fedha za Kigeni
-
Dar es Salaam, Tanzania – Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uchumi wa nchi, ambapo sasa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imechukua hatua kubwa ya kimkakati ya kununua dhahabu ya ndani ili kuimarisha hifadhi ya fedha za kigeni na kuongeza nguvu ya shilingi ya Tanzania. Tayari BoT inanunua dhahabu kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa ndani kwa kutumia shilingi ya Tanzania ambapo tayari imenunua kilogramu 418, lengo likiwa ni kununua kilogramu 6,000 katika mwaka wa fedha 2023/24. Hatua hii muhimu ina manufaa mbalimbali kwa taifa na wananchi kwa kununua dhahabu kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni, taifa letu linajikinga dhidi ya athari zitokanazo na mabadiliko ya ghafla (kutokuwepo kwa uhakika) ya kiuchumi wa kimataifa. Dhahabu imekuwa kimbilio la thamani kwa miongo mingi wakati wa migogoro ya kiuchumi na kisiasa duniani. Kwa hivyo, kwa kuchanganya dhahabu katika akiba ya fedha za kigeni, Tanzania inaweza kusaidia kulinda thamani ya shilingi ya nchi wakati wa mazingira magumu ya kiuchumi duniani. Pia, hatua ya kununua dhahabu kutoka kwa wazalishaji wa ndani kutachangia kukuza uchumi wa ndani kwani itachochea uzalishaji wa dhahabu. Kukua kwa uzalishaji kunaenda moja kwa moja na kuongezeka kwa ajira, kwani shughuli za uchimbaji na biashara ya dhahabu zinahitaji wafanyakazi, na pia ongezeko la wachimbaji litanufaisha sekta nyingine zinazofungamana na sekta hiyo ikiwemo ya huduma (chakula, maji, nishati, mawasiliano). Uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania wa kununua dhahabu kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni na kulinda uchumi unathibitisha nia ya serikali ya kusimamia utulivu wa kiuchumi na kujenga nguvu za kifedha, hatua ambayo inaweza kuwa na athari chanya kwa maendeleo na ustawi wa nchi. Read More
-
Benki ya Dunia (WB) imeipongeza Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi hali inayoonekana kama miujiza wakati huu ambapo chumi za nchi mbalimbali duniani zinadorora kutokana na athari za janga la UVIKO19, vita ya Urusi na Ukraine, kupanda kwa bei ya mafuta na mabadiliko ya tabianchi. Akitoa pongezi hizo, Makamu Rais wa Benki ya Dunia wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Victoria Kwaka amesema kuwa wakati nchi mbalimbali zikihangaika na janga la mfumuko wa bei wa tarakimu mbili, huku akiitaja Ghana kuwa na mfumuko wa bei wa 30%, Tanzania imeweza kuwa na mfumuko wa bei wa tarakimu moja tu, ambapo kwa Septemba ulikuwa 4.8%. Athari za kuwa na mfumuko mkubwa wa bei ni kuwa kunapandisha bei za bidhaa, kunapunguza uwezo wa kufanya manunuzi, hivyo kuathiri hali ya maisha ya wananchi. “Tumeona karibu nchi nyingi duniani zikiwa na akiba ndogo ya fedha za kigeni, lakini Tanzania imeweza kuwa na akiba ya fedha za kigeni inayotosha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi mitano,” amesema Kwaka. Fedha za kigeni zinaiwezesha serikali kutimiza mahitaji yake ya fedha za kigeni na mahitaji ya kuagiza bidhaa kutoka nje, kutoa imani kwamba serikali inaweza ikatimiza majukumu yake ya muda mfupi kulipa madeni ya nje na kusaidia utekelezaji wa sera za fedha na kubadilisha fedha za kigeni, pamoja na uwezo wa kuingilia kuhakikisha fedha ya taifa ni imara. Kuhusu nakisi ya bajeti amesema mataifa mataifa mengi yakihangaika kwa kuwa na nakisi kubwa ya bajeti, Tanzania ina nakisi ndogo ya 3.5% ya Pato la Taifa. Nakisi ndogo ya bajeti kwanza ni ishara nzuri kuwa uchumi wa Taifa unaimarika na ina maana kuwa nchi itahitaji kukopa kiasi kidogo cha fedha au kutokuweka kodi kubwa ili kupata fedha za kufadhili bajeti yake. Kwaka pia ameipongeza Tanzania kwa kuwa na sera nzuri za fedha na uchumi zinazoleta utulivu kwenye… Read More