Sera ya Fedha

  • Sera nzuri za uchumi za Rais Samia zaleta neema kwa mabenki

    Sera nzuri za uchumi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimi wa Rais Samia Suluhu Hassan zimeendelea kuleta neema kubwa kwenye sekta ya benki nchini, moja ya uthibitisho huo ukiwa ni namna benki za kibiashara zinavyovunja rekodi ya mapato na faida mwaka. Faida ya benki hizo ni ishara ya usimamizi imara wa sera ya fedha inayopelekea uchumi kuwa tulivu na kuwa moja ya uchumi unaokua kwa kasi zaidi duniani pamoja na kutanuka kwa huduma za kifedha zinazoendelea kuifnya Tanzania kusogea karibu zaidi na lengo la kuwa na huduma za kifedha jumuishi. Taarifa za robo ya nne ya mwaka (Oktoba-Desemba 2023) za mabenki ambazo zimechapishwa Januari 2024 zinaonesha kuwa benki mbili kubwa nchini, CRDB na NMB, zinaendelea kuwa vinara wa sekta ya fedha nchini ambapo NMB imevunja rekodi kwa kupata faida ghafi shilingi bilioni 775. Kutokana na mazingira mazuri ya uchumi nchini tangu Rais Samia aingie madarakani NMB imeongeza kiasi cha mikopo inayotoa kwa asilimia 28, hadi kufikia Shilingi trilioni 7.7 mwaka jana, hatua ambayo imewanufaisha maelfu ya wananchi, huku wengine wakinufaika kwa kuwa mawakala na kupata ajira kutokana na kupanuka kwa shughuli za benki hiyo. Kwa upande wa CRDB imeongeza jumla ya mali (total assets) kufikia shilingi trilioni 13.2, amana za wateja (customer deposits) ziliongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 8.8 na mikopo inayotoa imeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 8.8. Benki za biashara zinatarajiwa kuweka rekodi mpya ya faida mwaka huu mpya wa 2024 na kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi kutokana na mazingira mazuri ya uchumi na uwekezaji chini ya serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia. Uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania kuanza kutekeleza Sera ya Fedha kwa kigezo cha riba ya mikopo kwenda benki za kibiashara kunatarajiwa kuinufaisha maradufu Tanzania kwa kuhakikisha ukwasi wa kutosha kwenye shughuli za kiuchumi na kupunguza mfumuko wa bei nchini.… Read More

  • Mageuzi ya Mama Yanaendelea: Benki Kuu yaanza utekelezaji sera mpya ya fedha

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anaendeleza mageuzi chini ya falsafa ya 4R ambapo katika muktadha huo leo Benki Kuu Tanzania (BoT) imetangaza riba elekezi ya asilimia 5.5 ya benki kuu (CBR) kwa benki zote zinazokopa katika benki hiyo ambayo itakatumika kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024 kuanzia leo. Mabadiliko hayo yamefuatia taarifa ya BoT ya Januari 3 mwaka huu ambapo ilitangaza kuanza kutumia mfumo unaotumia riba katika kutekeleza Sera ya Fedha, badala ya mfumo unaotumia ujazi wa fedha, mabadiliko ambayo yanalenga kuongeza ufanisi wa sera ya fedha katika kudhibiti mfumuko wa bei na kuimarisha shughuli za kiuchumi. Utofauti wa mfumo wa zamani na wa sasa wa utekelezaji sera ya fedha (hyperlink) Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba amesema kiwango hicho cha riba kimezingatia lengo la kuhakikisha thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni inaendelea kuwa imara na kinaendana na malengo ya kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unabaki ndani ya lengo la asilimia 5 na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia lengo la asilimia 5.5 au zaidi kwa mwaka 2024. Kupitia mfumo mpya, pamoja na mambo mengine BoT inatekeleza majukumu yake kwa kupandisha au kushusha kiwango cha riba kwa mikopo kwenda benki za kibiashara, ili kuongeza au kupunguza fedha kwenye mzunguko, kudhibiti mfumuko wa bei, kuimarisha thamani ya shilingi au kukabiliana na changamoto nyingine ya kiuchumi kwa wakati husika. Mfumo unaotumia riba unatumika katika nchi zote za Afrika Mashariki kama sehemu ya mkakati wa kuwa na sarafu moja na benki kuu moja ya Afrika Mashariki, pia unatumika katika jumuiya nyingine za kiuchumi ambazo Tanzania ni mwanachama.     Read More

  • Mageuzi ya Mama Yanaendelea: Benki Kuu yatangaza sera mpya ya fedha

    Moja ya falsafa za uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ni Mageuzi (Reforms) ambapo mwaka 2023 yalifanyika makubwa ikiwemo kuanzisha wizara mpya, mageuzi ndani ya wizara, kuanzishwa kwa Tume ya Mipango pamoja na mitaala ya elimu. Mageuzi hayo yanaendelea mwaka 2024 ambapo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuanzia Januari 2024 itaanza kutumia mfumo unaotumia riba katika kutekeleza Sera ya Fedha, badala ya mfumo unaotumia ujazi wa fedha, mabadiliko ambayo yanalenga kuongeza ufanisi wa sera ya fedha katika kudhibiti mfumuko wa bei na kuimarisha shughuli za kiuchumi. Awali BoT katika utekelezaji wa Sera ya Fedha (kusimamia uchumi, mfumuko wa bei, mzunguko wa fedha, thamani ya shilingi na ustawi wa sekta ya fedha) ilifanya hivyo kwa kutumia kiwango cha fedha kilichopo mtaani (kwenye mzunguko), ambapo ilipunguza fedha kwenye mzunguko au kuziongeza kutokana na hali ya wakati huo, mfano mfumuko wa bei. Katika mfumo mpya wa kutumia riba, ambayo itafahamika kama Riba ya Benki Kuu (CBR), BoT itatekeleza majukumu yake kwa kupandisha au kushusha kiwango cha riba kwa mikopo kwenda benki za kibiashara, ili kuongeza au kupunguza fedha kwenye mzunguko au kukabiliana na changamoto nyingine ya kiuchumi kwa wakati husika. Kwa kutumia mfumo wa CBR, benki kuu inatekeleza makubaliano ya kutumia mfumo mmoja wa utekelezaji wa sera ya fedha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za kiuchumi ambazo Tanzania ni mwanachama. Mbali na kuhakikisha ukwasi katika uchumi, kukuza uchumi na kudhibiti mfumuko wa bei, riba hiyo itatumika pia kama kiashiria kimojawapo katika upangaji wa riba zinazotozwa na mabenki na taasisi nyingine za fedha nchini. Hii ikimaanisha kuwa, kadiri riba ya BoT itakavyozidi kuwa ndogo, kutatoa uwezekano mkubwa kwa wananchi kupata mikopo kwa riba nafuu zaidi. Hata hivyo, BoT imesisitiza kuwa riba yake haimaanishi kuweka ukomo katika viwango vya riba zinazotozwa na benki na taasisi nyingine za fedha… Read More