March 2024
-
Watumishi wa umma wanayo mengi ya kufurahia na kuonesha katika miaka mitatu ya Mama kwani ametoa majawabu ya changamoto nyingi zilizokuwa za zinawakabili, hali iliyowaongezea motisha na ari ya kuwatumikia wananchi. Kubwa la kwanza ambalo katika kila Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) lilikuwa likisubiriwa tangu mwaka 2016 ni nyongeza ya mishahara. Ndani ya uongozi wa Mama hilo limepatiwa majibu ambapo alipandisha kima cha chini cha mishahara kwa asilimia 23, nyongeza ambayo imewawezesha watumishi wa umma kumudu gharama za maisha ambapo pia aliahidi nyongeza itakuwa kila mwaka. Kwa miaka saba, tangu mwaka 2016 watumishi hao hawakuwa wamepandishwa vyeo. Chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu watumishi 375,319 wamepandishwa vyeo ambapo Serikali imetumia TZS bilioni 85.89, fedha ambazo matumizi yake yamekwenda kuongeza mzunguko wa fedha na kuboresha maisha ya watumishi. Ajira kilikuwa ni kilio kikubwa ambapo mbali na kuweka mazingira rafiki yaliyozalisha maelfu ya ajira kwenye sekta binafsi, Serikali tayari imeajiri watumishi wapya 81,137 katika taasisi mbalimbali za umma. Aidha, imetenga TZS bilioni 230 ambazo zitatumika kuajiri watumishi wapya 47,374 kabla ya mwaka wa fedha 2023/24 kumalizika. Mama amekuwa akisisitiza kuwa yeye na wasaidizi wake si watawala bali ni watumishi wa wananchi. Ili kuhakikisha utumishi uliotukuka ameendelea kutatua changamoto zao ambao amewalipa malimbikizo maelfu ya watumishi. Ndani ya miaka mitatu ya Mama jumla ya watumishi 142,793 wamelipwa malimbikizo yenye thamani ya TZS bilioni 240.7. Kwa lengo la kuendelea kuongeza ufanisi, Serikali imewabadilishia kada watumishi 30,924 ambapo imewalipa mishahara mipya yenye thamani ya TZS bilioni 2.56, mafanikio ambayo hayakuwa yamepatikana katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano kabla ya uongozi wa Mama. Kama hayo hayatoshi, kabla ya mwaka 2023/24 kumalizika, Serikali itakuwa imewapandisha vyeo watumishi 81,561 kwa gharama ya TZS bilioni 90.85, hatua hii mbali na kuongeza motisha kwa watumishi hao, utafungua fursa za ajira mpya. Mbali na maslahi yao, Serikali imeboresha pia maeneo… Read More
-
Kujua unakokwenda ni muhimu ili kuweza kufika, lakini njia ipi uitumie si tu ili ufike, bali ufike kwa wakati, ni muhimu zaidi. Tanzania inalenga kujenga uchumi ambao pamoja na mambo mengine utapunguza kiwango cha umasikini kwa mamilioni ya wananchi, ili kufanikisha hilo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameamua kuitumia sekta ya kilimo ambayo inagusa maisha ya Watanzania saba katika kila Watanzania 10. Takwimu zinaunga mkono uamuzi wake kuwa kilimo kinachangia asilimia 26 ya Pato la Taifa, kinatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 62 ya wananchi, kinachangia dola bilioni 2.3 kwa mwaka, hutoa malighafi za kiwandani kwa asilimia 65 na kinahakikisha usalama wa chakula nchini kwa asilimia 100. Hili ni wazi kuwa mageuzi ya kweli katika maisha ya wananchi ni lazima yahusishe kilimo, siri ambayo MAMA anaijua. Ni vigumu kueleza yote yaliyofanyika katika miaka mitatu ya MAMA madarakani kwani ni mengi mno. Baadhi ya mambo hayo ni bajeti ya kilimo imeongezwa zaidi ya mara tatu kutoka TZS bilioni 294 mwaka 2021/22 hadi TZS bilioni 970 mwaka 2023/24, ongezeko ambalo ni msingi wa mageuzi yote kwenye sekta hiyo. Ongezeko hilo limepelekea mafanikio makubwa katika uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia ambapo matumizi ya mbolea yameongezeka kutoka tani 363,599 hadi tani 580,628 kutokana na mpango wa mbolea ya ruzuku. Matumizi ya mbolea yameongeza uzalishaji wa mazao ulioiwezesha nchi kuongeza mauzo ya nje takribani mara mbili kutoka TZS trilioni 3 hadi TZS trilioni 5.7. Mageuzi yaliyofanyika yamemfikia mkulima katika ngazi ya kijiji kupitia vifaa vilivyotolewa kwa maafisa ugani wa halmashauri 166 zikiwemo pikipiki 5,889, vishkwambi 805, seti za vifaa vya kupimia udogo 143 ambavyo vimemwezesha mkulima kulima kisasa akijua atumie mbegu gani na mbolea gani kwenye aina fulani ya udongo. Kama hayo hayatoshi kuondoa kilimo cha mazoea tena cha msimu, MAMA amewekeza katika kilimo umwagiliaji kwa kuongeza bajeti ya umwagiliaji kwa takribani mara nane kutoka TZS… Read More