Ruzuku ya Mafuta

  • Mheshimiwa Rais Samia alivyotoa ahueni kwa wananchi kupitia ruzuku ya mafuta

    Ruzuku ya Serikali kwenye mafuta iliyoanza kutolewa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa ahueni kubwa kwa wananchi kutokana na bei ya mafuta kuendelea kupungua katika soko la ndani. Takwimu zinaonesha kuwa bei ya petroli kwa kipindi hicho imepungua kwa wastani wa asilimia 14 kwa petroli iliyoingizwa nchini kupitia bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara. Kuanzia Agosti hadi Januari 2023 bei ya petroli iliyopokelewa Bandari ya Dar es Salaam baada ya ruzuku imepungua kutoka TZS 3,410 hadi TZS 2,819. Wakati huo huo, bei ya petroli kupitia bandari ya Tanga imeshuka kutoka TZS 3,435 hadi TZS 2,989, huku petroli iliyopita Bandari ya Mtwara ikishuka kutoka TZS 3,393 hadi TZS 2,993. Kuendelea kushuka kwa bei ya mafuta nchini ni matokeo ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ili kumpa kila mwananchi nafuu ya maisha. Ruzuku ya TZS 100 bilioni ilianza kutumika kuanzia Juni 1, 2022 ambapo wadau na wananchi wamekiri kwamba imekuwa ahueni kubwa kwao, hasa ikilinganishwa na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania ndio ina bei ndogo zaidi ya petroli. Read More