maeneo matano ambayo yameendelea kudhihirisha kuimarika kwa uchumi wa Tanzania katika robo ya kwanza ya mwaka 2024 ambapo kwanza ni ukuaji wa uchumi unakadiriwa kufikia asilimia 5.1 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji unaofanywa na Serikali kuongeza uwekezaji kwa sekta binafsi. Ripoti ya BoT imeeleza kuwa hatua zinazochukuliwa na Mheshimiwa Rais Samia zinachangia kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi na uwekezaji kutoka nje ya nchi. Mikopo hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea kuongezeka ilielekezwa zaidi katika shughuli za kilimo, uchimbaji wa madini, usafirishaji na uzalishaji viwandani sawasawa na malengo ya Serikali. Eneo jingine ni mfumuko wa bei ambao umeendelea kuwa tulivu, kwa wastani wa asilimia 3, hali inayotokana na utekelezaji wa sera madhubuti ya fedha na uwepo wa chakula cha kutosha nchini, hivyo kuifanya Tanzania moja ya nchi chache zenye kiwango kidogo cha mfumuko wa bei Afrika. Kiwango hicho kipo ndani ya lengo la nchi la mfumuko wa bei usiozidi asilimia 5 na vigezo vya kikanda kwa jumuiya ambazo Tanzania ni mwanachama. Matokeo ya uwekezaji na uzalishaji yameendelea kuzaa matunda ambapo nakisi ya urari wa biashara nje ya nchi iliendelea kupungua kutokana na kupungua kwa gharama za uagizaji wa bidhaa na kuongezeka kwa mauzo nje ya nchi. Nakisi imepungua kwa zaidi ya asilimia 50, kufikia dola milioni 2,701.4 mwaka unaoishi Februari 2024, kutoka dola milioni 5,133.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2023. Kuongezeka kwa mauzo nje kumechangia kuongeza akiba ya fedha za kigeni ambapo imeendelea kuwa ya kutosha, kufikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 5.3 mwishoni mwa Machi… Read More
-
Dar es Salaam, Tanzania – Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uchumi wa nchi, ambapo sasa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imechukua hatua kubwa ya kimkakati ya kununua dhahabu ya ndani ili kuimarisha hifadhi ya fedha za kigeni na kuongeza nguvu ya shilingi ya Tanzania. Tayari BoT inanunua dhahabu kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa ndani kwa kutumia shilingi ya Tanzania ambapo tayari imenunua kilogramu 418, lengo likiwa ni kununua kilogramu 6,000 katika mwaka wa fedha 2023/24. Hatua hii muhimu ina manufaa mbalimbali kwa taifa na wananchi kwa kununua dhahabu kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni, taifa letu linajikinga dhidi ya athari zitokanazo na mabadiliko ya ghafla (kutokuwepo kwa uhakika) ya kiuchumi wa kimataifa. Dhahabu imekuwa kimbilio la thamani kwa miongo mingi wakati wa migogoro ya kiuchumi na kisiasa duniani. Kwa hivyo, kwa kuchanganya dhahabu katika akiba ya fedha za kigeni, Tanzania inaweza kusaidia kulinda thamani ya shilingi ya nchi wakati wa mazingira magumu ya kiuchumi duniani. Pia, hatua ya kununua dhahabu kutoka kwa wazalishaji wa ndani kutachangia kukuza uchumi wa ndani kwani itachochea uzalishaji wa dhahabu. Kukua kwa uzalishaji kunaenda moja kwa moja na kuongezeka kwa ajira, kwani shughuli za uchimbaji na biashara ya dhahabu zinahitaji wafanyakazi, na pia ongezeko la wachimbaji litanufaisha sekta nyingine zinazofungamana na sekta hiyo ikiwemo ya huduma (chakula, maji, nishati, mawasiliano). Uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania wa kununua dhahabu kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni na kulinda uchumi unathibitisha nia ya serikali ya kusimamia utulivu wa kiuchumi na kujenga nguvu za kifedha, hatua ambayo inaweza kuwa na athari chanya kwa maendeleo na ustawi wa nchi. Read More