Makamu wa Rais wa Marekani
-
Ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani nchini Tanzania, Kamala Harris si tu imekuwa na matokeo chanya kwenye kuendeleza ushirikiano wa kisiasa, bali pia ina mafanikio kiuchumi ambapo Tanzania imepata TZS trilioni 3.5 zitakazotumika kuiwezesha Tanzania kufikia malengo yake. Fedha hizo zitagusa maisha ya Watanzania kupitia sekta mbalimbali ikiwemo biashara, kuunganishwa na huduma za kidijitali, kuinua ustawi wa wanawake na vijana, kuimarisha usalama wa chakula, uhifadhi wa rasilimali za baharini na maziwa pamoja na afya. Aidha, taarifa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania imeeleza baadhi ya maeneo ambayo wafanyabiashara wa Marekani wamevutiwa nayo ni biashara na uwekezaji hasa katika kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, huduma za afya na madini. Wakati Serikali ya Rais Samia Suluhu ikiweka mkazo kwenye kilimo ambacho kimetoa ajira kwa mamilioni ya Watanzania, TZS bilioni 89 zitatumika kuongeza tija kwenye kilimo hasa cha mbogamboga na matunda, mkazo zaidi ukiwa kwa wanawake na vijana ambao pia ndio wanufaika wa mradi wa Building A Better Tommorow. Read More