February 2024
-
Sera nzuri za uchumi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu zimeendelea kuweka rekodi ambazo hazijawahi kufikiwa katika historia ya taifa letu ambapo shughuli kuu za kiuchumi za utalii, madini na uzalishaji viwandani zimeendelea kufanya vizuri zaidi. Mwaka 2023 mapato yatokanayo na utalii na dhahabu kwa mara ya kwanza yalivuka dola za Kimarekani bilioni 3 (zaidi ya TZS trilioni 7.6), huku uuzaji nje wa bidhaa za viwandani ukiendelea kuwa juu ya kiwango cha dola za Kimarekani bilioni 1 tangu MAMA aingie madarakani. Matokeo haya ambayo hayakuwahi kufikiwa kabla ni ushahidi kuwa sera nzuri za Rais Samia zinalipa ambapo kupaa kwa mapato ya utalii na dhahabu kumeiwezesha nchini kupunguza urari wa biashara kutoka TZS trilioni 13.6 mwaka 2022 hadi kufikia TZS trilioni 7.2 mwaka 2023. Takwimu toka Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kuwa shughuli mbalimbali za kiuchumi zimeimarika kuvuka kiwango kilichokuwepo kabla ya janga la UVIKO19, hali inayothibitisha kuwa, sio tu uchumi unaimarika kutoka kwenye janga hilo, bali unakuwa kwa kasi ambayo haijawahi kufikiwa kabla. Wakati sekta za kiuchumi zikiendelea kufanya vizuri, mfumuko wa bei umeendelea kushuka ambapo kwa wastani mwaka 2023 ulikuwa asilimia 3 kutoka asilimia 3.2 mwaka 2022, sawa na malengo ya nchi na ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika. Read More
-
Diplomasia ya Uchumi: Mheshimiwa Rais Samia avutia wafanyabiashara zaidi wa Norway kuwekeza Tanzania
Mwanadiplomasia namba moja wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameendelea kutekeleza kwa vitendo Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Diplomasia ya Uchumi, katika ziara zake nje ya nchi kwa kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini pamoja na kukutanisha wafanyabiashara wa ndani na wale wa kimataifa. Matokeo ya mkakati huo yameendelea kuonekana ambapo kwa mwaka 2023 miradi ya uwekezaji iliongezeka kufikia 526 kutoka miradi 293 mwaka 2022, uwekezaji ambapo utazalisha ajira kwa maelfu ya Watanzania, utachochea ukuaji wa biashara, mzunguko wa fedha na kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Katika ziara yake ya kihistoria ya kitaifa nchini Norway Mheshimiwa Rais ameendeleza mkakati huo ambapo akizungumza katika Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Norway ametaja sababu za Tanzania kuwa eneo zuri kwa uwekezaji ikiwa ni pamoja na ukweli kuwa itakuwa moja ya nchi 20 duniani ambazo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi mwaka 2024 kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Aidha, sababu nyingine ni amani chini ya demokrasia imara wa mfumo wa vyama vingi wenye kuzingatia tunu za utawala bora, kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria. Kijiografia, amesema Tanzania inafaa kwa uwekezaji kwani ina Bandari ya Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi, inayohudumia mataifa nane na ina usimamizi madhubuti wa uchumi na sera ya fedha. Rais Samia amesisitiza fursa tano za kipaumbele zikiwemo uwekezaji katika nishati mbadala, kilimo, mafuta na gesi, mifuko ya uwekezaji, miundombinu na usafirishaji. Tanzania na Norway zinaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano ambapo katika mazungumzo ya Rais Samia na viongozi waandamizi wa taifa hilo wamefikia makubaliano ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi kuendana na ukubwa wa historia ya uhusiano uliopo. Read More
-
