Rais Samia fursa
-
Kwa mara ya kwanza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza hadharani kuhusu suala la uwekezaji na uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na sekta binafsi akisisitiza kuwa ni mihimu kama nchi tukatumia fursa zinazojitokeza kabla hazijaondoka au kukwapuliwa na washindani wetu, wakati tukibaki kulumbana. Ametoa rai hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwaapisha viongozi aliowateua karibuni, mmoja wao akiwa ni Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo na kumueleza kwamba moja ya majukumu yake ni kuangalia changamoto na fursa zilizopo nchini ili zitumike vizuri kwa manufaa ya Watanzania. “Wakati sisi tunalumbana, bandari apewe nani, iende, isiende, wenzetu kwa kuona malumbano yetu wame-jump [kimbilia] wamekwenda kule kule […] sasa muone jinsi fursa zinavyokuja na kukimbia haraka haraka, na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia haraka haraka,” amesema. Amesema kazi kubwa iliyopo nchini ni kuleta mabadiliko, lakini kwenye nia safi ya kujenga nchi mabadiliko yanakaribishwa na kwamba licha ya kuwa watu hawajazoea, kwa kwenda nao taratibu na kadiri watakavyoendelea kuona matokeo, watazoea. Kupitia uwekezaji unaokusudiwa bandarini, Tanzania inalenga kuongeza uwezo wa bandari kufadhili bajeti ya nchi kw asilimia 30, kuzalisha ajira zaidi ya 70,000, kuongeza mapato ya Serikali, kupunguza muda wa kuhudumia meli, kuongeza uwezo wa bandari kupokea meli kubwa na kuifanya bandari hiyo kukidhi viwango vya kimataifa. Read More