-
Agizo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan la kuboresha mfumo wa elimu ili kumwezesha muhitimu kujiajiri na kuajiriwa baada ya kumaliza masomo yake limefanyiwa kazi ambapo serikali imekamilisha uandaaji na uidhinishaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na mitaala katika ngazi ya elimu ya awali, msingi, sekondari na mafunzo ya ualimu kwa lengo la kufanya elimu inayotolewa iendane na wakati. Kama alivyoelekeza Mheshimiwa Rais Samia, mitaala iliyoboreshwa imezingatia mahitaji ya sasa ikiwa ni pamoja na kuweka msisitizo katika stadi za karne ya 21 ili kumjengea mhitimu stadi za kuwasiliana, kushirikiana, ubunifu na fikra tunduizi. Aidha, kwa upande wa elimu ya kati na elimu ya juu, mapitio ya programu mbalimbali pia yanaendelea kwa lengo la kuifanya iendane na wakati, vipaumbele vya nchi na mahitaji ya soko la ajira ambapo elimu ya juu programu zaidi ya 300 zitahuishwa au kuanzishwa. Uamuzi huo wa kimageuzi wa Mheshimiwa Rais umetokana na uhalisia kwamba mfumo wa elimu wa sasa umejikita zaidi kwenye elimu ya jumla na kukosa fursa za elimu na mafunzo, mitaala kutokidhi mahitaji ya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia, mfumo usio fanisi wa udhibiti na ithibati ya elimu na upungufu wa nguvu kazi. Kwa maboresho hayo ambayo yataanza kutekelezwa mwaka 2027, elimu ya lazima itakuwa ya miaka 10 badala ya saba kama ilivyo sasa, ambapo mtihani wa darasa la saba utafutwa na badala yake kuanza kufanyika kwa tathimini darasa la sita kwa ajili ya kujiunga na elimu ya lazima ya sekondari. Serikali itatoa na kusimamia matumizi ya kitabu kimoja cha kiada kwa kila somo katika elimu ya msingi na sekondari ili kufanikisha upimaji wa matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji unaofanana, pia itaweka utaratibu wa kubaini na kuendeleza wanafunzi wenye vipaji na vipawa mbalimbali. Read More
-
Katika kuendelea kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji hasa kutoka nje ya Tanzania kutumia Bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yao, Serikali ya Tanzania imetenga hekta 20 za ardhi katika Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani kwa ajili ya mizigo inayokwenda Zambia, ikiwa ni sehemu ya kurahisisha ufanyaji biashara. Aidha, kwa kutambua umuhimu wa Zambia katika Bandari ya Dar es Salaam, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mizigo inayokwenda nchini humo itakuwa na kipindi cha neema (bure) kirefu zaidi cha kuhifadhi mizigo yao hadi siku 45, ikiwa ni mkakati wa kupunguza msongamano na ucheleweshaji, na hivyo kupunguza gharama za biashara. Mheshimiwa Rais Samia alisema hayo akihutubia katika maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wa Zambia ambapo alikuwa mgeni rasmi, na kuongeza kuwa “tunatarajia kuwa hatua hii itaongeza biashara kati ya nchi zetu mbili na kuzalisha fursa zaidi kwa ajili ya wananchi wetu. Hii ni zawadi kutoka kwa Tanzania mkisherehekea uhuru wenu.” Zambia ni nchi ye pili kwa kupitisha shehena kubwa ya mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam baada ya DR Congo ambapo kwa mwaka 2022 ilipitisha tani milioni 1.98, sawa na asilimia 24 ya mizigo yote iliyokwenda nje. Aidha, ifahamike kuwa asilimia 80 ya mizigo yote inayopita bandari ya Dar es Salaam kwenda nje ya nchi, inapita katika mpaka wa Zambia, jambo linaloifanya nchi hiyo kuwa mshirika wa kimkakati. Uamuzi wa Mheshimiwa Rais Samia umekuja wakati ambapo Tanzania imeanza mageuzi ya kiutendaji katika Bandari Dar es Salaam yatakayowezesha kupokea meli kubwa zaidi na kutoa huduma kwa kasi, hivyo inaihitaji sana Zambia kuwa na imani na mazingira mazuri ya biashara ili iendelee kuitumia bandari hiyo, badala ya kugeukia bandari shindani. Mbali na bandari, Mheshimiwa Rais Samia ameeleza azma ya Serikali yake kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika ukanda wa kusini na ukanda wa mashariki ili kuongeza usambazaji wa umeme… Read More
-