Watanzania mwaka huu na mwaka 2025 watatimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi ambao watawaongoza kwa miaka mitano ijayo, ambapo katika mchakato wote huo, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameahidi kuwa misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, haki vitadumishwa ili wananchi wapate viongozi wanaostahili. Ili kutimiza azma hiyo, ameeleza kuwa mabadiliko ya sheria zinazosimamia vyama vya siasa na uchaguzi yamefanyika kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na wananchi na wadau mbalimbali baada ya kuunda kikosi kazi huru kupitia mazingira ya kisiasa nchini, ambapo kwa kiasi kikubwa maoni yaliyotolewa yamehimiza kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Maoni mengine ambayo tayari yamefanyiwa kazi ni kubadili jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuakisi uhuru wake. Aidha, amesema baadhi ya maoni yaliyotolewa yalikinzana na Katiba ya nchi, na kuahidi kuwa yatafanyiwa kazi wakati wa maboresho ya kati. “Maboresho haya yatawezesha uchaguzi kufanyika katika mazingira huru na ya haki. Muwe na uhakika kuwa amani na utulivu vitatawala wakati wote kwa gharama yoyote, amesema Rais Samia Suluhu. Akizungumza katika sherehe za mwaka mpya 2024 kwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, amewahakikishia kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo kwa kuzingatia Katiba, tunu za taifa, usawa na umoja wetu wa kitaifa na kwamba watafuta sheria, na uingiliaji wa uchaguzi kutoka nje hautakuwepo. Read More
-
𝐓𝐡𝐚𝐦𝐚𝐧𝐢 𝐲𝐚 𝐮𝐰𝐞𝐤𝐞𝐳𝐚𝐣𝐢 𝐢𝐦𝐞𝐨𝐧𝐠𝐞𝐳𝐞𝐤𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐦𝐢𝐚 𝟖𝟎 𝐃𝐢𝐩𝐥𝐨𝐦𝐚𝐬𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐔𝐜𝐡𝐮𝐦𝐢 𝐧𝐚 𝐮𝐢𝐦𝐚𝐫𝐢𝐬𝐡𝐚𝐣𝐢 𝐦𝐚𝐳𝐢𝐧𝐠𝐢𝐫𝐚 𝐲𝐚 𝐛𝐢𝐚𝐬𝐡𝐚𝐫𝐚 𝐧𝐝𝐢𝐳𝐨 𝐬𝐢𝐫𝐢 𝐳𝐚 𝐦𝐚𝐟𝐚𝐧𝐢𝐤𝐢𝐨 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.4 (takribani TZS trilioni 4) ndani ya miezi mitatu ya mwisho ya mwaka jana, sawa na ongezeko la 80% ikilinganishwa na miradi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 769.6 iliyosajiliwa kipindi kama hicho mwaka 2022. Ongezeko hilo kubwa la uwekezaji limetokana na ziara za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan nje ya nchi ambazo zimevutia wawekezaji kupitia utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi na kuimarishwa kwa mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ambayo yamevutia wawekezaji wengi zaidi. Katika ziara hizo Mheshimiwa Rais Samia amekuwa akiambatana na wafanyabiashara kutoka Tanzania ambao hupata wasaa wa kuzungumza na wafanyabiashara kwenye nchi anazokwenda, hatua ambayo hutoa fursa ya kuwepo ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati yao. Ripoti mpya ya TIC inaonesha kuwa miradi 161 ilisajiliwa kati ya Oktoba-Desemba 2023 ikilinganishwa na miradi 58 kwenye kipindi kama hicho mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 178, ambapo sekta tano zilizoongoza kwenye uwekezaji huo ni viwanda, usafirishaji, huduma, kilimo na utalii. Miradi iliyosajiliwa Oktoba-Desemba 2023 inatarajiwa kutengeneza jumla ya ajira mpya 18,390, kutoka ajira 10,216 za kipindi kama hicho kilichopita kwa mwaka 2022 ambapo mikoa iliyoongoza kwa uwekezaji mkubwa ni Dar es Salaam na Pwani. Aidha, ili kutoa fursa pia kwa wawekezaji wa ndani, pamoja na mambo mengine TIC imeanzisha kampeni maalumu ya kukuza uwekezaji wa ndani lengo likiwa ni kusajili miradi ya uwekezaji wa ndani yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.5 (TZS trilioni 9) ifikapo mwaka 2028. Read More
-
