Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
-
Dunia ikiendelea kushika kasi katika matumizi ya kompyuta kwenye mambo mbalimbali, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hajaiacha Tanzania nyuma kwani anatekeleza ahadi yake ya kukuza sekta ya teknolojia, habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili vijana wengi zaidi waweze kujiajiri, lakini pia kurahisisha na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi. Mei 13 mwaka huu aliongoza utiaji saini miradi miwili ya ujenzi wa minara 758 katika Kata 713 pamoja na mradi wa kuongeza uwezo wa minara 304 ya mawasiliano hatua ambayo itafikisha mawasiliano na huduma ya intaneti kwa Watanzania zaidi ya milioni nane waishio vijijini, maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma hizo. Ili kuwezesha wananchi kunufaika na uwepo wa miundombinu hiyo, Rais Samia ameweka wazi dhamira ya Serikali anayoiongoza kupunguza gharama za intaneti kwa kuanza na kupunguza gharama za uendeshaji kampuni za mawasiliano, hatua ambayo itawezesha kampuni hizo kupunguza gharama za vifurushi, hivyo wananchi wengi, mathali waliojiajiri kupitia TEHAMA, waweza kumudu gharama. Asema kuwa Serikali inalifanyia kazi suala la gharama kubwa za kupitia mkongo kwa Taifa kwenye hifadhi ya barabara na pia Serikali itafikisha umeme kwenye minara ya mawasiliano ili kupunguza gharama za uendeleshaji mnara mmoja kutoka TZS shilingi milioni 1.8 kwa mwezi hadi TZS 400,000, hatua ambazo zitapunguza gharama za vifurushi. Rais Samia anachukua hatua hizi akiamini kuwa uwepo wa mawasiliano bora na intaneti nchi nzima kutachochea ukuaji wa sekta nyingine kama afya, elimu, kilimo, uchumi, haki pamoja na ulinzi na usalama kwani wananchi wataweza kupata taarifa sahihi kwa wakati, watapata njia ya kutoa maoni yao pamoja na kuimarika kwa biashara na uchumi wa kidijitali. Ni wazi pia kuwa, kwa hatua hizi za Rais Samia anaweka mazingira wezeshi ya kuanzisha viwanda vya uzalishaji wa vifaa vya TEHAMA vyenye uwezo wa kutoa ajira kwa wananchi wengi, kudhibiti majanga na kuchochea tafiti katika sekta mbalimbali. Read More