Tanzania na Indonesia
-
Mwanadiplomasia namba moja wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anaendelea kutekeleza kwa vitendo Diplomasia ya Uchumi ambapo sasa Tanzania inakusudia kuvutia uwekezaji wa dola za Kimarekani bilioni 1 (zaidi ya TZS trilioni 2.5) ndani ya miaka michache ijayo, kutoka uwekezaji wa sasa wenye thamani ya TZS bilioni 6.5 ambao umefanyika katika sekta za kilimo, uzalishaji wa viwandani na ujenzi. Ameeleza hayo akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia na ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wafanyabiashara na wawekezaji wa Indonesia sababu zinazowafanya kwanini Tanzania ni sehemu nzuri zaidi kuwekeza. Kwanza amesema ni amani na utulivu uliyopo nchini na Serikali inayofuata misingi ya demokrasia na utawala bora, pili ni eneo la kimkakati la Tanzania ambayo imepaka na nchi nane na ni lango kwa nchi sita kupitia anga, barabara, reli na maji. Aidha, amesema Tanzania inatoa uhakika wa soko la bidhaa zao kwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 61, huku pia ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye watu milioni 281.5, Jumuiya ya Mendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu milioni 390 na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfFTA) lenye watu bilioni 1.2. Tatu ni Tanzania kuwa na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuridhia sheria na mikataba ya kimataifa inayolinda mitaji na uwekezaji wa kigeni. Nne ni utashi wa kisiasa na nafasi ya Serikali kutambua umuhimu wa sekta binafsi kama injini ya maendeleo ya kiuchumi na kuweka msimamo wa kusaidia biashara na wafanyabiashara kukua. Sababu ya tani ni usimamizi imara wa sera ya fedha na uchumi unaowezesha uchumi kuzidi kukua na kufikia viwango vya kabla ya janga la UVIKO19. Kuthibitisha hilo, ripoti ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) imeitaja Tanzania kama moja ya nchi 20 duniani ambazo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi mwaka 2024. Katika ziara yake… Read More