Wizara ya Nishati
-
Oktoba 17 mwaka huu ilikuwa siku ya historia kwa Tanzania, hasa mkoa wa Kigoma baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzima jenereta la kuzalisha umeme la Kasulu na kuwasha umeme wa gridi ya Taifa uliofika mkoani humo kwa mara ya kwanza. Jenereta la Kasulu ambalo lilikuwa likizalisha umeme megawati 3.75 zilizotumika wilayani Kasulu na Buhigwe lakini hazikutosheleza ni moja ya majenereta matano yaliyozimwa mengine yakiwa ni Loliondo, Biharamulo, Kibondo na Ngara. Kuzimwa kwa mtambo wa Kasulu na kuwashwa umeme wa gridi ya Taifa kutabadilisha kabisa hadithi ya mkoa wa Kigoma pamoja na maisha ya wakazi wa mkoa huo kwa namna tofauti pamoja na uendeshaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). 1. Kutaipunguzia TANESCO mzigo wa kuendesha mitambo hiyo ambapo kwa mwaka kwa mkoa wa Kigoma ilikuwa ikizalisha umeme kwa gharama ya TZS bilioni 52 huku ikikusanya TZS bilioni 14 tu, hivyo kupelekea kutenga zaidi ya TZS bilioni 38 kila mwaka ili kuhakikisha wananchi wa Kigoma wanapata nishati hiyo muhimu. Uwepo wa umeme wa gridi utaiwezesha Serikali kuelekeza fedha hizo kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo na kijamii kama vile shule, afya, maji na miundombinu. 2. Uhitaji wa umeme kwa sasa katika mkoa wa ni megawati 14, lakini umeme uliopelekwa ni megawati 20, hivyo kuufanya kuwa na ziada, huku miradi mingine ya kuongeza umeme ikiendelea. Umeme wa uhakika utavutia wawekezaji hasa wa viwanda vikubwa kuwekeza mkoani humo katika viwanda vya kuchakata mawese na samaki, ambapo awali ingekuwa vigumu kutokana na kutokuwepo umeme wa kutosheleza. 3. Viwanda vikubwa na vidogo vitakavyoanzishwa kwa uwepo wa umeme vitawezesha wakazi wa mkoa huo, hasa vijana na wanawake kupata ajira za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja zitalazobadili maisha yao, na kuchangia ukuaji wa mkoa na Taifa. 4. Kukosekana kwa umeme wa uhakika kuliathiri hali ya maisha ya wakazi wa mkoa huo kutokana na… Read More