Katiba Mpya

  • Mheshimiwa Rais Samia atoa mwelekeo mchakato wa katiba mpya

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema anatambua umuhimu wa katiba mpya kama ambavyo maoni ya makundi mbalimbali, ikiwemo kikosi kazi, yaliyotolewa na kusisitiza kuendelezwa kwa mchakato huo ambao ulikwama tangu mwaka 2014. Licha wa umuhimu huo ametahadhari kuwa upatikanaji wa katiba mpya ni mchakato na kwamba mchakato huo sio mali ya wanasiasa bali ni ya Watanzania wote, hivyo amewataka wanasiasa kutokuhodhi sauti kwenye mchakato huu. “Katiba ni ya Watanzania, awe ana chama, awe hana, awe ana dini, awe hana, awe mrefu, awe mfupi, mnene, mwembamba, mkubwa, mdogo. Kwa hiyo matengenezo yake yanahitaji tafakuri kubwa sana,” amesema Mheshimiwa Rais. Hata hivyo, amesema kuwa katiba si kitabu, bali ni misingi ya maadili, itikadi na namna ambavyo Watanzania wanakubaliana kuendesha Taifa lao, hivyo, makubaliano hayo yanaandikwa, hivyo, haiwezi kuwa sawa na nchi nyingine. “Tunaanza na elimu Watanzania wajue [katiba] ni kitu gani […] Kwa hiyo tusiwaburuze wananchi. Katiba viongozi wa kisiasa si mali yetu, ni mali ya Watanzania. Tunachokitaka kwenu ni maoni katiba iweje,” ameongeza. Aidha, ameongeza demokrasia lazima iakisi namna watu ndani ya nchi yanavyoendesha masuala yao ikiwemo tamaduni, maadili, mila, desturi, na kwamba huwezi kuchukua demokrasia kutoka nchi nyingine na kuiingiza nchini bila kuzingatia masuala ya ndani. Read More

  • Utayari wa kisiasa wa Rais Samia utakavyoipa Tanzania katiba bora

    Uamuzi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wa kufufua mchakato wa kuipata Katiba Mpya uliokwama tangu mwaka 2014 umeonesha utayari wa kisiasa wa ofisi hiyo ya juu zaidi nchini kuleta Mabadiliko (Reformation) kama alivyoeleza kwenye msingi wa 4R za uongozi wake. Aidha, kurejeshwa mezani kwa mchakato huo kumethibitisha pamoja na mambo mengine kuwa Rais Samia ni msikivu, na anafanyia kazi maoni anayopokea kwa pendekezo la kufufua mchakato huo lilitolewa na kikosi kazi alichokiunda mwaka jana kwa ajili ya kutathmini hali ya kisiasa nchini. Kama wasemavyo Wahenga kuwa Ukimulika Nyoka Anzia Miguuni Pako, ndivyo Rais alivyofanya kwani Kamati Kuu ya CCM, chama anachokiuongoza, Juni 2022 iliielekeza Serikali kuangalia namna ya kufufua mchakato huo ambapo sasa TZS bilioni 9 zimetengwa kwa ajili ya shughuli hiyo. Utayari wake wa kisiasa umeweza kuufikisha mchakato hadi ulipo sasa ambapo mwanga unaonekana kuelekea kulifikia lengo, huku wadau mbalimbali wakimpongeza kwa kuvuka vikwazo vyote ndani ya Serikali na chama chake kwani amewahi kusema yeye mwenyewe kuwa uamuzi huo si kila mmoja anakubaliana nao. Amepongezwa pia kwa namna anavyoufanya mchakato huo kuwa shirikishi ukihusisha majadiliano ya vyama vyote, wanadau na wananchi kwa ujumla akiamkini kuwa maboresho yanayokwenda kufanyika ni kwa ajili ya manufaa ya Watanzania, hivyo ni lazima washirikishwe. Read More