Tanzania

 • EPUKA UPOTOSHAJI: Tanzania haijatoa bahari wala madini yake kwa Korea

  Mheshimiwa Rais Samia Suluhu yupo nchini Korea ambapo amekamilisha ziara rasmi na sasa anaendelea na ziara ya kikazi hadi Juni 6 mwaka huu, ambapo hadi sasa Tanzania imeendelea kunufaika na ziara hiyo kufuatia kusainiwa kwa mkataba, tamko na hati za makubaliano ambazo zitaimarisha uhusiano uliopo na kufungua fursa mpya za ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wa pande zote. Kufuatia kusainiwa kwa makubaliano hayo, kumekuwa na upotoshaji mitandaoni ambapo moja ya vyombo vya habari kimeeleza kuwa Tanzania imepokea mkopo toka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini. Balozi wa Tanzania nchini Korea, Togolani Mavura amekanusha habari hiyo akieleza kuwa Tanzania haijasaini mkataba wowote na Korea unaohusu bahari wala madini katika ziara ya Mheshimiwa Rais Samia, na kwamba katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais ameshuhudia utiwaji saini wa mkataba mmoja wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu. Mbali na mkataba huo, Mheshimiwa Rais alishuhudia utiwaji saini wa hati za makubaliano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za ushirikiano katika sekta za uchumi wa buluu na madini ya kimkakati pamoja na Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA). Amesisitiza kuwa Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandika, kwani inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu. Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028). Aidha, ameweka wazi kuwa Tanzania ni moja ya nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinazofaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF. Mkopo ambao Tanzania imeupata, tofauti na ilivyopotoshwa na chomho hicho, ni mkopo wa masharti nafuu na una riba ya asilimia 0.01,… Read More

 • Mama Yuko Kazini: Miradi ya uwekezaji yaongezeka mara mbili robo ya kwanza ya 2024

  Mikakati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kupitia Diplomasia ya Uchumi inazidi kuzaa matunda ambapo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili ongezeko la miradi ya uwekezaji kwa asilimia 111, kutoka miradi 100 Januari hadi Machi 2023 hadi miradi 211 kipindi kama hicho mwaka 2024. Thamani ya uwekezaji huo imeongezeka kwa USD milioni 217.98 (TZS bilioni 566.75) kutoka USD bilioni 1.26 (TZS trilioni 3.26) katika robo ya kwanza ya mwaka 2023 hadi kufikia USD bilioni 1.48 (TZS trilioni 3.85) katika robo ya kwanza ya mwaka 2024. Uwekezaji huu utawanufaisha maelfu ya wananchi ambapo idadi ya ajira imeongezeka kufikia 24,931 katika kipindi tajwa kwa mwaka 2024 kutoka ajira 17,016 zilizosajiliwa mwaka jana, sawa na ongezeko la asilimia 46.5. Mafanikio haya ni matokeo ya hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwemo kuboresha Sheria ya Uwekezaji ambayo inatoa msamaha wa ushuru wa forodha wa asilimia 75, imepunguza kiwango cha mtaji wa uwekezaji kwa wazawa toka USD 100,000 hadi USD 500,000. Mengine yaliyofanyika ni kuwa na kituo cha pamoja ambacho mwekezaji atapata huduma zote, kuwezesha usajili wa miradi kwa njia ya mtandao, kufuta au kupunguza ada na tozo, kurahisisha utoaji wa leseni pamoja na kufanya mikutano na wafanyabishara nje ya nchi, hasa kupitia ziara za Mheshimiwa Rais na maonesho mbalimbali, ambavyo vimeendelea kuitangaza nchi yetu na kuendelea kuimarika kwa amani na utulivu nchini.   Read More