Tanzania imefungua ukurasa mpya kwenye uwekazaji katika sekta ya uchukuzi kwa kusaini mikataba mitatu na kampuni ya DP World kwa ajili ya uwekezaji bandarini, uwekezaji ambao utashuhudia ufungwaji wa mifumo na mitambo ya kisasa itakayoleta mageuzi kwenye bandari, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha inakuwa kitovu cha biashara na usafirishaji Afrika Mashariki na Kati. Utiaji saini wa mikatanba mitatu ambayo ni mkataba wa nchi mwenyeji (HGA), mkataba wa uendeshaji gati namba 4 hadi 7 na mkataba wa ukodishaji gati namba 4 hadi 7 umetoa majibu kwenye hoja au maswali yaliyoibuliwa na wananchi yaliyotokana na mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai (IGA). Moja ya hoja kubwa iliyoibuka wakati wa mjadala wa IGA ilikuwa ni ukomo wa mikataba, ambapo baadhi ya watoa hoja, hususani wanasiasa na wanaharakati walisema kuwa bandari hizo zimekabidhiwa kwa mwekezaji kwa muda usio na ukomo, wengine wakisema ni miaka 100. Hata hivyo, taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaa ya Bandari Tanzania imeeleza kuwa mikataba hiyo ni ya miaka 30, na kwamba mapitio ya utendaji wa mwekezaji yatafanyika kila baada ya miaka mitano kuona kama anatimiza vigezo alivyowekewa. Pia, baadhi ya watoa hoja walidai kuwa Tanzania haiwezi kujitoa kwenye mikataba, lakini taarifa ya TPA imeeleza kuwa Serikali ya Tanzania inayohaki na inaweza kujitoa kwenye mikataba hiyo pindi itakapoona ni muhimu kufanya hivyo. Aidha, mambo mengine yaliyoelezwa kutoka kwenye mikataba hiyo ambayo yanajibu maswali ya wananchi ni pamoja na sheria za Tanzania kutumika kwenye mikataba husika, serikali kuwa na umiliki wa hisa kwenye kampuni itakayoendesha sehemu ya bandari, mwekezaji kulipa kodi kwa mujibu wa sheria, masuala ya usalama kubaki kwa mamlaka za ndani, hakuna mtumishi wa bandari atakayepoteza kazi yake na kuwa uwekezaji huo utaihusu bandari ya Dar es Salaam. Kwa upande wake Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema maoni ya watu wote… Read More
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali anayoiongoza inatambua na kuthamini mchango wa wachimbaji wadogi katika kuzalisha ajira nchini, na ameahidi kuwa ataendelea kuwaunga mkono kwa kuboresha mazingira ya uchimbaji pamoja na biashara ya madini ili waweze kuboresha maisha yao na kuchangia kwenye uchumi wa taifa. Ametoa ahadi hiyo leo wakati akizindua vifaa vya uchimbaji madini vilivyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambapo ni pamoja mitambo mitano ya kuchoronga, ambayo inatarajiwa kuongezwa kufikia 15 ifikapo Juni 2024. Mitambo mingine ni mitambo 10 ya kutwanga mawe yanayoaminika kuwa na dhahabu, mitambo mitatu ya kuzalisha mkaa mbadala pamoja na makontena ya kusambaza mkaa huo na magari ya STAMICO. Mitambo hiyo ambayo itatumiwa na wachimbaji wadogo nchi nzima itawapunguzia gharama, mfano mtambo wa kuchoronga sasa utakodishwa kwa bei nafuu ikilinganishwa na gharama ya TZS 375,000 ambayo walitozwa na wamiliki binafsi kwa kuchoronga kwa kila mita moja. Mitambo ya kutwanga mawe itaongeza uwezo wao kutoka tani 2 za sasa kwa siku hadi tani 12 kwa siku. Kununuliwa kwa mitambo hiyo ni mwendelezo wa mikakati ya serikali kuwainua wachimbaji wadogo ambapo hatua nyingine zilizochukuliwa ni kufutwa kwa kodi ya ongezeko la thamani ya asilimia 18 pamoja na kodi ya zuio ya asilimia 5 kwa wachimbaji wadogo watakaouza madini yao kwenye masoko ya ndani ya nchi. Kama haitoshi, serikali pia imetoa punguzo la asilimia mbili la mrahaba pamoja na kuondoa asilimia 1 ya ada ya ukaguzi wa madini kwa wachimbaji wa dhahabu ambao wengi wao ni wachimbaji wadogo. “Hii ina maana wale watakaouza dhahabu kwenye viwanda hivyo watapata punguzo la asilimia tatu ya tozo za serikali kwenye mauzo ghafi ya madini yao,” amesema Mheshimiwa Rais Samia akiongeza kuwa hatua hizo ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoielekeza serikali kubuni na kuendeleza mikakati ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo kufanya shughuli zao kwa… Read More
-
