Mama anaiimarisha TAKUKURU mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Ili kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Serikali imekabidhi magari 88 kwa taasisi hiyo.

Magari hayo ambayo yatasambazwa mikoa yote Tanzania yamekabidhiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi hiyo, hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa huku mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea.