Mazingira ya Biashara

  • Miaka miwili ya Mheshimiwa Rais inavyonufaisha vijana na wanawake kwa mitaji

    Msemo wa Wahenga kuwa Mgaagaa na upwa hali wali mkavu umejirihirisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na manufaa lukuki yanayowafaidisha Watanzania kutokana na safari za nje ya nchi ambapo manufaa hayo awamu hii yanagusa zaidi wanawake na vijana. Ziara zake zimewezesha wafanyabiashara kutoka Ulaya kuja nchini wiki iliyopita ambapo kupitia Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) walitoa mikopo yenye masharti nafuu ya TZS trilioni 1.4 kwenye benki za CRDB, NBC na KCB ambayo itawanufaisha wajasiriamali, pamoja na TZS bilioni 318 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ujasiriamali ya Uholanzi (FMO) na Taasisi ya Ufaransa ya Kufadhili Maendeleo (PROPARCO). Nusu ya fedha za EIB, TZS bilioni 700 zitatumika kukuza biashara za wajasiriamali ambapo TZS bilioni 421 zitaelekezwa kufanikisha miradi na biashara zinazoendeshwa na kusimamiwa na wanawake na TZS bilioni 248 zitatumika kwenye miradi iliyopo kwenye uchumi wa bahari. Kupitia mikopo hiyo, benki za ndani zitakuwa na uwezo wa kutoa mikopo kwa wanawake na wajasiriamali wengi zaidi ambao changamoto ya mitaji imekuwa kubwa kwao. Tukio hili moja ni ushuhuda namna kila safari ambayo Mheshimiwa Rais anafanya nje ya nchi imeleta fursa zaidi za kibiashara na kuvutia wawekezaji nchini. Read More

  • Historia nyingine chini ya Mheshimiwa Rais Samia, faida ya benki yavunja rekodi ikivuka trilioni 1

    Faida ya benki za kibiashara nchini imeongezeka kwa TZS bilioni 400 mwaka 2022 na kuvuka ukomo wa shilingi trilioni moja kwa mara ya kwanza katika historia ya sekta ya fedha nchini Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa za benki ambazo zimetoa taarifa zao za fedha hadi Januari 30 mwaka huu, zinaonesha kuwa zaidi ta TZS trilioni 1.164 zilikusanywa kama faida (net profit) ikiwa ni ongezeko kutoka TZS bilioni 740 zilizokusanywa mwaka 2021. Ongezeko hilo la faida ambalo limeambatana na kupungua kwa mikopo chechefu, kuongezeka kwa kiwango cha fedha kinachowekwa na wateja wa benki pamoja na mikopo kwa wateja kumetokana kuimarika kwa mazingira mazuri ya biashara nchini chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Benki hizo zimesema kuwa ongezeko hilo la faida ni ishara kuwa ajenda ya Serikali ya kukuza biashara inafanya vizuri ambayo inatokana na usimamizi mzuri ikiwemo wa kisera ambazo zinatoa nafasi kwa sekta binafsi kukua. Ukuaji huo unatarajiwa kuwa na matokeo chanya kwa wananchi kwani unaongeza uwezo wa benki kupanua huduma za kifedha kuwafikia wananchi wengi zaidi lakini pia kuongeza kiwango cha mikopo kwenda sekta binafsi ambayo ina mchango mkubwa kwa maendeleo na kuzalisha ajira. Read More