Diplomasia ya Uchumi

  • Diplomasia ya Uchumi: Mheshimiwa Rais Samia avutia wafanyabiashara zaidi wa Norway kuwekeza Tanzania

    Mwanadiplomasia namba moja wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameendelea kutekeleza kwa vitendo Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Diplomasia ya Uchumi, katika ziara zake nje ya nchi kwa kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini pamoja na kukutanisha wafanyabiashara wa ndani na wale wa kimataifa. Matokeo ya mkakati huo yameendelea kuonekana ambapo kwa mwaka 2023 miradi ya uwekezaji iliongezeka kufikia 526 kutoka miradi 293 mwaka 2022, uwekezaji ambapo utazalisha ajira kwa maelfu ya Watanzania, utachochea ukuaji wa biashara, mzunguko wa fedha na kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Katika ziara yake ya kihistoria ya kitaifa nchini Norway Mheshimiwa Rais ameendeleza mkakati huo ambapo akizungumza katika Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Norway ametaja sababu za Tanzania kuwa eneo zuri kwa uwekezaji ikiwa ni pamoja na ukweli kuwa itakuwa moja ya nchi 20 duniani ambazo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi mwaka 2024 kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Aidha, sababu nyingine ni amani chini ya demokrasia imara wa mfumo wa vyama vingi wenye kuzingatia tunu za utawala bora, kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria. Kijiografia, amesema Tanzania inafaa kwa uwekezaji kwani ina Bandari ya Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi, inayohudumia mataifa nane na ina usimamizi madhubuti wa uchumi na sera ya fedha. Rais Samia amesisitiza fursa tano za kipaumbele zikiwemo uwekezaji katika nishati mbadala, kilimo, mafuta na gesi, mifuko ya uwekezaji, miundombinu na usafirishaji. Tanzania na Norway zinaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano ambapo katika mazungumzo ya Rais Samia na viongozi waandamizi wa taifa hilo wamefikia makubaliano ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi kuendana na ukubwa wa historia ya uhusiano uliopo.   Read More

  • Tanzania kuvutia uwekezaji wa trilioni 2.5 toka Indonesia

    Mwanadiplomasia namba moja wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anaendelea kutekeleza kwa vitendo Diplomasia ya Uchumi ambapo sasa Tanzania inakusudia kuvutia uwekezaji wa dola za Kimarekani bilioni 1 (zaidi ya TZS trilioni 2.5) ndani ya miaka michache ijayo, kutoka uwekezaji wa sasa wenye thamani ya TZS bilioni 6.5 ambao umefanyika katika sekta za kilimo, uzalishaji wa viwandani na ujenzi. Ameeleza hayo akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia na ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wafanyabiashara na wawekezaji wa Indonesia sababu zinazowafanya kwanini Tanzania ni sehemu nzuri zaidi kuwekeza. Kwanza amesema ni amani na utulivu uliyopo nchini na Serikali inayofuata misingi ya demokrasia na utawala bora, pili ni eneo la kimkakati la Tanzania ambayo imepaka na nchi nane na ni lango kwa nchi sita kupitia anga, barabara, reli na maji. Aidha, amesema Tanzania inatoa uhakika wa soko la bidhaa zao kwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 61, huku pia ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye watu milioni 281.5, Jumuiya ya Mendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu milioni 390 na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfFTA) lenye watu bilioni 1.2. Tatu ni Tanzania kuwa na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuridhia sheria na mikataba ya kimataifa inayolinda mitaji na uwekezaji wa kigeni. Nne ni utashi wa kisiasa na nafasi ya Serikali kutambua umuhimu wa sekta binafsi kama injini ya maendeleo ya kiuchumi na kuweka msimamo wa kusaidia biashara na wafanyabiashara kukua. Sababu ya tani ni usimamizi imara wa sera ya fedha na uchumi unaowezesha uchumi kuzidi kukua na kufikia viwango vya kabla ya janga la UVIKO19. Kuthibitisha hilo, ripoti ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) imeitaja Tanzania kama moja ya nchi 20 duniani ambazo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi mwaka 2024. Katika ziara yake… Read More

  • Rais Samia anavyotumia Diplomasi ya Uchumi kuchochea maendeleo nchini

    Tanzania imeendelea kutekeleza sera yake ya Diplomasia ya Uchumi inayolenga kujenga na kuimarisha uhusiano wake wa kimataifa na kujenga mahusiano ya kibiashara na kiuchumi na taasisi pamoja na mataifa mengine ili kuchochea maendeleo. Historia nyingine imeandika baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kushiriki na kuhutubia katika Mkutano wa 15 wa BRICS (Brazil, Russia, India, China, South Africa) ambalo ni jukwaa la nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi duniani ambapo pato la Taifa la mataifa hayo ni quadrilioni TZS 63.3, ambapo pia kutokana na kupokea wanachama wapya sita, kuanzia Januari 2024 nchi sita kati ya tisa zinazozalisha mafuta zaidi duniani zitakuwa mwanachama wa jukwaa hilo. Kwa kushiriki kwenye mkutano huo, Tanzania itapata manufaa makubwa kiuchumi na kibiashara kwani kunaiwezesha kujenga mahusiano ya kiuchumi na biashara na nchi hizo zenye nguvu hatua inayoweza kufungua fursa mpya au kupanua fursa zilizopo za kuuza bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya nchi hizo, na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi. Ni wazi pia kuwa mataifa ya BRICS yamepiga hatua kwenye teknolojia, hivyo Tanzania inaweza kujifunza matumizi bora ya teknolojia katika kurahisisha utoaji huduma na kuchochea maendeleo. China ambayo ni mwanachama wa BRICS ni mshirika mkubwa maendeleo wa Tanzania ambapo kwa miezi saba ya mwaka 2023 imeongoza kwa uwezekaji (Foreign Direct Investment) nchini ikiwekeza mtaji wa zaidi ta TZS trilioni 1.2 ambao pamoja na mambo mengi utazalisha ajira kwa maelfu ya Watanzania. Katika mkutano huo Rais Samia alipata nafasi ya kuzungumza na Rais wa China, Xi Jinping, ikiwa ni mara nyingine kwa viongozi hao kukutana baada ya ziara ya Rais Samia nchini China. Mazungumzo hayo huenda yakaongeza uwezekano wa kufadhili miradi muhimu kama miundombinu, nishati, kilimo, na teknolojia, uwekezaji pamoja ushirikiano wa kiusalama. Katika dunia ya sasa, nchi haiwezi kujitenga kama kisiwa, inailazimu kutoka, kukutana na kushirikiana na mataifa mengine ili kufanikisha masuala mbalimbali… Read More