Rais wa China
-
Wafanyabiashara wa kahawa kutoka Tanzania wanaolengeka kuuza kahawa katika soko la China wametakiwa kujisajili kupitia Wizara ya Kilimo nchini Tanzania, ili kukidhi vigezo vya kulifikia soko hilo. Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amenukuliwa akisema kuwa mabadiliko hayo yatarahisisha usajili wa kampuni za Tanzania zenye nia ya kuuza kahawa katika soko la China ambapo awali kampuni nyingi zilikuwa zikipata changamoto kufanya usajili katika mtandao wa Mamlaka ya Forodha ya China (GACC). Hatua hii ni mwendelezo wa fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo Tanzania inaendelea kuzipata tangu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara nchini China ambapo akiwa na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping walishuhudia utiaji saini mikataba 15 ya kimkakati inayolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Hadi sasa kampuni saba zimeshasajiliwa kuingiza kahawa nchini China ikiwa ni pamoja Kilimanjaro Cables (T) Limited, Cotacof Limited, Taylor Winch Tanzania Limited, Dorman (Tanzania) Ltd, Kamal Agro Limited, Redloong Investment Company Limited na Ibero Coffee Trading Company (T) Limited. Uhakika wa soko la kahawa unaweka uhakika ajira na kuzalisha ajira zaidi kupitia mnyororo wa uongezaji thamani kahawa, soko la uhakika kwa wakulima na kuongeza mapato ya Serikali kwa kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi. Wakati Tanzania ikilenga kuongeza uzalishaji wa kahawa kutoka tani 65,235 mwaka 2021/2022 hadi tani 72,000 mwaka 2022/2023, wakati huo huo inalenga kuongeza mauzo yake ya kahawa nchini China na mipango inaendelea kwa wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki katika Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yanayotarajiwa kufanyika Juni 2023 huko Hunan. Read More
-
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu nchini China kuanzia Novemba 2 hadi 4 mwaka huu kufuatia mwaliko wa Rais Xi Jinping suala la uendelezaji wa eneo maalum la kiuchumila Bagamoyo (BSEZ) ni moja ya ajenda atakazozibeba. Mwaliko huo uliokuja siku chache baada ya Rais huyo wa Taifa kubwa la Asia kuchaguliwa kwa muhula wa tatu kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China (CCP) unamfanya Rais Samia kuwa mkuu wa nchi wa kwanza kutoka Afrika kuzuru nchi hiyo. Kufuatia mwaliko huo unaolenga kukuza ushirikiano baina ya mataifa haya mawili, baadhi ya Watanzania wameeleza matamanio yao ikiwa ni pamoja na China iombwe kukarabati reli ya TAZARA na kujenga daraja juu ya bahari kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar. “Ni faraja kusikia Rais Samia amepata mwaliko wa Rais Jinping, ningetamani sana pamoja na mambo mengine hili la kuboresha TAZARA na kujenga daraja yame miongoni mwa vitu ambavyo ataviomba,” amesema Profesa Humphrey Moshi. Kwa upande wake Msemaji Mkuu Serikali, Gerson Msigwa amesema miradi inayofanyika na nchi hizi mbili ni mingi na mingine inakuja na kwamba na kwamba itakapokamilika Watanzania watajulishwa. Kwa mujibu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) hadi January 2021 kwa upande wa Tanzania Bara China ilikuwa ina jumla ya miradi 940 iliyozalisha ajira takribani 120,000. Read More