Katika kitabu cha historia na rekodi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa taifa letu, leo amefungua sura mpya ambapo Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa mara ya kwanza limeongeza hisa za umiliki na ushiriki kwenye kitalu cha gesi kwa kununua hisa asilimia 20 kati ya hisa asilimia 31.94 za kampuni ya WentWorth Resources katika kitalu cha gesi asilia cha Mnazi Bay mkoani Mtwara. Kufuatia hatua hiyo, umiliki wa Tanzania kwenye kitalu hicho umefikia asilimia 40, huku kampuni ya Maurel & Prom Tanzania ikinunua hisa asilimia 11.94, na hivyo kufikisha umiliki wa asilimia 60 wa kitalu hicho, na leo kampuni hizo mbili zimesaini mikataba miwili; wa kwanza wa mauziano ya hisa na wa pili wa uendeshaji wa kitalu cha gesi asilia cha Mnazi Bay Hatua ya Tanzania kuongeza umiliki kwenye kitalu hicho ina manufaa mengi ikiwa ni pamona na kuongeza mapato ya Serikali, kuimarisha usalama wa upatikanaji wa nishati nchini, ikiwafahamika kuwa asilimia 65 ya umeme unaotumika nchini ni wa gesi asilia. Manufaa mengine ni kuepusha kitalu kumilikiwa na kuendeshwa na kampuni moja, pamoja na TPDC kuwa na nguvu katika uendeshaji na uendelezaji za kitalu hicho hatua itakayowajengea uwezo zaidi. Kupitia mkataba mpya, sasa uamuzi wa uendeshaji na uendelezaji wa kitalu utafanywa na wanahisa wote, tofauti na awali ambapo Maurel & Prom ambayo ilikuwa inamiliki asilimia 48.05 ilikuwa ifanya shughuli hizo kwa niaba ya wanahisa wengine. Aidha, TPDC imepata haki ya kupeleka wafanyakazi katika shughuli za uendeshaji na uendelezaji kitalu kwa muda mrefu tofauti na awali ambapo walikuwa wanakwenda kwa muda mfupi tu, hivyo kutawajengea uwezo wataalamu wa ndani. Mageuzi haya ya kihistoria yanayofanyika chini ya Mheshimiwa Rais Samia ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (2020-2025) ambayo imeelekeza Serikali kutekeleza mapinduzi ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu ambao ndio wanapaswa kuwa wanufaika wakuu wa… Read More
-
Sera nzuri za uchumi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimi wa Rais Samia Suluhu Hassan zimeendelea kuleta neema kubwa kwenye sekta ya benki nchini, moja ya uthibitisho huo ukiwa ni namna benki za kibiashara zinavyovunja rekodi ya mapato na faida mwaka. Faida ya benki hizo ni ishara ya usimamizi imara wa sera ya fedha inayopelekea uchumi kuwa tulivu na kuwa moja ya uchumi unaokua kwa kasi zaidi duniani pamoja na kutanuka kwa huduma za kifedha zinazoendelea kuifnya Tanzania kusogea karibu zaidi na lengo la kuwa na huduma za kifedha jumuishi. Taarifa za robo ya nne ya mwaka (Oktoba-Desemba 2023) za mabenki ambazo zimechapishwa Januari 2024 zinaonesha kuwa benki mbili kubwa nchini, CRDB na NMB, zinaendelea kuwa vinara wa sekta ya fedha nchini ambapo NMB imevunja rekodi kwa kupata faida ghafi shilingi bilioni 775. Kutokana na mazingira mazuri ya uchumi nchini tangu Rais Samia aingie madarakani NMB imeongeza kiasi cha mikopo inayotoa kwa asilimia 28, hadi kufikia Shilingi trilioni 7.7 mwaka jana, hatua ambayo imewanufaisha maelfu ya wananchi, huku wengine wakinufaika kwa kuwa mawakala na kupata ajira kutokana na kupanuka kwa shughuli za benki hiyo. Kwa upande wa CRDB imeongeza jumla ya mali (total assets) kufikia shilingi trilioni 13.2, amana za wateja (customer deposits) ziliongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 8.8 na mikopo inayotoa imeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 8.8. Benki za biashara zinatarajiwa kuweka rekodi mpya ya faida mwaka huu mpya wa 2024 na kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi kutokana na mazingira mazuri ya uchumi na uwekezaji chini ya serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia. Uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania kuanza kutekeleza Sera ya Fedha kwa kigezo cha riba ya mikopo kwenda benki za kibiashara kunatarajiwa kuinufaisha maradufu Tanzania kwa kuhakikisha ukwasi wa kutosha kwenye shughuli za kiuchumi na kupunguza mfumuko wa bei nchini.… Read More