Huduma za Afya
-
Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa yaliyoboresha sekta ya afya nchini na kufanya huduma za afya kuwa karibu, bora na nafuu zaidi. Vituo vya kutolewa huduma za afya (zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, mikoa, rufaa na za kanda) 1,061 vimejengwa ambapo ni wastani wa vituo 353 kila mwaka. Ujenzi wa vituo hivi umeenda sambamba na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa ambavyo vimetoa ahueni kubwa kwa wananchi. MAMA amenunua mashine mpya za CT Scan 27, na kufanya mashine hizo nchini kufikia 45, kutoka 13 za awali. Hivi sasa mashine hizo za kiuchunguzi zinapatikana kwenye hospitali zote za rufaa za mikoa. Manufaa makubwa yanaonekana ambapo awali wakazi wa Katavi walilazimika kusafiri zaidi ya kilomita 600 kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Mbeya, lakini sasa huduma hiyo inapatikana mkoani mwao. Tangu tupate uhuru, kwa miaka 61, Tanzania ilinunua mashine za MRI saba, lakini ndani ya miaka mitatu MAMA amenunua mashine sita na kuifanya nchi kuwa na MRI 13 ambazo zimefungwa kwenye hospitali za rufaa za kanda. Mashine za X-Ray ambazo awali hazikupatikana kwa wingi kwenye vituo vya afya, sasa zimejaa tele baada ya kununuliwa kwa Digital X-Ray 199, na kuifanya nchi kuwa namashine 346. MAMA pia amenunua mashine za ultrasound 192 na kuifanya nchi kuwa na mashine 668 ambazo ni muhimu hasa katika kufuatilia ukuaji wa mimba. Vifaa tiba vingine vilivyoongezwa ni Echocardiogram kutoka 95 mwaka 2021 hadi 102 mwaka 2024, Cathlab kutoka moja mwaka 2021 hadi nne mwaka 2024 pamoja na PET Scan ambayo ndiyo ya kwanza nchini mwetu. Vitanda vipya 40,078 vya kulaza wagonjwa, vitanda vipya 1,104 vya vya ICU pamoja na kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa kufikia asilimia 84 kutoka asilimia 58 mwaka 2022. Mageuzi haya yaliyofanyika yamewezesha kupungua kwa vifo vinavyoepukika… Read More
-
Madaktari bingwa 60 wa mifupa na nyonga kutoka Los Angeles, Marekani wanatarajiwa kuwasili nchi Agosti 10 mwaka huu kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu bure ya upasuaji wa magoti na nyonga katika Hospitali ya Rufaa ya Seliani inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Madaktari hao wanakuja kwa mwaliko wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na watawasili nchini kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro (KIA) ambapo wanatarajiwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa 200 kwa wiki mbili ambapo walengwa ni wananchi wenye hali ya chini. Kuja kwa madaktari hao ni fursa kwa wananchi wenye changamoto hizo kupata msaada ambapo pengine wasingeweza kumudu gharama hizo kwani gharama za upasuaji huo ni kubwa ambazo hufika hadi TZS milioni 75, lakini zitatolewa bure na wataalamu hao. Mbali na kutoa huduma hiyo, madaktari hao pia watatoa mafunzo kwa madaktari bingwa wa hospitali hiyo kuhusu upasuaji wa magoti, mifupa na nyonga, ili hata watakapoondoka, huduma hizo ziendelee kutolewa kwa viwango vya juu zaidi. Ili kuwezesha hilo, Serikali sikivu chini ya Mheshimiwa Rais imeruhusu vifaa vitakavyotumika kwenye upasuaji, dawa na vitendea kazi vingine viingizwe nchini bila kulipiwa kodi. Read More