Vijana vyuo Vikuu
-
Moja ya ahadi za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ilani ya mwaka 2020-2025 ni kutengeneza ajira zisizopungua milioni 8 katika sekta rasmi na isiyo rasmi kwa ajili ya vijana nchini. Ndani ya muda mfupi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameendelea kuweka mikakati ya kufikia lengo hilo ambapo anaendelea kutoa ajira rasmi kwenye kada mbalimbali, ameboresha mazingira ya biashara yanayowezesha vijana kujiajiri na kupata ajira kupitia uwekezaji unaosajiliwa nchini pamoja na kuwezesha upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya ujasirimali kwa vijana nchini. Kwa kutambua umuhimu mkubwa wa vijana katika maendeleo ikiwa ndio nguvu kazi kubwa, Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo ya TZS bilioni 1.88 kwa ajili ya kuwezesha miradi 85 ya vijana katika sekta za kilimo, viwanda na biashara kwenye halmashauri 28. Aidha, Serikali imetoa fursa za mafunzo ya ujuzi wa kujiajiri au kuajiriwa kwa vijana 118,415 katika fani za uanagenzi, uzoefu wa kazi, ufugaji wa samaki na viumbe maji na kilimo cha kisasa kwa njia ya vizimba. Pamoja na hayo, Serikali imefungua fursa zaidi kupitia kilimo, TEHAMA na pia vijana na wajasiriamali wengine wanaofungua biashara mpya wamepewa neema ya miezi sita hadi mwaka mmoja kutokulipa kodi tangu kuanza kwa biashara zao, mpango unaolenga kulea biashara ndogo ili ziweze kukua zaidi. Read More