June 2023
-
Mageuzi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii anayoendelea kuyafanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa manufaa ya Watanzania wote yameendelea kuwavutia wengi wanaopongeza juhudi zake ambapo mwisho wa wiki Msimamizi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bi. Samantha Power ametoa pongezi zake kwa Rais kwa juhudi zake katika kuendeleza mageuzi ya kidemokrasia na ushirikishwaji wa wananchi. Bi. Power amesema kuwa jitahda za Rais Samia zimewezesha Tanzania kupanua ushirikiano wa kimaendeleo na kuifanya iwe rahisi kwa sekta binafsi ya Marekani kuizingatia Tanzania kama mahali pazuri pa kuwekeza. Aidha, ameeleza kuwa kazi ya kuvutia uwekezaji na biashara itakuwa rahisi Tanzania ikiendelea na mageuzi katika maeneo ya utawala na kusisitiza kuwa makubaliano ya malengo ya maendeleo yanatoa fursa ya kuongeza mara mbili zaidi mafanikio yaliyopatikana katika ushirikiano imara kati ya nchi hizo mbili. Amempongeza Rais pia kwa ushirikishwaji wa wananchi, hususani vijana, katika shughuli za maendeleo akisema tofauti na maeneo mengine ambayo vijana huchukuliwa kama Taifa la kesho, kwa Tanzania vijana ndio Taifa la sasa. Kupitia ujenzi wa uchumi shirikishi kwa kutumia teknolojia ameeleza imani yake kuwa Tanzania itanufaika kwani wananchi wake wengi ni vijana. Pongezi zaidi amezitoa kwa Rais kwa namna Tanzania inavyotumia teknolojia kupitia Programu ya M-Mama inayowawezesha wajawazito kupata huduma zinazowawezesha kuokoa maisha yao, hasa katika maeneo ya vijijini ambapo hadi sasa imepunguza vifo vya uzazi kwa asilimia 38. Read More
-
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Serikali imesaini mikataba saba ya ujenzi wa barabara kuu ambazo zina jumla ya urefu wa kilomita 2,035, ambapo kwa miaka ya nyuma ili kuwa ikijenga wastani wa kilomita 200 hado 250 kwa mwaka. Barabara hizo ambazo zitapita kwenye mikoa 13 zitaboresha mtandao wa barabara nchini na kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji na kuchochea uzalishaji katika maeneo zinapopita hatua ambayo itaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla, pamoja na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine. Zaidi ya Watanzania 20,000 watapata ajira za moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wahitimu wa vyuo vikuu kwa masharti ya mikataba ya ujenzi na usimamizi ambapo wahitimu wasiopungua 70 watapata ajira. Barabara zikazojengwa pamoja na mikoa ambayo zitapita; i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo; ii) Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa; iii) Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki; iv) Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma; v) Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya… Read More
-
Dhamira za dhati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza sekta binafsi na kuhakikisha inashiriki katika kuchochea maendeleo ya wananchi inazidi kudhihirika kufuatia marekebisho yaliyofanyika kwenye Sheria ya Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2023 ili kuondoa changamoto zilizosababisha ushiriki hafifu wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa utaratibu wa ubia. Maboresho yaliyofanyika yataongeza kasi ya ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kupunguza muda wa maandalizi ya miradi na hivyo kuharakisha utekelezaji wa miradi ya PPP, hatua ambazo zitaipunguzia Serikali mzigo wa kibajeti sambamba na kukuza sekta binafsi. Changamoto zilizotatuliwa ni pamoja na sheria kutotoa haki kwa wabia kutoka sekta binafsi kuwasilisha migogoro kwenye mahakama za kimataifa kwa utatuzi, kutoainisha aina ya misaada ya kifedha (public funding) itakayoidhinishwa kupitia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada. Nyingine ni sheria kutoruhusu mamlaka za Serikali kufanya ununuzi wa moja kwa moja wa mbia kutoka sekta binafsi kwa ajili ya kutekeleza miradi inayoibuliwa na mamlaka hizo na kutoweka masharti kwa mwekezaji kutoka sekta binafsi aliyeshinda zabuni ya kutekeleza mradi wa PPP kuunda Kampuni. Tayari Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi ikiwemo barabara (Expressway) kutoka Kibaha – Chalinze – Morogoro, mradi ambao utaweka historia ya kuwa mradi mkubwa zaidi wa barabara kujengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi. Read More