Ripoti ya uchumi ya robo ya pili imethibitisha kuwa hatua za kimkakati zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali zinaleta matokeo yanayowezesha uchumi kustahimili na kukua licha ya changamoto za janga UVIKO19, vita ya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya tabianchi. Katika kipindi hicho (Aprili-Juni 2023) ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeonesha kuwa uchumi umekua kwa asilimia 5.2, ikiwa ni hatua kubwa kutoka asilimia 4.7 na asilimia 3.8 zilizorekodiwa kipindi kama hicho mwaka 2022 na mwaka 2021, mtawalia. Shuguli zote za kiuchumi zilizofanyika katika kipindi hicho zimechangia katika ukuaji huo, lakini sekta iliyokuwa na mchango mkubwa zaidi kilimo (11.9%), hali inayoonesha mwitikio mkubwa wa mkazo ambao Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameuweka kwenye kilimo. Sekta nyingine ni usafiri na utunzaji mizigo (11.6%), fedha na bima (10.5%), biashara na ukarabati (10.3%), viwanda (9.2%) na ujenzi 6.9%). Aidha, sekta za kiuchumi zilizoshuhudia ukuaji mkubwa ni huduma za kifedha na bima (15.6%), umeme (12.4%), huduma nyinginezo zinazojumuisha sanaa, burudani na shughuli za majumbani (11.5%) usafiri na uhifadhi mizigo (7.6%), chakula na malazi (7.2%), biashara na ukarabati (7.6%) pamoja na madini (6.3%). Ukuaji huo unalandana na takwimu za ripoti ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) iliyotolewa Oktoba 2023 ambayo imeonesha kuwa uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.2 kwa mwaka 2023 kutoka asilimia 4.7 mwaka 2022, huku ukuaji kwa mwaka 2023 ukitarajiwa kufikia asilimia 6.1. Takwimu za IMF zinaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi 10 za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unatazamiwa kukua kwa kasi. Read More
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa Tanzania inalenga kusajili miradi ya uwekezaji kutoka nje (FDI) yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 15 (TZS trilioni 37.5) ifikapo mwaka 2025. Ameweka wazi mpango huo wakati akizungumza na wafanyabiashara wakubwa wa India katika jukwaa la uwekezaji la India na Tanzania jijini New Delhi ambapo amesema ili kufanikisha azma hiyo Serikali yake imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuboresha mfumo wa kisheria kwa kuufanya kuwa rafiki zaidi. Ameeleza kuwa Serikali yake inatambua umuhimu wa sekta binafsi na uwekezaji kama vichocheo vya ukuaji wa kiuchumi, hivyo mazingira ya biashara yameboreshwa ili kupanua biashara zilizopo na kuvutia uwekezaji mpya, jambo ambalo ni moja ya malengo ya ziara yake ya kimkakati nchini India. Kama sehemu ya mageuzi makubwa, Tanzania imeboresha matumizi ya teknolojia kuruhusu wawekezaji kusajili miradi popote pale duniani kupitia dirisha la kuhudumia wawekezaji kielektroniki, na hivyo kupata majibu kabla hata ya kutembelea Tanzania. “Tumepiga hatua kutoka kusajili uwekezaji wa dola bilioni 2 [TZS trilioni 5] mwaka 2020 hadi dola bilioni 5 [TZS trilioni 12.5] katika mwaka ulioishia Juni 2023. Lengo letu ni kufikia dola bilioni 15 kwa mwaka ifikapo mwisho wa 2025,” amesema. Tangu mwaka 1997 Tanzania imepokea jumla ya dola bilioni 3.87 za uwekezaji katika miradi 675 kutoka India ambayo imezalisha ajira zaidi ya 61,000, hivyo kufanya India kuwa miongoni mwa wawekezaji watano bora nchini Tanzania. Read More
-
Tanzania na India zimefikia makubaliano ya kuongeza matumizi ya fedha za nchi husika katika biashara, badala ya kutegemea dola ya Marekani kama ilvyokuwa hapo awali. Azimio hilo limefikiwa katika mazungumzo kati ya Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi ambapo itawezesha kupunguza mfumuko wa bei tofauti na awali ambapo Tanzania ingelazimika kutumia fedha nyingi kupata dola ya Marekani ili kuagiza bidhaa. Utekelezaji wa uamuzi huo ulishaanza kufanyiwa kazi ambapo hadi sasa biashara yenye thamani ya TZS bilioni 125 imefanyika kwa fedha za nchi husika, hatua inayodhihirisha utayari wa nchi zote kutekeleza makubaliano haya, na sasa hatua inayofuata ni kuongeza matumizi ya fedha hizo. Katika hatua nyingine, India na Tanzania zimebadili uhusiano wao kutoka wa kawaida kidiplomasia kuwa wa mkakati, ambapo nchi zote mbili zimeainisha maeneo mahususi ya kushirikiana yenye maslahi kwa pande zote mbili. Tanzania inatarajia kuendelea kunufaika na ushirikiano wake wa kimkakati na India ikizingatiwa kuwa ni nchi ya tano kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani, ikiwa imepiga hatua katika sekta za afya, TEHAMA, nishatia, miundombinu, ulinzi na usalama ambazo ni kipaumbele kwa Tanzania. Hadi mwaka 2022, kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kilifikia TZS trilioni 7.7, hivyo kuifanya India kuwa mshirika wa tatu kwa ukubwa katika biashara na mwekezaji wa tano kwa ukubwa nchini Tanzania. Read More
