Biashara

  • Shilingi na Rupia kutumika zaidi katika biashara kati ya Tanzania na India

    Tanzania na India zimefikia makubaliano ya kuongeza matumizi ya fedha za nchi husika katika biashara, badala ya kutegemea dola ya Marekani kama ilvyokuwa hapo awali. Azimio hilo limefikiwa katika mazungumzo kati ya Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi ambapo itawezesha kupunguza mfumuko wa bei tofauti na awali ambapo Tanzania ingelazimika kutumia fedha nyingi kupata dola ya Marekani ili kuagiza bidhaa. Utekelezaji wa uamuzi huo ulishaanza kufanyiwa kazi ambapo hadi sasa biashara yenye thamani ya TZS bilioni 125 imefanyika kwa fedha za nchi husika, hatua inayodhihirisha utayari wa nchi zote kutekeleza makubaliano haya, na sasa hatua inayofuata ni kuongeza matumizi ya fedha hizo. Katika hatua nyingine, India na Tanzania zimebadili uhusiano wao kutoka wa kawaida kidiplomasia kuwa wa mkakati, ambapo nchi zote mbili zimeainisha maeneo mahususi ya kushirikiana yenye maslahi kwa pande zote mbili. Tanzania inatarajia kuendelea kunufaika na ushirikiano wake wa kimkakati na India ikizingatiwa kuwa ni nchi ya tano kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani, ikiwa imepiga hatua katika sekta za afya, TEHAMA, nishatia, miundombinu, ulinzi na usalama ambazo ni kipaumbele kwa Tanzania. Hadi mwaka 2022, kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kilifikia TZS trilioni 7.7, hivyo kuifanya India kuwa mshirika wa tatu kwa ukubwa katika biashara na mwekezaji wa tano kwa ukubwa nchini Tanzania. Read More

  • #MiakaMiwiliYaMama na Diplomasia ya Uchumi: Shilingi ya Tanzania kutumika kununua bidhaa nchini India

    Azma ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji inazaa matunda ambapo Tanzania na India zimefikia makubaliano ya kibiashara ambayo yatawezesha wafanyabiashara kutoka pande zote kutumia fedha zao (shilingi na rupia) katika kufanya miamala ya kibiashara. Nafasi hii itarahisisha biashara ambapo India ni moja ya washirika wakubwa wa kibiashara na Tanzania ambapo thamani ya biashara kati ya nchi hizi ni TZS trilioni 10.4 katika mwaka ulioishia Machi 2022. Takwimu zinaonesha kuwa katika mwaka wa kwanza wa Rais Samia, India iliingiza nchini bidhaa zenye thamani ya TZS trilioni 5.3, huku ikipokea bidhaa za TZS trilioni 5.1 kutoka Tanzania. Utaratibu huu mpya si tu utakuza biashara kati ya mataifa haya kufikia lengo la zaidi ya TZS trilioni 13.8 mwaka huu, bali pia utaziwezesha kutunza akiba ya fedha za kigeni ambao sasa hazitahitajika kufanya miamala. Watanzania wanaofanya kazi katika sekta za kilimo na madini watanufaika zaidi kutokana na sekta hizo kuingiza bidhaa zaidi nchini India. Kwa mujibu wa wachumi na wataalamu wa biashara, uamuzi huo pia utaimarisha utabirikaji wa viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni jambo ambalo ni la muhimu sana katika biashara za kimataifa kwani ina usimamizi wa fedha yake tofauti na awali ilipokuwa ikitumia dola za Marekani. Read More

  • #MamaYukoKazini: Asilimia 79 ya vikwanzo vya biashara kati ya Kenya Tanzania vyatatuliwa

    Mauzo ya Tanzania nchini Kenya mwaka 2021 yalikua kwa asilimia 42 kutoka TZS bilioni 537 mwaka 2020 hadi TZS bilioni 929 mwaka 2021, mchango mkubwa ukitokana na kutatuliwa kwa vikwazo vya kibiashara. Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika kipindi tajwa, Tanzania ilishuhudia ongezeko la usafirishaji wa chai, mahindi, ngano, alizeti, mchele, maharagwe, mbogamboga, karatasi, bidhaa za chuma, marumaru, saruji, vioo na bidhaa za vioo, sabuni na vipodozi kwenda Kenya. Akizungumza leo wakati wa ziara ya Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu amesema kwamba wataalamu wa pande zote walibaini uwepo wa vikwazo 68 visivyo vya kikodi, ambapo vikwazo 54 vimetatuliwa na 14 bado havijatatuliwa ambapo wametumia jukwaa kueleza kuwa wamedhamiria kutatua vikwazo vilivyobaki, ili wananchi wa pande zote ambao wana uhusiano wa kindugu, kihistoria na kijiografia wanafanya biashara kwa uhuru kwani kukua kwa biashara kunanufaisha pande zote. “Tumekubaliana ya kwamba mawaziri wakutane, maafisa wengine wakutane, tuyakamilishe, tuyaondoe ili biashara iweze kukua zaidi kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Kenya tukiwa sote ni watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Rais Ruto. Aidha, amesema “wakati wewe [Rais Samia] na Rais Uhuru Kenyatta mlipokuwa mnafanyia kazi vikwazo hivi, watu walidhani Kenya itanufaika zaidi kuliko Tanzania, lakini Tanzania imenufaika zaidi Kenya. Kwa kuangazia takwimu za biashara, Kenya ni mshirika mkubwa wa kibiashara na utalii kwa Tanzania, na hiyo huenda imechangia Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki ambayo Rais Ruto amefanya ziara ya kikazi tangu alipoapishwa Septemba 13 mwaka huu. Read More