September 2022
-
Wanafunzi 640 wanatarajiwa kunufaika na mpango wa ufadhili wa masomo ya chuo kikuu, Samia Scholarship, utakaoanza mwaka wa masomo 2022/23 kwa kutoa ufadhili wa asilimia 100 kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi na hisabati kwenye mtihani wa kidato cha sita. Licha ya kuwa wanafunzi 640 (wavulana 396 na wasichana 244) wamekidhi kigezo cha ufaulu cha kupata ufadhili, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeainisha vigezo vingine vitakavyozingatiwa ambavyo ni; 1. Lazima awe Mtanzania 2. Awe amefaulu ufaulu wa juu katika mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2022 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN). 3. Mwombaji awe amepata udahili kusoma fani ya teknolojia, hisabati, uhandisi na elimutiba katika chuo kikuu kinachotambuliwa na Serikali hapa nchini. 4. Aombe ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa. Mpango huu utakuwa na manufaa mbalimbali ambayo ni; 1. Kuchochea ari ya wanafunzi kupenda na kusoma masomo ya sayansi 2. Kutoa ahueni kubwa wazazi ambao pengine wangelazimika kuuza mali zao ili kumudu gharama za kusomesha watoto fani za sayansi. 3. Kukuza sekta ya sayansi na teknolojia nchini ili kunufaika zaidi na mapinduzi ya nne ya viwanda. 4. Kuongeza idadi ya wasichana/wanawake kwenye fani za sayansi ambao wamebaki nyuma kutokana na mifumo na imani potofu za jamii. Ufadhili huo ambao utazingatia vigezo vya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) utagharamia maeneo yafuatayo; Ada ya mafunzo, posho ya chakula na malazi, posho ya vitabu na viandikwa, mahitaji maalum ya vitivo, mafunzo kwa vitendo, tafiti, vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na bima ya afya. Wanafunzi watakaofadhiliwa watagharamiwa kwa miaka mitatu hadi mitano kulingana kila mmoja programu aliyodahiliwa, na atatakiwa kuwa na ufaulu usiopungua GPA ya 3.8 katika mwaka wa masomo ili kukidhi kigezo cha kuendelea na ufadhili. Read More
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameidhinisha Shilingi za Kitanzania bilioni 150 kwa ajili ya ruzuku ya mbolea. Kufuatia hatua hii, wakulima 956,920 katika maeneo mbalimbali nchini wameanza kunufaika na mbolea ya gharama nafuu. Hatua hii ni sehemu ya malengo ya kisera ya serikali katika kumpunguzia mkulima gharama na kuongeza uzalishaji. Kilimo kinachangia takribani asilimia 30 ya pato ghafi la Taifa ikiwa na maana kwamba katika kila shilingi mia moja ya pato ghafi la Taifa walau shilingi 30 inachangiwa na kilimo. Mbali na hatua hii ya kupunguza bei ya mbolea, Mheshimiwa Rais ameendelea kuwa muumini mkubwa wa mageuzi katika kilimo akiongoza serikali katika kasi ya kuhakikisha pembejeo zinapatikana, ardhi inarasimishwa na uhuru wa mkulima kuuza mazao yake kwa bei ifaanyo. Uamuzi mkubwa pia wa kisera na kibajeti kuleta mapinduzi ya kilimo umefanyika katika Bajeti ya Mwaka huu 2022/23 ambapo Mhe. Rais Samia ongeza bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 250 hadi shilingi bilioni 990. Wanufaika wakubwa katika ruzuku hii ya kwanza ya mbolea ni mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Rukwa, Arusha na Songwe. #MamaYukoKazini #KaziInaendelea Read More
-