-
Mwaka 2022 Tanzania iliuza zaidi bidhaa zake nchini India, biashara ambayo ilichangia asilimia 17.3 ya mauzo yote, huku India ikiwa ni nchi ya tatu ambayo Tanzania iliagiza bidhaa nyingi zaidi (asilimia 12.5), takwimu ambazo zinadhihirisha namna mataifa haya yanauhusiano wa kibiashara wenye manufaa kwa pande zote. Katika muktadha wa kukuza zaidi biashara na ushirikiano katika sekta nyingine, Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kimkakati ya kitaifa ya siku tatu nchini India (Oktoba 8-10, 2023) kwa mwaliko wa Serikali ya India, ziara ambayo inatarajiwa kuwa matokeo chanya kwa Tanzania hasa katika sekta za afya, diplomasia, elimu, biashara na uwekezaji, uchumi wa bluu, maji, kilimo na teknolojia. Ziara hiyo ni kubwa kwani inafanyika miaka na tangu kiongozi wa mwisho wa Tanzania kutembelea nchi hiyo, na inatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa miaka 62 wa nchi hizo, ambao chimbuko lake ni Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Waziri Mkuu wa India, Hayati Jawaharlal Nehru. Ziara ya Mheshimiwa Rais nchini India ina malengo makubwa mawili ambayo ni kudumisha, kuimarisha na kuendelea uhusiano uliopo katika sekta takribani 10 na kufungua fursa za biashara na uwekezaji, ikifahamika kuwa India ni moja ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani na ni moja yenye miradi mingi ya uwekezaji nchini. Matarajio ya mafanikio kutokana na ziara hiyo; ELIMU 1. Fursa za mafunzo kwa Watanzania katika nyanja mbalimbali nchini India ambapo kwa kuanzia kutatolewa nafasi 1,000. BIASHARA VYA UWEKEZAJI 1. Kuongezeka kwa uwekezaji nchini hasa viwanda vya kutengeneza simu na vifaa vya kielektroniki AFYA 1. Kuanzishwa kwa taasisi ya upandikizaji wa figo hapa nchini 2. Kuanzishwa kwa kiwanda cha kutengeneza chanjo za binadamu na wanyama 3. Kuongeza ushirikiano kati ya hospitali za Tanzania na India ili kuimarisha uwezo na weledi katika utoaji wa huduma za afya. 4. Kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa (ubora na unafuu)… Read More
-
Doha- Qatar: Oktoba 2 mwaka huu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki uzinduzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Mboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) ambayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kujifunza na kuwekeza katika kilimo, hususani kwenye teknolojia rafiki ya mazingira. Kazi kubwa ya kuimarisha sekta ya mboga na matunda inayagusa moja kwa moja maisha ya vijana na wanawake ambao ndio wanufaika wakubwa wa ajira takribani milioni 6.5 zinazotokana na sekta, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa familia na taifa kwa ujumla. Ushiriki wake kwenye jukwaa hilo la kimataifa ni mwendelezo wa mageuzi ya kilimo aliyoyaanzisha nchini ambapo Serikali ya Tanzania kupitia taasisi zake mbalimbali na sekta binafsi inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutafuta masoko ya mazao ya kilimo pamoja na kuvutia uwekezaji kwenye sekta hiyo iliyoajiri zaidi ya asilimi 65 ya Watanzania. Mkakati wa Mheshimiwa Rais ni kuona kilimo kinakuwa kwa wastani wa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030, ambapo mbali na kufungua fursa za masoko kimataifa, hatua nyingine za kimkakati alizochukua kutimiza lengo ni pamoja na upatikanaji wa mbegu bora, miundombinu ya umwagiliaji, utafiti na upatikanaji wa mbolea nafuu na viuatilifu. Juhudi hizi zinalenga kupunguza gharama za uzalishaji kwa mkulima na kuongeza tija na uzalishaji, kuimarisha usalama wa chakula nchini na kuiwezesha Tanzania kuuza chakula nje, ikiendelea ushiriki wake katika kuongeza usalama wa chakula duniani na kutunza mazingira kwa wakati mmoja. Read More