 • Mama hana jambo dogo: Uchumi wakua kwa asilimia 5.2 robo ya pili ya mwaka 2023

  Ripoti ya uchumi ya robo ya pili imethibitisha kuwa hatua za kimkakati zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali zinaleta matokeo yanayowezesha uchumi kustahimili na kukua licha ya changamoto za janga UVIKO19, vita ya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya tabianchi. Katika kipindi hicho (Aprili-Juni 2023) ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeonesha kuwa uchumi umekua kwa asilimia 5.2, ikiwa ni hatua kubwa kutoka asilimia 4.7 na asilimia 3.8 zilizorekodiwa kipindi kama hicho mwaka 2022 na mwaka 2021, mtawalia. Shuguli zote za kiuchumi zilizofanyika katika kipindi hicho zimechangia katika ukuaji huo, lakini sekta iliyokuwa na mchango mkubwa zaidi kilimo (11.9%), hali inayoonesha mwitikio mkubwa wa mkazo ambao Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameuweka kwenye kilimo. Sekta nyingine ni usafiri na utunzaji mizigo (11.6%), fedha na bima (10.5%), biashara na ukarabati (10.3%), viwanda (9.2%) na ujenzi 6.9%). Aidha, sekta za kiuchumi zilizoshuhudia ukuaji mkubwa ni huduma za kifedha na bima (15.6%), umeme (12.4%), huduma nyinginezo zinazojumuisha sanaa, burudani na shughuli za majumbani (11.5%) usafiri na uhifadhi mizigo (7.6%), chakula na malazi (7.2%), biashara na ukarabati (7.6%) pamoja na madini (6.3%). Ukuaji huo unalandana na takwimu za ripoti ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) iliyotolewa Oktoba 2023 ambayo imeonesha kuwa uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.2 kwa mwaka 2023 kutoka asilimia 4.7 mwaka 2022, huku ukuaji kwa mwaka 2023 ukitarajiwa kufikia asilimia 6.1. Takwimu za IMF zinaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi 10 za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unatazamiwa kukua kwa kasi. Read More

 • Umoja wa Mataifa: Tanzania ya tatu kwa kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi Afrika

  Licha ya kuwa ukuaji wa bara la Afrika unatarajiwa kushuka kutoka asilimia 4.1 mwaka 2022 hadi asilimia 3.8 mwaka 2023, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua zaidi huku Umoja wa Mataifa (UN) ukiitaja kuwa ni nchi ya tatu barani Afrika kwa kuwa na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi mwaka 2023. Tanzania ambayo inaendelea kuwa mfano Afrika kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, inatarajiwa kushuhudia ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.6, ikitanguliwa na Ivory Coast ambayo uchumi wake utakua kwa asilimia 6.5 pamoja na Rwanda itakayoshuhudia ukuaji wa asilimia 7.8. Mafanikio hayo ni matokeo ya mikakati ya Rais Samia ambapo katika miaka miwili ya uongozi wake amesajili miradi ya uwekezaji ya TZS trilioni 17, ambayo imechochea ukuaji wa sekta nyingine pamoja na kutoa fursa za ajira kwa maelfu ya Watanzania. Mikakati hiyo pia imewezesha uchumi kukabiliana na changamoto za dunia kama mfumuko wa bei, gharama kubwa za ukopaji na mabadiliko ya tabianchi. Wakati ripoti ya UN ikionesha hivyo, Benki ya Dunia (WB) imeitaja Tanzania kuwa nchi ya 10 kwa utajiri barani Afrika kwa kwa kuzingatia Pato Ghafi la Taifa (FDP) kwa kuangalia viwango vya sasa vya kubadili fedha. Ukuaji huo mbali na kuendelea kuboresha maisha ya Watanzania lakini pia unawapa imani wawekezaji waliopo na wanaokusudia kuwekeza nchini, kwa kuwafanya waamini Tanzania ni sehemu salama kuwekeza mitaji yao ya mabilioni, hivyo kufanya uchumi kukua zaidi na zaidi. Read More

 • #MiakaMiwiliYaMama na Diplomasia ya Uchumi: Shilingi ya Tanzania kutumika kununua bidhaa nchini India

  Azma ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji inazaa matunda ambapo Tanzania na India zimefikia makubaliano ya kibiashara ambayo yatawezesha wafanyabiashara kutoka pande zote kutumia fedha zao (shilingi na rupia) katika kufanya miamala ya kibiashara. Nafasi hii itarahisisha biashara ambapo India ni moja ya washirika wakubwa wa kibiashara na Tanzania ambapo thamani ya biashara kati ya nchi hizi ni TZS trilioni 10.4 katika mwaka ulioishia Machi 2022. Takwimu zinaonesha kuwa katika mwaka wa kwanza wa Rais Samia, India iliingiza nchini bidhaa zenye thamani ya TZS trilioni 5.3, huku ikipokea bidhaa za TZS trilioni 5.1 kutoka Tanzania. Utaratibu huu mpya si tu utakuza biashara kati ya mataifa haya kufikia lengo la zaidi ya TZS trilioni 13.8 mwaka huu, bali pia utaziwezesha kutunza akiba ya fedha za kigeni ambao sasa hazitahitajika kufanya miamala. Watanzania wanaofanya kazi katika sekta za kilimo na madini watanufaika zaidi kutokana na sekta hizo kuingiza bidhaa zaidi nchini India. Kwa mujibu wa wachumi na wataalamu wa biashara, uamuzi huo pia utaimarisha utabirikaji wa viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni jambo ambalo ni la muhimu sana katika biashara za kimataifa kwani ina usimamizi wa fedha yake tofauti na awali ilipokuwa ikitumia dola za Marekani. Read More

