Julius Nyerere
-
Tanzania Bara leo imeadhimisha miaka 61 tangu ipate Uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1961, safari ambayo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema “imekuwa safari yenye changamoto na mafanikio mengi ambayo Taifa letu linajivunia.” Katika kuadhimisha siku hii kubwa, mjadala mkubwa huzunguka mchango wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Uhuru, na misimamo aliyoiweka ambayo imekuwa ikitumiwa kama rejea katika kuliongoza Taifa. Mambo mengi ambayo aliyahimiza, Rais Samia ameendelea kuyahimiza na kuyatekeleza ili kuchochea maendeleo ya Watanzania ambayo ni pamoja na; 1. Kupiga vita rushwa Mwalimu Nyerere alikiri kuwa, katika awamu ya kwanza kulikuwa na rushwa, lakini walikuwa wakali sana kuipinga. Serikali yake ilipitisha sheria, mtu akithibitika amepokea au ametoa rushwa, atahukumiwa kifungo kisichopungua miaka miwili na viboko 24 (12 akiingia na 12 akitoka). Vivyo hivyo, Dkt. Samia ameendeleza ari hiyo ya kupinga rushwa akiamini kuwa rushwa inaathiri utoaji haki kwa kumwacha mwenye hatia mtaani na kumfunga asiye na hatia, inawanyima wasio na uwezo fursa ya kupata huduma lakini pia ni kinyume na mafundisho wa kidini. 2. Huduma za Jamii (Elimu, Maji na Afya) Mara baada ya Uhuru, Mwalimu Nyerere aliainisha maadui watatu wa Taifa ambao ambao ni Ujinga, Maradhi na Umasikini. Katika miaka miwili ya Dkt. Rais madarakani amejipambanua kwa kupamba na maadui hao ambapo amewezesha ujenzi wa madarasa zaidi ya 23,000, shule mpya, ajira za walimu, vituo vya afya zaidi ya 230, kujenga na kukarabati hospitali, kufufua na kuanzisha na kukamilisha miradi ya maji pamoja na kuajiri watumishi katika sekta hizo ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi. 3. Kilimo cha kisasa “Tubadili kilimo chetu kusudi kilimo kitusukume kwa sababu hatuna kitu kingine cha kuisukuma nchi hii isipokuwa ni kilimo. Lakini kilimo hiki cha jembe la mkono, kilimo hiki cha kutegemea mvua peke yake, hakina mbolea, hakina dawa, unapanda hovyo hovyo tu, hakitusaidii sana,” alisema Hayati… Read More