April 2024

  • #ZiaraYaMamaUturuki ni heshima na fursa kwa Tanzania kidiplomasia, kiuchumi na kijamii

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameanza ziara yake rasmi nchini Uturuki kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mheshimiwa Recep Erdoğan. Ziara hiyo ya kimkakati inatarajiwa kuwa na matokeo chanya kidiplomasia, kiuchumi na kimaendeleo ambapo inafanyika kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 14 (tangu mwaka 2010), na miaka saba tangu ziara ya Rais Erdoğan nchini. Tanzania na Uturuki zina uhusiano wa miaka 61 (tangu mwaka 1963), ambapo Uturuki ilifungua ubalozi wake nchini mwaka 1969, ikaufunga mwaka 1984 na kuufungua tena mwaka 2009, na hivyo kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na uhusiano baina ya mataifa haya. Malengo makuu matatu ya ziara hiyo ya kimkakati ni kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo, kufungua fursa mpya za ushirikiano wa kiuchumi, na kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo. Maeneo hayo yanatarajia yatapewa uzito katika mazungumzo atakayofanya na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais Erdoğan. Nchi hizi zina ushirikiano mkubwa kwenye biashara na uwekezaji ambapo Uturuki ni miongoni mwa nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani imewekeza nchini zaidi ya TZS trilioni 1.3 na kuzalisha ajira zaidi ya 6,700. Kwa upande wa Tanzania, huuza wastani wa bidhaa zenye thamani ya TZS bilioni 41 kila mwaka nchini Uturuki. Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) unaotekelezwa na kampuni ya Uturuki, Yapi Merkez ni kielelezo kikubwa cha ushirikiano baina ya nchi, na ziara hii inatarajiwa kuwa chachu ya kuongeza kasi ya kutekeleza mradi huo utakaobadili maisha na uchumi wa Tanzania. Aidha, Uturuki ni mshirika mkubwa katika kukuza utalii nchini ambapo safari za ndege za moja kwa moja kwenda Dar es Salaam na Kilimanjaro zimerahisisha usafiri wa watalii, sekta ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wetu. Katika kufanikisha lengo la kufungua fursa mpya za ushirikiano, akiwa nchini Uturuki, Mheshimiwa Rais Samia atashiriki jukwaa la uwekezaji pamoja na kuzungumza na kampuni 15 kubwa zaidi nchini humo na kuwashawishi kuja kuwekeza nchini. Mheshimiwa Rais… Read More

  • Mafanikio makubwa ya kiuchumi robo ya kwanza mwaka 2024 yamedhihirisha maono ya MAMA

    Utekelezaji imara wa sera za kiuchumi, kuimarika kwa amani na utulivu na mikakati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuifungua nchi kumeendelea kuimarisha uchumi wa Tanzania licha ya changamoto zilizotokana na mtikisiko katika uchumi wa dunia, uimara unaotarajiwa kuendelea katika siku zijazo, hususan robo ya pili ya mwaka 2024. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeainisha maeneo matano ambayo yameendelea kudhihirisha kuimarika kwa uchumi wa Tanzania katika robo ya kwanza ya mwaka 2024 ambapo kwanza ni ukuaji wa uchumi unakadiriwa kufikia asilimia 5.1 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji unaofanywa na Serikali kuongeza uwekezaji kwa sekta binafsi. Ripoti ya BoT imeeleza kuwa hatua zinazochukuliwa na Mheshimiwa Rais Samia zinachangia kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi na uwekezaji kutoka nje ya nchi. Mikopo hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea kuongezeka ilielekezwa zaidi katika shughuli za kilimo, uchimbaji wa madini, usafirishaji na uzalishaji viwandani sawasawa na malengo ya Serikali. Eneo jingine ni mfumuko wa bei ambao umeendelea kuwa tulivu, kwa wastani wa asilimia 3, hali inayotokana na utekelezaji wa sera madhubuti ya fedha na uwepo wa chakula cha kutosha nchini, hivyo kuifanya Tanzania moja ya nchi chache zenye kiwango kidogo cha mfumuko wa bei Afrika. Kiwango hicho kipo ndani ya lengo la nchi la mfumuko wa bei usiozidi asilimia 5 na vigezo vya kikanda kwa jumuiya ambazo Tanzania ni mwanachama. Matokeo ya uwekezaji na uzalishaji yameendelea kuzaa matunda ambapo nakisi ya urari wa biashara nje ya nchi iliendelea kupungua kutokana na kupungua kwa gharama za uagizaji wa bidhaa na kuongezeka kwa mauzo nje ya nchi. Nakisi imepungua kwa zaidi ya asilimia 50, kufikia dola milioni 2,701.4 mwaka unaoishi Februari 2024, kutoka dola milioni 5,133.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2023. Kuongezeka kwa mauzo nje kumechangia kuongeza akiba ya fedha za kigeni ambapo imeendelea kuwa ya kutosha, kufikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 5.3 mwishoni mwa Machi… Read More

  • #MiakaMitatuYaMama: Mageuzi sekta ya afya ameweka rekodi na kuimarisha huduma za afya

    Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa yaliyoboresha sekta ya afya nchini na kufanya huduma za afya kuwa karibu, bora na nafuu zaidi. Vituo vya kutolewa huduma za afya (zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, mikoa, rufaa na za kanda) 1,061 vimejengwa ambapo ni wastani wa vituo 353 kila mwaka. Ujenzi wa vituo hivi umeenda sambamba na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa ambavyo vimetoa ahueni kubwa kwa wananchi. MAMA amenunua mashine mpya za CT Scan 27, na kufanya mashine hizo nchini kufikia 45, kutoka 13 za awali. Hivi sasa mashine hizo za kiuchunguzi zinapatikana kwenye hospitali zote za rufaa za mikoa. Manufaa makubwa yanaonekana ambapo awali wakazi wa Katavi walilazimika kusafiri zaidi ya kilomita 600 kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Mbeya, lakini sasa huduma hiyo inapatikana mkoani mwao. Tangu tupate uhuru, kwa miaka 61, Tanzania ilinunua mashine za MRI saba, lakini ndani ya miaka mitatu MAMA amenunua mashine sita na kuifanya nchi kuwa na MRI 13 ambazo zimefungwa kwenye hospitali za rufaa za kanda. Mashine za X-Ray ambazo awali hazikupatikana kwa wingi kwenye vituo vya afya, sasa zimejaa tele baada ya kununuliwa kwa Digital X-Ray 199, na kuifanya nchi kuwa namashine 346. MAMA pia amenunua mashine za ultrasound 192 na kuifanya nchi kuwa na mashine 668 ambazo ni muhimu hasa katika kufuatilia ukuaji wa mimba. Vifaa tiba vingine vilivyoongezwa ni Echocardiogram kutoka 95 mwaka 2021 hadi 102 mwaka 2024, Cathlab kutoka moja mwaka 2021 hadi nne mwaka 2024 pamoja na PET Scan ambayo ndiyo ya kwanza nchini mwetu. Vitanda vipya 40,078 vya kulaza wagonjwa, vitanda vipya 1,104 vya vya ICU pamoja na kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa kufikia asilimia 84 kutoka asilimia 58 mwaka 2022. Mageuzi haya yaliyofanyika yamewezesha kupungua kwa vifo vinavyoepukika… Read More