Benki ya Maendeleo Afrika

  • AfDB yaunga mkono mkakati wa Rais Samia kwenye kilimo

    Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inakusudia kuipatia Tanzania TZS bilioni 244 kwa ajili ya kutekeleza programu ya kilimo ya ‘Building A Better Tomorrow-Youth Initiative for Agribusiness (BBT-YIA) na kilimo cha mashamba makubwa kwa mwaka 2023/24. Kupitia programu hiyo iliyoasisiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali inakusudia kukuza ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo kwa kuwawezesha kufanya kilimo endelevu cha kibiashara, pamoja na kuondoa dhana kuwa kilimo hakilipi au kilimo sio kwa ajili ya vijana. Mkakati huo unaendana na malengo ya Serikali ya kukuza sekta ya kilimo kwa kuhakikisha wakulima wananufaika kwa kufanya kilimo cha kisasa, kuwezesha kuongeza akiba ya ya chakula nchini, pamoja na kufungua fursa za ajira kupitia sekta za uzalishaji ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi. Benki hiyo anaendelea kuimarisha mnyororo wa thamani wa kilimo ambapo mbali na fedha hizo imewezesha pia ujenzi wa vituo vya mazao mbalimbali mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi, na vitu vingine mkoani Mbeya, Njombe na Iringa kwa ajili ya matunda na mbogamboga ambavyo vitaanza kutumika mwaka ujao wa fedha. Aidha, kutokana na azma ya Rais ya kukuza kilimo, AfDB inakusudia kuendeleza ushirikiano na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ambayo inawezesha ujenzi wa miradi ya umwagiliaji pamoja na uongezaji thamani. Read More