Bandari ya Dar es Salaam

  • Diplomasia ya Uchumi: Mheshimiwa Rais Samia aivuta Zambia kutumia zaidi Bandari ya Dar es Salaam

    Katika kuendelea kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji hasa kutoka nje ya Tanzania kutumia Bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yao, Serikali ya Tanzania imetenga hekta 20 za ardhi katika Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani kwa ajili ya mizigo inayokwenda Zambia, ikiwa ni sehemu ya kurahisisha ufanyaji biashara. Aidha, kwa kutambua umuhimu wa Zambia katika Bandari ya Dar es Salaam, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mizigo inayokwenda nchini humo itakuwa na kipindi cha neema (bure) kirefu zaidi cha kuhifadhi mizigo yao hadi siku 45, ikiwa ni mkakati wa kupunguza msongamano na ucheleweshaji, na hivyo kupunguza gharama za biashara. Mheshimiwa Rais Samia alisema hayo akihutubia katika maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wa Zambia ambapo alikuwa mgeni rasmi, na kuongeza kuwa “tunatarajia kuwa hatua hii itaongeza biashara kati ya nchi zetu mbili na kuzalisha fursa zaidi kwa ajili ya wananchi wetu. Hii ni zawadi kutoka kwa Tanzania mkisherehekea uhuru wenu.” Zambia ni nchi ye pili kwa kupitisha shehena kubwa ya mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam baada ya DR Congo ambapo kwa mwaka 2022 ilipitisha tani milioni 1.98, sawa na asilimia 24 ya mizigo yote iliyokwenda nje. Aidha, ifahamike kuwa asilimia 80 ya mizigo yote inayopita bandari ya Dar es Salaam kwenda nje ya nchi, inapita katika mpaka wa Zambia, jambo linaloifanya nchi hiyo kuwa mshirika wa kimkakati. Uamuzi wa Mheshimiwa Rais Samia umekuja wakati ambapo Tanzania imeanza mageuzi ya kiutendaji katika Bandari Dar es Salaam yatakayowezesha kupokea meli kubwa zaidi na kutoa huduma kwa kasi, hivyo inaihitaji sana Zambia kuwa na imani na mazingira mazuri ya biashara ili iendelee kuitumia bandari hiyo, badala ya kugeukia bandari shindani. Mbali na bandari, Mheshimiwa Rais Samia ameeleza azma ya Serikali yake kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika ukanda wa kusini na ukanda wa mashariki ili kuongeza usambazaji wa umeme… Read More

  • Rais Samia anatimiza ndoto ya Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji Afrika Mashariki na Kati

    Hatua ya Bunge la Tanzania kupitisha azimio la kuridhia ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika uendelezaji na uboreshaji utendaji kazi wa bandari Tanzania ni hatua nyingine kubwa katika mkakati wa Tanzania kuelekea kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji Afrika Mashariki na Kati ndani ya muongo mmoja ujao. Kupitishwa kwa azimio hilo kunaipa nafasi Tanzania kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Dubai kupitia Kampuni ya DP World kuanza majadiliano yanayolenga kuangazia namna ya kushirikiana ili kuongeza ufanisi wa bandari nchini, hasa Bandari ya Dar es Salaam ambayo imekuwa lango la kibiashara kwa nchi za Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini wa Afrika. Kufanikiwa kwa ushirikiano baina ya Serikali hizi mbili kutatimiza ndoto ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ya kuongeza mapato ya bandari kutoka TZS trilioni 7.7 za sasa hadi TZS trilioni 26 ndani ya muongo mmoja, ambayo yataweza kufadhili shughuli za kijamii na kimaendeleo nchini, hivyo kupunguza utegemezi kwa washirika wa maendeleo, jambo ambalo ni msingi katika kudhihirisha Uhuru wa nchi kwenye kupanga na kuamua mambo yake. Mafanikio mengine ambayo Tanzania itayapata ni kuongezeka kwa ajira kutoka nafasi 28,990 za sasa hadi ajira 71,907, kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 hadi saa 24, kupunguza muda wa ushushaji makontena kutoka siku 4.5 hadi siku 2, kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka saa 12 hadi saa 1, kupunguza gharama ya usafirishaji mizigo kutoka nje ya nchi kwenda nchi jirani kwa asilimia 50, pamoja na kuongeza shehena ya mizigo kutoka tani milioni 18 hadi tani milioni 47. Mbali na manufaa hayo, uendelezaji wa bandari pia utachochea ukuaji wa sekta nyingine kama uvuvi, kilimo, ufugaji, viwanda na biashara, usafirishaji (anga, reli, barabara), kiimarisha diplomasia pamoja na Watanzania kunufaika na teknolojia na ujuzi wa uendeshaji wa bandari kisasa. Ili kuendeleza uwazi na uwajibika, Serikali chini… Read More

  • Bandari ya Dar es Salaam yaipita Bandari ya Mombasa kwa ufanisi

    Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuwa na mchango muhimu katika ukuaji wa uchumi, ajira, mapato ya serikali na ukuzaji wa sekta nyingine. Uwezo wake wa kuhudumia mizigo umeendelea kuimarika ambapo makasha yaliyohudumiwa yameongezeka kufikia makasha 63,529 mwaka 2022 kutoka makasha 56,198 mwaka 2021. Ripoti ya Benki ya Dunia (The Container Port Performance Index 2022) imeiweka Bandari ya Dar es Salaam katika nafasi ya kwanza kwa ufanisi Afrika Mashariki ikiipita Bandari ya Mombasa nchini Kenya kutoka na kuimarika kwa ufanisi ambao umepunguza kwa muda ambao meli zinatumia bandarini, jambo ambalo ni muhimu kwa kukuza ushindani wa kibiashara. Katika ripoti hiyo ya dunia imeiweka Bandari ya Dar es Salaam katika nafasi ya 312, huku Mombasa ikiwa nafasi ya 326. Dar es Salaam imepanda kwa nafasi 49 ikitoka nafasi ya 361 mwaka 2021, huku Mombasa ikishuka kwa nafasi 30 kutoka 296 mwaka 2021. Mafanikio hayo ni matokeo ya uwekezaji wa takribani bilioni 1 uliofanyika bandarini ukihusisha upanuzi wa gati namba 1 hadi 7 kwa kuongeza kina kutoka mita 7 hadi mita 14.7 ambazo zinaruhusu meli kubwa yenye uwezo wa kubeba mizigo tani 6,500 kutia nanga. Maboresho mengine ni mashine za kisasa za kupakua mizigo ambazo zinafanyakazi kwa kasi mara mbili ya awali mikakati ambayo sambamba na uimiarisha matumizi ya TEHAMA imeongeza mara mbili idadi ya meli za mizigo zilizokuwa zikihudumiwa bandarini. Aidha, ikilinganishwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), bandari ya Dar es Salaam imepanda kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 9 mwaka 2021 hadi nafasi ya 6 mwaka 2022. Ukuaji huu umeendelea kuwa na matokeo chanya katika kuvutia uwekezaji na biashara, ajira zaidi na kuongeza mapato ya Serikali yanayorudi kuwahudumia Watanzania. Read More