Utalii Tanzania

  • Royal Tour Imejibu: Utalii waongoza katika kuingiza fedha za kigeni

    Kazi kubwa aliyoifanya na inayoendelea kufanywa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza fursa za utalii unaweza kusema ‘imejibu’ baada ya sekta hiyo kuendelea kuimarika na kupita madini ya dhahabu katika kuiingizia nchi fedha za kigeni, ikiwa ni kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne tangu ilipoanza kushuka. Mlipuko wa janga la kidunia la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO) mwaka 2019 kuliiathiri sekta hiyo ambapo mchango wake kwenye fedha za kigeni ulishuka kutoka dola za kimarekani bilioni 2.52 (TZS trilioni 6.3) mwishoni mwa mwaka 2019 hadi dola za Kimarekani bilioni 1 (TZS trilioni 2.5) mwishoni mwa mwaka 2020, na hivyo kupelekea dhahabu iliyoingiaza dola za Kimarekani bilioni 2.9 (TZS trilioni 7.2) kuongoza. Kuhakikisha sekta ya utalii ambayo inatoa ajira zaidi ya milioni 1.6, inachangia asilimia 25 ya fedha za kigeni na asilimia 21 ya Pato la Taifa inaimarika, Mheshimiwa Rais Samia alichukua jukumu la kurekodi filamu ya Tanzania: The Royal Tour ambayo ilizinduliwa nchini Marekani na hivyo kuiwezesha nchi kutangaza fursa za utalii na vivutio vya utalii kwa mamilioni ya watu dunia, hatua ambayo imepelea kuendelea kuongezeka kwa watalii kutoka ndani na nje ya nchi. Matokeo yameendelea kuonekana ambapo takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kuwa mapato yatokanayo na utalii yamepanda kufikia dola za Kimarekani bilioni 2.999 (TZS trilioni 7.5) katika mwaka ulioishia Julai 2023 kutoka dola za Kimarekani bilioni 1.95 (TZS trilioni 4.8) mwaka ulioishia Julai 2022, huku mapato ya dhahabu kwa mwaka ulioishia Julai 2023 yakiwa dola za Kimarekani bilioni 2.9 (TZS trilioni 7.3). Mafanikio hayo yametokana na kuendeleo kuongezeka kwa watalii kutoka nje ya nchi ambapo ripoti ya BoT inaonesha kuwa watalii wameongezeka kwa asilimia 37.2 kufikia 1,658,043 katika mwaka huo, idadi ambayo haijawahi kufikiwa kabla. Licha ya mafanikio haya, Mheshimiwa Rais Samia anaendelea kutangaza utalii ili kufikia lengo la watalii milioni 5 ifikapo… Read More

  • Rais Dkt. Samia atunukiwa tuzo ya kimataifa kukuza sekta ya utalii

    Utendaji kazi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umeendelea kutambulika kimataifa ambapo siku chache tangu atajwe miongoni mwa wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka wa pili mfululizo, sasa ametunukiwa tuzo ya Mwongozaji Bora wa Watalii, tuzo iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Awards ya nchini India. Taasisi hiyo imemtunuku Dkt. Samia tuzo hiyo kutokana na mchango wake katika uandaaji wa filamu ya Tanzania: The Royal Tour ambayo imekuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza sekta ya utalii, hasa baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO19 tangu mwaka 2019. Akipokea tuzo hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana amesema itaipa Serikali ari ya kuendelea kuboresha sekta ya utalii ambayo imeendelea kukua ambapo mwaka 2021 Tanzania ilipokea watalii 992,692 lakini mwaka 2022 tayari imepokea watalii zaidi ya milioni 1, huku wengine wakiendelea kuingia. Mbali na kutangaza utalii filamu hiyo imeonesha fursa za biashara na uwekezaji zilizomo nchini ambapo wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali, ikiwemo Marekani, wamefika nchini kwa ajili ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji. Read More