Tanzania na India

  • Mheshimiwa Rais aweka mikakati ya kuvutia uwekezaji wa trilioni 37 ifikapo 2025

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa Tanzania inalenga kusajili miradi ya uwekezaji kutoka nje (FDI) yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 15 (TZS trilioni 37.5) ifikapo mwaka 2025. Ameweka wazi mpango huo wakati akizungumza na wafanyabiashara wakubwa wa India katika jukwaa la uwekezaji la India na Tanzania jijini New Delhi ambapo amesema ili kufanikisha azma hiyo Serikali yake imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuboresha mfumo wa kisheria kwa kuufanya kuwa rafiki zaidi. Ameeleza kuwa Serikali yake inatambua umuhimu wa sekta binafsi na uwekezaji kama vichocheo vya ukuaji wa kiuchumi, hivyo mazingira ya biashara yameboreshwa ili kupanua biashara zilizopo na kuvutia uwekezaji mpya, jambo ambalo ni moja ya malengo ya ziara yake ya kimkakati nchini India. Kama sehemu ya mageuzi makubwa, Tanzania imeboresha matumizi ya teknolojia kuruhusu wawekezaji kusajili miradi popote pale duniani kupitia dirisha la kuhudumia wawekezaji kielektroniki, na hivyo kupata majibu kabla hata ya kutembelea Tanzania. “Tumepiga hatua kutoka kusajili uwekezaji wa dola bilioni 2 [TZS trilioni 5] mwaka 2020 hadi dola bilioni 5 [TZS trilioni 12.5] katika mwaka ulioishia Juni 2023. Lengo letu ni kufikia dola bilioni 15 kwa mwaka ifikapo mwisho wa 2025,” amesema. Tangu mwaka 1997 Tanzania imepokea jumla ya dola bilioni 3.87 za uwekezaji katika miradi 675 kutoka India ambayo imezalisha ajira zaidi ya 61,000, hivyo kufanya India kuwa miongoni mwa wawekezaji watano bora nchini┬áTanzania. Read More

  • Shilingi na Rupia kutumika zaidi katika biashara kati ya Tanzania na India

    Tanzania na India zimefikia makubaliano ya kuongeza matumizi ya fedha za nchi husika katika biashara, badala ya kutegemea dola ya Marekani kama ilvyokuwa hapo awali. Azimio hilo limefikiwa katika mazungumzo kati ya Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi ambapo itawezesha kupunguza mfumuko wa bei tofauti na awali ambapo Tanzania ingelazimika kutumia fedha nyingi kupata dola ya Marekani ili kuagiza bidhaa. Utekelezaji wa uamuzi huo ulishaanza kufanyiwa kazi ambapo hadi sasa biashara yenye thamani ya TZS bilioni 125 imefanyika kwa fedha za nchi husika, hatua inayodhihirisha utayari wa nchi zote kutekeleza makubaliano haya, na sasa hatua inayofuata ni kuongeza matumizi ya fedha hizo. Katika hatua nyingine, India na Tanzania zimebadili uhusiano wao kutoka wa kawaida kidiplomasia kuwa wa mkakati, ambapo nchi zote mbili zimeainisha maeneo mahususi ya kushirikiana yenye maslahi kwa pande zote mbili. Tanzania inatarajia kuendelea kunufaika na ushirikiano wake wa kimkakati na India ikizingatiwa kuwa ni nchi ya tano kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani, ikiwa imepiga hatua katika sekta za afya, TEHAMA, nishatia, miundombinu, ulinzi na usalama ambazo ni kipaumbele kwa Tanzania. Hadi mwaka 2022, kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kilifikia TZS trilioni 7.7, hivyo kuifanya India kuwa mshirika wa tatu kwa ukubwa katika biashara na mwekezaji wa tano kwa ukubwa nchini Tanzania. Read More

  • Ziara ya Mheshimiwa Rais Samia nchini India itakavyofungua fursa kwa Tanzania

    Mwaka 2022 Tanzania iliuza zaidi bidhaa zake nchini India, biashara ambayo ilichangia asilimia 17.3 ya mauzo yote, huku India ikiwa ni nchi ya tatu ambayo Tanzania iliagiza bidhaa nyingi zaidi (asilimia 12.5), takwimu ambazo zinadhihirisha namna mataifa haya yanauhusiano wa kibiashara wenye manufaa kwa pande zote. Katika muktadha wa kukuza zaidi biashara na ushirikiano katika sekta nyingine, Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kimkakati ya kitaifa ya siku tatu nchini India (Oktoba 8-10, 2023) kwa mwaliko wa Serikali ya India, ziara ambayo inatarajiwa kuwa matokeo chanya kwa Tanzania hasa katika sekta za afya, diplomasia, elimu, biashara na uwekezaji, uchumi wa bluu, maji, kilimo na teknolojia. Ziara hiyo ni kubwa kwani inafanyika miaka na tangu kiongozi wa mwisho wa Tanzania kutembelea nchi hiyo, na inatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa miaka 62 wa nchi hizo, ambao chimbuko lake ni Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Waziri Mkuu wa India, Hayati Jawaharlal Nehru. Ziara ya Mheshimiwa Rais nchini India ina malengo makubwa mawili ambayo ni kudumisha, kuimarisha na kuendelea uhusiano uliopo katika sekta takribani 10 na kufungua fursa za biashara na uwekezaji, ikifahamika kuwa India ni moja ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani na ni moja yenye miradi mingi ya uwekezaji nchini. Matarajio ya mafanikio kutokana na ziara hiyo; ELIMU 1. Fursa za mafunzo kwa Watanzania katika nyanja mbalimbali nchini India ambapo kwa kuanzia kutatolewa nafasi 1,000. BIASHARA VYA UWEKEZAJI 1. Kuongezeka kwa uwekezaji nchini hasa viwanda vya kutengeneza simu na vifaa vya kielektroniki AFYA 1. Kuanzishwa kwa taasisi ya upandikizaji wa figo hapa nchini 2. Kuanzishwa kwa kiwanda cha kutengeneza chanjo za binadamu na wanyama 3. Kuongeza ushirikiano kati ya hospitali za Tanzania na India ili kuimarisha uwezo na weledi katika utoaji wa huduma za afya. 4. Kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa (ubora na unafuu)… Read More