-
Hatua ya Bunge la Tanzania kupitisha azimio la kuridhia ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika uendelezaji na uboreshaji utendaji kazi wa bandari Tanzania ni hatua nyingine kubwa katika mkakati wa Tanzania kuelekea kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji Afrika Mashariki na Kati ndani ya muongo mmoja ujao. Kupitishwa kwa azimio hilo kunaipa nafasi Tanzania kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Dubai kupitia Kampuni ya DP World kuanza majadiliano yanayolenga kuangazia namna ya kushirikiana ili kuongeza ufanisi wa bandari nchini, hasa Bandari ya Dar es Salaam ambayo imekuwa lango la kibiashara kwa nchi za Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini wa Afrika. Kufanikiwa kwa ushirikiano baina ya Serikali hizi mbili kutatimiza ndoto ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ya kuongeza mapato ya bandari kutoka TZS trilioni 7.7 za sasa hadi TZS trilioni 26 ndani ya muongo mmoja, ambayo yataweza kufadhili shughuli za kijamii na kimaendeleo nchini, hivyo kupunguza utegemezi kwa washirika wa maendeleo, jambo ambalo ni msingi katika kudhihirisha Uhuru wa nchi kwenye kupanga na kuamua mambo yake. Mafanikio mengine ambayo Tanzania itayapata ni kuongezeka kwa ajira kutoka nafasi 28,990 za sasa hadi ajira 71,907, kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 hadi saa 24, kupunguza muda wa ushushaji makontena kutoka siku 4.5 hadi siku 2, kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka saa 12 hadi saa 1, kupunguza gharama ya usafirishaji mizigo kutoka nje ya nchi kwenda nchi jirani kwa asilimia 50, pamoja na kuongeza shehena ya mizigo kutoka tani milioni 18 hadi tani milioni 47. Mbali na manufaa hayo, uendelezaji wa bandari pia utachochea ukuaji wa sekta nyingine kama uvuvi, kilimo, ufugaji, viwanda na biashara, usafirishaji (anga, reli, barabara), kiimarisha diplomasia pamoja na Watanzania kunufaika na teknolojia na ujuzi wa uendeshaji wa bandari kisasa. Ili kuendeleza uwazi na uwajibika, Serikali chini… Read More
-
Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anaiunda upya Tume ya Mipango ambayo itakuwa chini ya Rais ikiwa na jukumu la kubuni, kupanga, kuratibu na kusimamia mipango ya maendeleo ili kuwa na mfumo jumuishi wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa vipaumbele vya maendeleo ya Taifa. Kuunda upya kwa tume hiyo na kuiweka chini ya Rais ni kuendelea kuyaishi maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye kwa mara ya kwanza alianzisha mwaka 1962 ikiwa ni idara ambapo wakati wa uanzishaji wake walisema “Nakusudia kuanzisha idara mpya, idara ya mipango ya maendeleo, idara hiyo itakuwa chini yangu mwenyewe.” Uamuzi wa Rais kurejesha tume hiyo utawezesha uwepo wa utaratibu wa kupanga pamoja mipango ya kisekta, hususani sekta zenye majukumu yanayotegemeana na kuwa na mfumo wa kisheria na chombo mahsusi cha kusimamia uandaaji, utekkelezaji wa mipango ya maendeleo, utafiti na kuishauri Serikali kuhusu vipaumbele vya maendeleo ya Taifa. Majukumu haya kwa sasa yanatekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango, lakini kumekuwepo na changamoto ya miradi inayoendana kutekelezwa kwa nyakati tofauti sehemu husika, mfano barabara inajengwa baada ya muda inavunjwa ili kupitisha bomba la maji. Hivyo kuwepo kwa tume maalum chini ya ofisi ya Rais kutaondoka mkanganyiko huo ili miradi kama hiyo itekelezwe kwa wakati mmoja ili kuleta ufanisi na kuipunguzia serikali gharama zisizo za lazima. Aidha, tofauti na tume iliyokuwepo awali ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa hati idhini (instruments) tume mpya itakuwa na hadhi ya kisheria ambayo itaipa tume nguvu zaidi na kulinda mawazo yanayotolewa na kuleta utofauti katika mfumo wa uendeshaji. Read More