Tozo za miamala ya simu
-
Watumiaji wa huduma za kifedha kwa simu wenye akaunti zaidi ya milioni 44 wamefurahia hatua ya serikali ya kuondoa tozo ya kutumia fedha, hatua ambayo imeanza kutekelezwa na kampuni za mawasiliano ya simu kuanzia Julai Mosi mwaka huu ili kuondoa utozaji tozo mara mbili kwenye muamala mmoja. Utekelezaji huo ni matokeo ya Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuifanyia marekebisho Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Sura ya 437 ambapo lengo ni kuchochea ufanyaji wa miamala kwa njia za kielektroniki ili kukuza uchumi wa kidijiti (cashless economy). Watoa huduma za mawasiliano na wananchi waliotoa maoni yao kuhusu uamuzi huo wamesema kuondolewa kwa tozo za Serikali kumepunguza gharama ya kutuma fedha, hatua itakaypchochea ongezeko la miamala kwa njia ya simu, hasa kwa kufanya malipo kwenye biashara na huduma mbalimbali. Kwa miaka ya karibuni huduma za kifedha kwa njia ya simu imekuwa mkombozi kwa wananchi wengi hasa vijijini ikiwapa uwezo wa kuweka akiba, kukopa, bima, huduma ambazo zinachochea ustawi wa jamii. Katika muktadha wa kupanua huduma za mawasiliano na kuyafanya kuwa nafuu zaidi, Serikali imepunguza gharama za kupitisha miundombinu ya mawasiliano kwenye hifadhi ya barabara kutoka USD 1,000 kwa kilomita hadi USD 100 kwa kilomita, hatua itakayorahisisha ufikisha mawasiliano vijijini. Read More