Tume ya Mipango

  • Maeneo 8 ya vipaumbele ya Mheshimiwa Rais Samia uandaaji wa Dira ya 2050

    Tanzania ipo katika mchakato wa kuandaa dira mpya ya Taifa ya maendeleo ya miaka 25 (mwaka 2025 hadi mwaka 2050) ambayo itakuwa ni dira ya pili kuandaliwa nchini baada ya ile iliyoanza mwaka 2000 na inatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Akizindua mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi kwa ajili ya kuandaa dira mpya, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameainisha maeneo nane ya kipaumbele katika dira mpya ambayo yanatokana na mahitaji ya sasa ya dunia, makosa na mafanikio yaliyotokana na utekelezaji wa dira inatoelekea ukomo pamoja na mahitaji mengine ya kitaifa. Kwanza, ukuaji wa uchumi kufungamanishwa na sekta za uzalishaji zinazowagusa wananchi wengi zaidi na kutengeneza ajira kwaajili yao kama vile sekta ya kilimo. Pili, kukusanywa kwa takwimu kutoka sekta isiyo rasmi ili kupata hali halisi ya uchumi badala ya kutumia takwimu za sekta rasmi pekee, hali inayosababisha kukosa uhalisia wa hali ya uchumi. Eneo la tatu ni tathmini na ufuatiliaji ambao utawezesha kubaini viashiria vya kasoro kwenye utekelezaji wa dira mapema na kuzifanyia kazi ili kuhakikisha malengo yanafikiwa. Nne, uratibu wa kufungamanisha miradi ya kipaumbele kwa sekta zinazohusika katika uzalishaji. Katika hili Mheshimiwa Rais amesisitiza kuwa mipango ya sekta moja inapotekelezwa iwe na mwingiliano na mchango katika sekta nyingine ili kutumia rasilimali chache kwa matokeo makubwa. Tano, amesisitiza dira iweke mwelekeo wa uwekezaji na usimamizi wa maboresho ya kiutendaji wa mashirika ya serikali ili yaongeze ufanisi katika uendeshaji na yaweze kuhimili ushindani wa kikanda na kimataifa. Ushiriki wa sekta binafsi katika kukuza uchumi ni eneo la sita alilolitaja ambapo amesema lazima sekta binafsi iimarishwe na iwe tayari kuimarika ili ziwe na uwezo na utayari wa kufanya biashara, kutengeneza ajira pamoja na kushirikiana na sekta binafsi nje ya nchi. Uimarishaji huo unajumuisha uwepo wa mifumo rafiki ya kisheria, upatikanaji wa mitaji na rasilimali watu yenye ujuzi. Kuzingatiwa kwa maadili ya Taifa ni sehemu… Read More

  • Rais Samia airejesha Tume ya Mipango kwa sura mpya ili kuchochea maendeleo nchini

    Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anaiunda upya Tume ya Mipango ambayo itakuwa chini ya Rais ikiwa na jukumu la kubuni, kupanga, kuratibu na kusimamia mipango ya maendeleo ili kuwa na mfumo jumuishi wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa vipaumbele vya maendeleo ya Taifa. Kuunda upya kwa tume hiyo na kuiweka chini ya Rais ni kuendelea kuyaishi maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye kwa mara ya kwanza alianzisha mwaka 1962 ikiwa ni idara ambapo wakati wa uanzishaji wake walisema “Nakusudia kuanzisha idara mpya, idara ya mipango ya maendeleo, idara hiyo itakuwa chini yangu mwenyewe.” Uamuzi wa Rais kurejesha tume hiyo utawezesha uwepo wa utaratibu wa kupanga pamoja mipango ya kisekta, hususani sekta zenye majukumu yanayotegemeana na kuwa na mfumo wa kisheria na chombo mahsusi cha kusimamia uandaaji, utekkelezaji wa mipango ya maendeleo, utafiti na kuishauri Serikali kuhusu vipaumbele vya maendeleo ya Taifa. Majukumu haya kwa sasa yanatekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, lakini kumekuwepo na changamoto ya miradi inayoendana kutekelezwa kwa nyakati tofauti sehemu husika, mfano barabara inajengwa baada ya muda inavunjwa ili kupitisha bomba la maji. Hivyo kuwepo kwa tume maalum chini ya ofisi ya Rais kutaondoka mkanganyiko huo ili miradi kama hiyo itekelezwe kwa wakati mmoja ili kuleta ufanisi na kuipunguzia serikali gharama zisizo za lazima. Aidha, tofauti na tume iliyokuwepo awali ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa hati idhini (instruments) tume mpya itakuwa na hadhi ya kisheria ambayo itaipa tume nguvu zaidi na kulinda mawazo yanayotolewa na kuleta utofauti katika mfumo wa uendeshaji. Read More