Septemba 17 mwaka huu Rais Samia aliondoka nchini kuelekea Uingereza kuhudhuria mazishi wa Malkia Elizabeth II baada ya kualikwa kama mmoja wa viongozi wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola. Watu mashuhuri dunianiani takribani 500 walipewa mualiko huo ambao ulizingatia si tu uanachama wa Jumuiya ya Madola lakini pia rekodi ya haki za binadamu kwa kiongozi mwalikwa na nchi anayotoka. Pamoja na mambo na kupata nafasi ya kukutana na viongozi wa mataifa mengine, kuhudhuria mazishi hayo kitendo hicho ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uingereza pamoja na jumuiya hiyo ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa kwa zaidi ya miaka 50 hivi sasa. Kwa mujibu wa takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania, Uingereza ni moja ya wawekezaji wakubwa zaidi Tanzania ikiwa na zaidi ya 30% ya uwekezaji wa Tanzania unaotoka nje (FDI). Mfano kati ya mwaka 1990 hadi 2013 Uingereza iliwekeza Tanzania zaidi ya shilingi Trilioni 8.5 ikizalisha ajira 271,000 kwa Watanzania. Baada ya shughuli hiyo, Rais Samia alielekea nchini Msumbiji kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu ambayo imekuwa na manufaa makubwa kati ya mataifa haya jirani katika kuimarisha ushirikiano wake. Tanzania na Msumbiji zina uhusiano mkubwa wa kihistoria. Nchi hizi zinashea mpaka wa pamoja wa zaidi ya kilometa 800, eneo muhimu katika usalama na uchumi hasa nyakati hizi za ugunduzi wa gesi kwenye mikoa ya kusini mwa nchi yetu. Mwenendo huu unafanya Msumbiji kuwa mbia muhimu wa Tanzania katika uchumi, ulinzi na usalama. Ili kuimarisha ulinzi na usalama ambao ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi, Tanzania na Msumbiji zilitia saini hati mbili za makubaliano, moja ikiwa ni ushirikiano katika masuala ya ulinzi na ya pili ikiwa Uratibu wa Huduma za Utafutaji na Uokoaji ikikumbukwa kuwa Taifa hilo limekuwa likipambana na magaidi katika jimbo la Cabo Delgado ambalo kwa Tanzania limepakana na… Read More
-
Tanzania inatimiza miaka 30 tangu turejee rasmi katika siasa za mfumo wa vyama vingi katika kipindi hicho, Taifa letu limepitia kipindi cha furaha, majonzi, misukusuko na changamoto zote wakati Taifa linapoanza njia mpya. Jambo hili si jepesi, kwa sababu nyakati hizo hazikuwa rahisi duniani kote. Miaka ambayo Tanzania ilirejea katika mfumo huo ilikuwa migumu. Miaka ya mwanzoni ya 1990, ndiyo ilishuhudia changamoto kama vile kuanguka kwa iliyokuwa Urusi, vita vya wenyewe kwa wenyewe Afrika, mauaji ya Kimbari na migogoro mingi ya kisiasa na kiuchumi katika nchi zinazoendelea kama yetu Lakini Watanzania walipita wakati wote huo, wakiwa wamoja na tumeendeleza utamaduni huo miaka 30 baadaye. Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza wote, na ni matumaini yangu makubwa, kwamba viongozi watakaokuja miaka 50 hadi 100 baadaye wataendelea kuongoza nchi iliyo moja na wananchi wasiobaguana na kupigana, hata kama wanapingana kuhusu namna ya kuendesha nchi yao. Ni vizuri kuzungumza kuhusu nana tulivyoingia katika mfumo huu. Rais Ali Hassan Mwinyi aliunde Tume ya Jaji Francis Nyalali iliykuja na majibu kwamba ni azilimia 20 tu ya Watanzania ndio walitaka mfumo wa vyama vingi. Ni busara ya Mzee Mwinyi na viongozi wenzake wa wakati huo walioamua kusikiliza wachache. Kama wazee wetu wangesubiri mpaka asilimia 80 itake vyama vingi ndiyo tukubali pengine leo tusingekuwa tulipo. Hili ni miongoni mwa mafunzo makubwa kwa wanasiasa wa kizazi changu na watakaokuja baadaye. Kwenye jambo la maslahi ya nchi, maarifa na busara ndiyo muhimu kuliko namba. Kutoka kuwa na chama kimoja cha siasa – Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa tuna vyama vilivyosajiliwa 20. Badala ya kusikia sauti moja. Badala ya kusikia sauti moja na wakati mwingine tukisema “Zidumu Fikra za Mwenyekiti”. Sasa Watanzania wanasikia kuhusu fikra za sauti tofauti. Kwa bahati nzuri, hata Mwenyekiti Mao alipata kusema “acha maua 100 yamee kwa pamoja”. Kipekee kabisa, nitumie nafasi hi kuwapongeza wote waliofanikisha safari… Read More