Mirabaha
-
Machi 2023 Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatimiza miaka miwili tangu achukue usukani wa kuiongoza Tanzania. Watanzania wakitazama nyuma wanaona kuwa amefanya mambo mengi makubwa, ambayo yameboresha taswira ya nchi kikanda na kimataifa pamoja na kuchochea maendeleo ya Mtanzania mmoja mmoja. Sekta ya sanaa haikuwa mbali kufikiwa na mafanikio haya, ambapo kwa sasa wasanii wana mengi ya kuelekeza kwa namna walivyoshikwa mkono. Haya ni baadhi ya mengi aliyoyafanya; Kuwa Mwigizaji namba moja wa filamu Filamu ya kutangaza utalii nchini, Tanzania: The Royal Tour ilikuwa ishara ya kwanza kwa wasanii juu ya namna Rais anavyoitazama kwa umuhimu tasnia ya filamu, na hivyo kuwapa hamasa kubwa wasanii. Tuzo za Muziki Machi 2022 tuzo za muziki zilirejeshwa nchini ikiwa ni miaka sita tangu mara ya mwisho zilipotolewa na sasa zinasimamiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia. Kurejeshwa kwa tuzo hizo kumewapa hamasa wasanii kufanya kazi bora zaidi za sanaa na kuonesha kuwa Serikali inatambua jitihada zao. Tuzo za Filamu Tangu Rais Samia aingie madarakani, tuzo za filamu zimetolewa mara mbili, utaratibu ambao awali haukuwepo, huku Watanzania wakiziona katika nchi nyingine. Mwaka 2021 tuzo zilitolewa jijini Mbeya na mwaka 2022 zilitolewa jijini Arusha, na hivyo kuongeza motisha kwa wasanii kufanya kazi bora kuanzia uandaaji, picha na maudhui. Mirabaha Ombi la miaka mingi la wasanii lilipata majibu ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia ambapo walilipwa fedha kutokana na kazi zao kutumika katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana ambapo TZS milioni 312 zilitolewa. Mikopo kwa Wasanii TZS bilioni 2.5 zilizotengwa kwa ajili ya wasanii kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa zinawawezesha wasanii kuboresha kazi zao na kutoa fursa za ajira kwa vijana zaidi. Rais Samia alifufua mfuko huo ambao uliacha kufanya kazi tangu mwaka 2013, na tayari wasanii wamepewa mikopo ya hadi TZS milioni 40. Tanzania Mwenyeji mashindano ya kimataifa Mashindano ya urembo… Read More