Sherehe za Uhuru
-
Desemba 9 kila mwaka Tanzania huadhimisha Siku ya Uhuru ambapo kwa mwaka 2022 maadhimisho hayo yatakuwa ya 61 tangu nchi ipate uhuru kutoka kwa wakoloni. Hata hivyo, maadhimisho hayo yatafanyika tofauti na miaka mingine ambapo hakutakuwa na sherehe za kitafa baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu kuelekeza fedha zilizokuwa zimetengwa kujenga mabweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum. Kufuatia uamuzi huo, TZS milioni 960 zitatumika kujenga mabweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kutoka katika shule nane ambazo ni, Longido (Arusha), Songambele (Manyara), Buhangija (Shinyanga), Goeko (Tabora), Darajani (Singida), Msanzi (Rukwa), Idofi (Njombe) na Mtanga (Lindi). Kwa hatua hii ambayo imepokewa kwa furaha na wananchi wengine, Rais Samia ameendelea kudhihirisha dhamira yake ya boresha mazingira ya kujifunzia kwa watu wenye ulemavu pamoja na kuwawezesha kiuchumi ili kutekeleza dhana ya maendeleo jumuishi. Kwa ufupi, miongoni mwa mambo aliyofanya kwa ajili ya wenye ulemavu ni pamoja na kuwezesha ujenzi wa mabweni 50 kwa wanafunzi wenye ulemavu mwaka 2021, na pia kupitia mkopo wa TZS trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Dunia wa kukabiliana na athari za UVIKO-19,TZS bilioni 5 zilikwenda kuwasaidia wanawake na watu wenye ulemavu. Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilitenga TZS bilioni 3.46 kwa ajili ukarabati wa vyuo vya watu wenye ulemavu ambapo ukarabati wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu vya Luanzari (Tabora) na Masiwani (Tanga) umekamilika, na ukarabati katika vyuo vinne katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Singida na Tabora unaendelea. Mbali na kuzisimamia mamlaka za Serikali kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu, Serikali inaendelea na maboresho ya Sera ya Taifa ya Huduma na Maendeleo ya watu wenye ulemavu, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa saidizi na kuendelea kuhamasisha jamii kuondokana na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu. Asilimia 10 inayotokana na makusanyo ya halmashauri imeendelea kuboresha maisha ya wenye ulemavu ambapo hadi Desemba… Read More