Uchaguzi Huru na Haki
-
Watanzania mwaka huu na mwaka 2025 watatimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi ambao watawaongoza kwa miaka mitano ijayo, ambapo katika mchakato wote huo, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameahidi kuwa misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, haki vitadumishwa ili wananchi wapate viongozi wanaostahili. Ili kutimiza azma hiyo, ameeleza kuwa mabadiliko ya sheria zinazosimamia vyama vya siasa na uchaguzi yamefanyika kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na wananchi na wadau mbalimbali baada ya kuunda kikosi kazi huru kupitia mazingira ya kisiasa nchini, ambapo kwa kiasi kikubwa maoni yaliyotolewa yamehimiza kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Maoni mengine ambayo tayari yamefanyiwa kazi ni kubadili jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuakisi uhuru wake. Aidha, amesema baadhi ya maoni yaliyotolewa yalikinzana na Katiba ya nchi, na kuahidi kuwa yatafanyiwa kazi wakati wa maboresho ya kati. “Maboresho haya yatawezesha uchaguzi kufanyika katika mazingira huru na ya haki. Muwe na uhakika kuwa amani na utulivu vitatawala wakati wote kwa gharama yoyote, amesema Rais Samia Suluhu. Akizungumza katika sherehe za mwaka mpya 2024 kwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, amewahakikishia kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo kwa kuzingatia Katiba, tunu za taifa, usawa na umoja wetu wa kitaifa na kwamba watafuta sheria, na uingiliaji wa uchaguzi kutoka nje hautakuwepo. Read More