Samia mazishi ya Malkia
-
Septemba 17 mwaka huu Rais Samia aliondoka nchini kuelekea Uingereza kuhudhuria mazishi wa Malkia Elizabeth II baada ya kualikwa kama mmoja wa viongozi wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola. Watu mashuhuri dunianiani takribani 500 walipewa mualiko huo ambao ulizingatia si tu uanachama wa Jumuiya ya Madola lakini pia rekodi ya haki za binadamu kwa kiongozi mwalikwa na nchi anayotoka. Pamoja na mambo na kupata nafasi ya kukutana na viongozi wa mataifa mengine, kuhudhuria mazishi hayo kitendo hicho ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uingereza pamoja na jumuiya hiyo ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa kwa zaidi ya miaka 50 hivi sasa. Kwa mujibu wa takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania, Uingereza ni moja ya wawekezaji wakubwa zaidi Tanzania ikiwa na zaidi ya 30% ya uwekezaji wa Tanzania unaotoka nje (FDI). Mfano kati ya mwaka 1990 hadi 2013 Uingereza iliwekeza Tanzania zaidi ya shilingi Trilioni 8.5 ikizalisha ajira 271,000 kwa Watanzania. Baada ya shughuli hiyo, Rais Samia alielekea nchini Msumbiji kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu ambayo imekuwa na manufaa makubwa kati ya mataifa haya jirani katika kuimarisha ushirikiano wake. Tanzania na Msumbiji zina uhusiano mkubwa wa kihistoria. Nchi hizi zinashea mpaka wa pamoja wa zaidi ya kilometa 800, eneo muhimu katika usalama na uchumi hasa nyakati hizi za ugunduzi wa gesi kwenye mikoa ya kusini mwa nchi yetu. Mwenendo huu unafanya Msumbiji kuwa mbia muhimu wa Tanzania katika uchumi, ulinzi na usalama. Ili kuimarisha ulinzi na usalama ambao ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi, Tanzania na Msumbiji zilitia saini hati mbili za makubaliano, moja ikiwa ni ushirikiano katika masuala ya ulinzi na ya pili ikiwa Uratibu wa Huduma za Utafutaji na Uokoaji ikikumbukwa kuwa Taifa hilo limekuwa likipambana na magaidi katika jimbo la Cabo Delgado ambalo kwa Tanzania limepakana na… Read More