Uwekezaji
-
Mikakati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kupitia Diplomasia ya Uchumi inazidi kuzaa matunda ambapo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili ongezeko la miradi ya uwekezaji kwa asilimia 111, kutoka miradi 100 Januari hadi Machi 2023 hadi miradi 211 kipindi kama hicho mwaka 2024. Thamani ya uwekezaji huo imeongezeka kwa USD milioni 217.98 (TZS bilioni 566.75) kutoka USD bilioni 1.26 (TZS trilioni 3.26) katika robo ya kwanza ya mwaka 2023 hadi kufikia USD bilioni 1.48 (TZS trilioni 3.85) katika robo ya kwanza ya mwaka 2024. Uwekezaji huu utawanufaisha maelfu ya wananchi ambapo idadi ya ajira imeongezeka kufikia 24,931 katika kipindi tajwa kwa mwaka 2024 kutoka ajira 17,016 zilizosajiliwa mwaka jana, sawa na ongezeko la asilimia 46.5. Mafanikio haya ni matokeo ya hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwemo kuboresha Sheria ya Uwekezaji ambayo inatoa msamaha wa ushuru wa forodha wa asilimia 75, imepunguza kiwango cha mtaji wa uwekezaji kwa wazawa toka USD 100,000 hadi USD 500,000. Mengine yaliyofanyika ni kuwa na kituo cha pamoja ambacho mwekezaji atapata huduma zote, kuwezesha usajili wa miradi kwa njia ya mtandao, kufuta au kupunguza ada na tozo, kurahisisha utoaji wa leseni pamoja na kufanya mikutano na wafanyabishara nje ya nchi, hasa kupitia ziara za Mheshimiwa Rais na maonesho mbalimbali, ambavyo vimeendelea kuitangaza nchi yetu na kuendelea kuimarika kwa amani na utulivu nchini. Read More
-
Mwanadiplomasia namba moja wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anaendelea kutekeleza kwa vitendo Diplomasia ya Uchumi ambapo sasa Tanzania inakusudia kuvutia uwekezaji wa dola za Kimarekani bilioni 1 (zaidi ya TZS trilioni 2.5) ndani ya miaka michache ijayo, kutoka uwekezaji wa sasa wenye thamani ya TZS bilioni 6.5 ambao umefanyika katika sekta za kilimo, uzalishaji wa viwandani na ujenzi. Ameeleza hayo akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia na ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wafanyabiashara na wawekezaji wa Indonesia sababu zinazowafanya kwanini Tanzania ni sehemu nzuri zaidi kuwekeza. Kwanza amesema ni amani na utulivu uliyopo nchini na Serikali inayofuata misingi ya demokrasia na utawala bora, pili ni eneo la kimkakati la Tanzania ambayo imepaka na nchi nane na ni lango kwa nchi sita kupitia anga, barabara, reli na maji. Aidha, amesema Tanzania inatoa uhakika wa soko la bidhaa zao kwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 61, huku pia ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye watu milioni 281.5, Jumuiya ya Mendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu milioni 390 na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfFTA) lenye watu bilioni 1.2. Tatu ni Tanzania kuwa na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuridhia sheria na mikataba ya kimataifa inayolinda mitaji na uwekezaji wa kigeni. Nne ni utashi wa kisiasa na nafasi ya Serikali kutambua umuhimu wa sekta binafsi kama injini ya maendeleo ya kiuchumi na kuweka msimamo wa kusaidia biashara na wafanyabiashara kukua. Sababu ya tani ni usimamizi imara wa sera ya fedha na uchumi unaowezesha uchumi kuzidi kukua na kufikia viwango vya kabla ya janga la UVIKO19. Kuthibitisha hilo, ripoti ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) imeitaja Tanzania kama moja ya nchi 20 duniani ambazo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi mwaka 2024. Katika ziara yake… Read More
-
Ripoti ya uchumi ya robo ya pili imethibitisha kuwa hatua za kimkakati zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali zinaleta matokeo yanayowezesha uchumi kustahimili na kukua licha ya changamoto za janga UVIKO19, vita ya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya tabianchi. Katika kipindi hicho (Aprili-Juni 2023) ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeonesha kuwa uchumi umekua kwa asilimia 5.2, ikiwa ni hatua kubwa kutoka asilimia 4.7 na asilimia 3.8 zilizorekodiwa kipindi kama hicho mwaka 2022 na mwaka 2021, mtawalia. Shuguli zote za kiuchumi zilizofanyika katika kipindi hicho zimechangia katika ukuaji huo, lakini sekta iliyokuwa na mchango mkubwa zaidi kilimo (11.9%), hali inayoonesha mwitikio mkubwa wa mkazo ambao Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameuweka kwenye kilimo. Sekta nyingine ni usafiri na utunzaji mizigo (11.6%), fedha na bima (10.5%), biashara na ukarabati (10.3%), viwanda (9.2%) na ujenzi 6.9%). Aidha, sekta za kiuchumi zilizoshuhudia ukuaji mkubwa ni huduma za kifedha na bima (15.6%), umeme (12.4%), huduma nyinginezo zinazojumuisha sanaa, burudani na shughuli za majumbani (11.5%) usafiri na uhifadhi mizigo (7.6%), chakula na malazi (7.2%), biashara na ukarabati (7.6%) pamoja na madini (6.3%). Ukuaji huo unalandana na takwimu za ripoti ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) iliyotolewa Oktoba 2023 ambayo imeonesha kuwa uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.2 kwa mwaka 2023 kutoka asilimia 4.7 mwaka 2022, huku ukuaji kwa mwaka 2023 ukitarajiwa kufikia asilimia 6.1. Takwimu za IMF zinaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi 10 za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unatazamiwa kukua kwa kasi. Read More