 • Usuluhushi wa kihistoria wa Mheshimiwa Rais Samia katika migogoro ya ardhi

  Miongoni mwa sifa nyingi zinazomtambulisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na uongozi ni USULUHISHI na UPATANISHI. Sifa hizi mbili zimeonekana katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na siasa na kijamii (masuala ya ardhi). Tukiangazia migogoro ya ardhi, katika mwaka 2021/22, asilimia 86 ya migogoro yote ya ardhi iliyopokelewa ilipatiwa ufumbuzi. Miongoni mwa migogoro hiyo ipo iliyoshindikana kwa muda mrefu huku ikigharimu uhai wa baadhi ya wananchi na mali zao na kuleta mifarakano kwenye jamii. Baadhi tu ya migogoro mikubwa aliyoitatua ni pamoja na; Kwanza, ametatua mgogoro wa Bonde la Usangu mkoani Mbeya uliodumu kwa miaka 15 baada ya kumega eneo lenye ukubwa wa hekta 74,000 kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kilimo na ufugaji. Pili, Mgogoro wa Gereza la King’ang’a na Kata ya Kingale juu ya eneo lenye ukubwa wa ekari 7,495.74 mkoani Dodoma ambapo ameamua ekari 3,272.4 zibaki kwa wananchi watumie kwa shughuli za kilimo, mifugo na za kiuchumi na Magereza wachukue zilizobaki. Tatu, aliruhusu kaya 269 zilizokuwa zinaishi kwenye eneo la kilomita za mraba 9.6 ambazo ni sehemu ya Pori la Akiba Swagaswaga kubaki kwenye eneo hilo, na wananchi hao watapatiwa elimu ya uhifadhi. Ili kupunguza migogoro ya ardhi na kuhakikisha haiwi na madhara zaidi Rais Samia ameendelea kuyawezesha mabaraza ya usuluhishi kutoa uamuzi kwa wakati, elimu kwa wananchi inaendelea kutolewa, mamlaka zinaendelea kupima ardhi kwa ajili ya kuanisha matumizi mbalimbali pamoja na kufanya maboresho ya sheria zinazosimamia sekta ya ardhi. Read More

 • Benki ya Dunia yataja miujiza mitano uchumi wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu

  Benki ya Dunia (WB) imeipongeza Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi hali inayoonekana kama miujiza wakati huu ambapo chumi za nchi mbalimbali duniani zinadorora kutokana na athari za janga la UVIKO19, vita ya Urusi na Ukraine, kupanda kwa bei ya mafuta na mabadiliko ya tabianchi. Akitoa pongezi hizo, Makamu Rais wa Benki ya Dunia wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Victoria Kwaka amesema kuwa wakati nchi mbalimbali zikihangaika na janga la mfumuko wa bei wa tarakimu mbili, huku akiitaja Ghana kuwa na mfumuko wa bei wa 30%, Tanzania imeweza kuwa na mfumuko wa bei wa tarakimu moja tu, ambapo kwa Septemba ulikuwa 4.8%. Athari za kuwa na mfumuko mkubwa wa bei ni kuwa kunapandisha bei za bidhaa, kunapunguza uwezo wa kufanya manunuzi, hivyo kuathiri hali ya maisha ya wananchi. “Tumeona karibu nchi nyingi duniani zikiwa na akiba ndogo ya fedha za kigeni, lakini Tanzania imeweza kuwa na akiba ya fedha za kigeni inayotosha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi mitano,” amesema Kwaka. Fedha za kigeni zinaiwezesha serikali kutimiza mahitaji yake ya fedha za kigeni na mahitaji ya kuagiza bidhaa kutoka nje, kutoa imani kwamba serikali inaweza ikatimiza majukumu yake ya muda mfupi kulipa madeni ya nje na kusaidia utekelezaji wa sera za fedha na kubadilisha fedha za kigeni, pamoja na uwezo wa kuingilia kuhakikisha fedha ya taifa ni imara. Kuhusu nakisi ya bajeti amesema mataifa mataifa mengi yakihangaika kwa kuwa na nakisi kubwa ya bajeti, Tanzania ina nakisi ndogo ya 3.5% ya Pato la Taifa. Nakisi ndogo ya bajeti kwanza ni ishara nzuri kuwa uchumi wa Taifa unaimarika na ina maana kuwa nchi itahitaji kukopa kiasi kidogo cha fedha au kutokuweka kodi kubwa ili kupata fedha za kufadhili bajeti yake. Kwaka pia ameipongeza Tanzania kwa kuwa na sera nzuri za fedha na uchumi zinazoleta utulivu kwenye… Read More