Rais Samia Suluhu Hassan
-
Desemba 9 kila mwaka Tanzania huadhimisha Siku ya Uhuru ambapo kwa mwaka 2022 maadhimisho hayo yatakuwa ya 61 tangu nchi ipate uhuru kutoka kwa wakoloni. Hata hivyo, maadhimisho hayo yatafanyika tofauti na miaka mingine ambapo hakutakuwa na sherehe za kitafa baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu kuelekeza fedha zilizokuwa zimetengwa kujenga mabweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum. Kufuatia uamuzi huo, TZS milioni 960 zitatumika kujenga mabweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kutoka katika shule nane ambazo ni, Longido (Arusha), Songambele (Manyara), Buhangija (Shinyanga), Goeko (Tabora), Darajani (Singida), Msanzi (Rukwa), Idofi (Njombe) na Mtanga (Lindi). Kwa hatua hii ambayo imepokewa kwa furaha na wananchi wengine, Rais Samia ameendelea kudhihirisha dhamira yake ya boresha mazingira ya kujifunzia kwa watu wenye ulemavu pamoja na kuwawezesha kiuchumi ili kutekeleza dhana ya maendeleo jumuishi. Kwa ufupi, miongoni mwa mambo aliyofanya kwa ajili ya wenye ulemavu ni pamoja na kuwezesha ujenzi wa mabweni 50 kwa wanafunzi wenye ulemavu mwaka 2021, na pia kupitia mkopo wa TZS trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Dunia wa kukabiliana na athari za UVIKO-19,TZS bilioni 5 zilikwenda kuwasaidia wanawake na watu wenye ulemavu. Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilitenga TZS bilioni 3.46 kwa ajili ukarabati wa vyuo vya watu wenye ulemavu ambapo ukarabati wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu vya Luanzari (Tabora) na Masiwani (Tanga) umekamilika, na ukarabati katika vyuo vinne katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Singida na Tabora unaendelea. Mbali na kuzisimamia mamlaka za Serikali kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu, Serikali inaendelea na maboresho ya Sera ya Taifa ya Huduma na Maendeleo ya watu wenye ulemavu, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa saidizi na kuendelea kuhamasisha jamii kuondokana na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu. Asilimia 10 inayotokana na makusanyo ya halmashauri imeendelea kuboresha maisha ya wenye ulemavu ambapo hadi Desemba… Read More
-
Baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka tisa, hatimaye Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza kima cha chini cha mishahara kwa sekta binafsi ambacho kimewezesha watumishi katika kada mbalimbali kushuhudia kuongezwa kwa mishahara yao. Mara ya mwisho kutolewa kwa viwango vya kima cha chini kwa sekta binafsi ilikuwa mwaka 2013, na hivyo watumishi wa sekta hiyo walikuwa wakiisihi Serikali kupandisha viwango vya mishahara ili kuweza kumudu gharama za maisha. Katika viwango ambavyo vitaanza kutumika Januari 2023, mfano, watumishi wa majumbani watalipwa hadi TZS 250,000 kwa mwezi, huku wale wanaofanya katika sekta za huduma ya mawasiliano wakilipwa hadi TZS 500,000. Mbali na nyongeza hiyo, Serikali imeanisha maslahi mengine ambayo watumishi wa sekta binafsi watastahili ikiwa ni pamoja na likizo ya mwaka yenye malipo, posho itakayotolewa mara moja kwa kila miaka miwili na posho nyingine kama watakavyokubaliana. Aidha, dereva wa lori atastahili posho kwa ajili ya umbali wa safari, na kwa mtumishi ambaye kwa sasa anapokea mshahara na maslahi bora kuliko yaliyoanishwa na amri mpya ya kima cha chini, ataendelea kupokea mashahara huo huo ikiwa amejiriwa na mwajiriwa huyo huyo. Kuongezeka kwa viwango hivyo, kwanza ni hatua ya Rais Samia kutimiza ahadi yake ya kuboresha maslahi ya watumishi nchini kwa lengo la kuinua hali zao za kiuchumi ili waweze kumudu gharama za maisha. Pili, nyongeza hiyo ambayo itawagusa Watanzania wengi ambao wameajiriwa kwenye sekta hiyo itawawezesha kumudu gharama za maisha, ambapo awali ilikuwa changamoto kwao, itachochea ukuaji wa uchumi na kukuza sekta nyingine. Read More