Maendeleo Tanzania
-
Moja ya mikakati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoiweka wazi baada ya kuingia madarakani ni kutoa fursa zaidi kwa Watanzania waishio nje kushiriki katika shughuli za maendeo na kijamii nchini kwa kuweka mazingira yatakayowawezesha kufanya shughuli zao nchini. Mafanikio yameendelea kuonekana ambapo kwa mwaka 2022 pekee diaspora walituma nchini TZS trilioni 2.6, na pia wamewekeza kupitia ununuzi wa nyumba na viwanja wenye thamani ya TZS bilioni 4.4 na ununuzi wa hisa za TZS bilioni 2.5. Ili kupanua ushiriki wa diaspora katika maendeo ya Tanzania Serikali inatarajia kuwa imekamilisha mfumo wa kidigitali wa uandikishaji wa diaspora Juni mwaka huu ili kuwezesha ukusanyaji endelevu wa takwimu zao. Mbali na kutuma fedha na kuwekeza nchini, diaspora pia huchangia ukuaji wa uchumi kwa kutangaza fursa za kiuchumi, biashara, utalii na uwekezaji zinazopatikana nchini. Mchango mwingine ni kuleta mitaji, utaalam na teknolojia ambavyo huchangia katika kukuza uzalishaji wa mazao, bidhaa na huduma mbalimbali zenye tija kiuchumi. Hadi sasa idadi ya diaspora wa Tanzania ni milioni 1.5, idadi ambayo Rais anaamini itakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi ikiwekewa mazingira rafiki. Read More
-
Wanafunzi zaidi ya milioni 1 wakianza kidato cha kwanza kwa pamoja leo Januari 9, 2023, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amevuka lengo la ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambao umetoa nafasi kwa kila mwenye sifa kuanza masomo kwa wakati. Katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26), Serikali ilikuwa imepanga kujenga vyumba vya madarasa 4,040, ambapo kwa mwaka 2022 pekee Serikali imejenga madarasa 8000, ikiwa ni takribani mara mbili ya lengo. Kwa ujumla katika miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Serikali imejenga madarasa 2,3000 katika ngazi zote za elimu, huku ikikarabati yaliyokuwa yamechakaa pamoja na kujenga shule mpya zikiwemo shule maalum za sayansi za wasichana kila mkoa. Kwa miaka miwili ya uongozi wake, Rais Samia ameweka rekodi iliyowezesha wanafunzi wote wanaoanza kidato cha kwanza kufanya hivyo kwa pamoja, hivyo kuondoa utaratibu wa chaguzi za awamu ya pili au zaidi, ambazo hushuhudia wanafunzi wakichelewa kuanza masomo. Mafanikio haya ni utekelezaji wa dira ya Serikali anayoiongoza ambayo inalenga kuboresha elimu nchini na kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anayekosa fursa ya masomo kwa uhaba wa madarasa. Read More